Mzee una fix wewe 😃
haha! kama mimi nina fix jana mmiliki wa telegram ameachiwa baada yakukubali kuwa anatoa taarifa za watumiaji wa telegram!, takribani wiki 3 telegram ilifungiwa ikawa huwezi kutumia bila vpn haya kama unayo fungua sasahivi bila vpn uone kama kitu hakifanyi kazi..
😅

narudia tena hakuna serikali itakaa hivihivi bila kutafuta taarifa,wanapozitaka watazipata na hata ukiwazuia watatumia gharama yoyote!,shida sisi raia huku chini huwa tunahadaiwa na vitu vyakipuuzi mno nawakati uhalisia tofauti!.
sasa nyie endeleeni kujifunika giza!
 
haha! kama mimi nina fix jana mmiliki wa telegram ameachiwa baada yakukubali kuwa anatoa taarifa za watumiaji wa telegram!, takribani wiki 3 telegram ilifungiwa ikawa huwezi kutumia bila vpn haya kama unayo fungua sasahivi bila vpn uone kama kitu hakifanyi kazi..
😅

narudia tena hakuna serikali itakaa hivihivi bila kutafuta taarifa,wanapozitaka watazipata na hata ukiwazuia watatumia gharama yoyote!,shida sisi raia huku chini huwa tunahadaiwa na vitu vyakipuuzi mno nawakati uhalisia tofauti!.
sasa nyie endeleeni kujifunika giza!
Mkuu sikupingi, ila hivi vitu vina process na procedure zake. Sio kienyeji hivo
 

Tundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo, Jumatano Septemba 25.2024 na kueleza kuhusu Tigo kuhusika na tukio lake la kushambuliwa

Simulizi ya Tukio la kushambuliwa kwake
"Ilichukua takribani wiki moja kama siku tisa (tangu Polisi wamuachilie huru Tundu Lissu bila masharti yoyote, ambapo alokamatwa baada ya kutoa taarifa ya kukamatwa kwa ndege ya Bombadier ya Tanzania nchini Canada), baadaye Septemba saba 2017 ndiyo nikashambuliwa kwa risasi, sasa baada ya kushamhuliwa kwa risasi haya ambayo nimeyasema (kuhusu kile kinachodaiwa kuwa kampuni ya tiGO ilitoa mawasiliano ya Siri kwa Tundu Lissu na kupeleka serikalini ambako anadai kuwa yalisaidia waliofanya jaribuo la kumuua kumfuatilia) tumeyafahamu jana (Jumanne ya Septemba 24.2024) na ushahidi uliotolewa Mahakamani huko nchini Uingereza" -Lissu

Namna TIGO walivyohusika
"Inaelekea tiGO walikuwa wameajiri mtu anayechunguza (yaani mchunguzi wa ndani), waliajiri askari Polisi wa kiingereza aliyekuwa anafanya kazi London Metropolitan Police, walikuwa wameajiri aliyekuwa mfanyakazi wa London Metropolitan Police, sasa siku chache baada ya kushambuliwa huyu Internal Investigater wa tiGO anaitwa MichaeL Clofford akasikia kwenye kikao cha siri kwamba yule jamaa aliyepigwa risasi sisi ndiyo tulitoa data zake, na kwamba sisi ndiyo tulipewa kazi ya kufuatilia" -Lissu"Sasa akaanzisha uchunguzi, kwamba inakuaje kampuni ambayo inapaswa kutunza siri za wateja inakuaje inashiriki kutoa siri za mteja ili auawe, sasa alianza kuchunguza, akachunguza akapeleka taarifa kwa mabosi wake, taarifa ya uchunguzi wake mabosi walipoona kwamba huyu jamaa amefanya uchunguzi sasa hii inaweza kutuharibia baadaye wakamuachisha kazi, sasa Michael Cliffod ameishtaki hiyo kampuni kwa kumuchisha kazi kwa sababu ya kufanya uchunguzi wa tiGO ya Tanzania na kumpa Magufuli (Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) taarifa zangu ili niuawe" -Lissu

"Sasa tangu 2019 walikuwa wanapambana Mahakamani hii kesi ifanyike hadharani au ifanyike faragha, Mahakama ya Uingereza ikasema hii kesi inahusisha viongozi wakubwa, na ina maslahi kwa umma kwa hiyo siyo siri, mimi nimefahamu siku marehemu Ali Kibao alipouawa" -Lissu

Mashtaka kwa Tigo
"Kwa kifupi Millicom (kampuni mama ya tiGO) hawajakanusha hiyo taarifa (taarifa ya kudai kuwa kampuni ya tiGO imetoa taarifa za siri za Tundu Lissu), kwa hiyo Milicom hawapingi (Mahakamani) kwamba walimsaidia Magufuli (Rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli) kunifanyi upelelezi ili nishambuliwe ili niuawe, Mawakili wamefuatilia na jana (Jumanne Septemba 24.2024 kwa mara ya kwanza 'The Guardiana' ya Uingereza imechapisha hii taarifa" -Lissu

"Sasa hii habari kubwa sana kwa kuwa tunapata mwanya wa kuwajua waliiohusika na waliowawezesha, kesi bado inaendelea na ndio kwanza imetolewa hadharani, huyu Clifford ameanza kutoa ushahidi na matumaini yetu ni mwamba ataeleza zaidi lakini amesema ameandaa ushahidi katika ripoti ya maandishi na amewapa mabosi tiGO anayo zao labda wachome moto na wakiichoma moto itabidi wachome mambo mengi sana na vilevile tutailazimisha tiGO ituambue ilikuwa inawasiliana na akina nani na nani wa serikali ya Tanzani, na nani aliyeomba mawasiliano yangu yafuatiliwe masaa 24" -Lissu

"Itabidi tupewe tuambiwe majina na itakayotuambia majina hayo ni tiGO, sasa kampuni mama si ipo Uingereza tunaanzanao tukiwapeleka kwenye Mahakama za Prof. Juma (Mahakama za Tanzania) hatutaenda kwenye Mahakama za Prof. Juma tunaenda Uingereza, tutakwenda huko walipo na majeshi ya kutosha ya wanasheria wa kimataifa, hii inahitaji watu wa kimataifa zaidi na tukienda huko tumewaambia walianzishe, leo nimezungumza na Bom Amsteederm nimemuambia una mamlaka kamili ya kulianzisha dhidi ya tiGO na serikali ya Tanzania,

Sasa hatujazungumza juu ya madai ya mapesa nafikiri yatakuwa mengi sana" -LissuTundu Lissu ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo, Jumatano Septemba 25.2024.

PIA SOMA
- Tundu Lissu: Aliyeongoza Kikosi cha wauaji walioagizwa kuniua ni Paul Makonda, ndio maana Marekani ilimzuia


Ndani ya Makampuni ya simu kuna Secret Agents wengi Sana wamepandikizwa huko, kazi yao ni kutoa Data za watu ambao ni walengwa wao. Hata baadhi ya Wafanyakazi waliopo kwenye Makampuni hayo ambao si 'mawakala wa kazi za siri' nao pia wanapaswa kuwa waangalifu Sana juu ya usalama wao binafsi kwa sababu kutokana na utendaji wao wa kazi unaozingatia weledi na uadilifu wanaweza wakajikuta wanakuwa kikwazo kwa 'watendaji mawakala wa shetani.'
Mfano hai kwenye suala hili ni tukio la mauaji dhidi ya aliyekuwa mfanyakazi mmojawapo wa mitandao ya simu iliyopo hapa nchini, tukio hilo lilitokea miaka kadhaa iliyopita katika eneo la Makutano ya Barabara kwenye Mataa ya Kuongozea Magari hapo Mwenge Jijini Dsm. Tukio hilo lilifanyika wakati wa muda wa mchana kweupe jua linawaka, na Askari wa Usalama wa Barabarani walikuwepo hapo Mwenge kwenye traffic lights wakiendelea na kazi yao ya kuongoza magari. Wauaji hao baada ya kutekeleza tukio hilo walichukua bahasha tu iliyokuwa na documents kutoka kwenye gari ya huyo mtu aliyeuawa, huku wakiziacha pesa zilizokuwemo kwenye hiyo gari, Huyo Mfanyakazi aliyeuawa inasemekana alikuwa akitokea eneo la Mlimani City kwenye moja ya Ofisi za kampuni yake. Nafikiri wapo baadhi ya members humu mtandaoni watakuwa wanalikumbuka vizuri Sana tukio hilo.
 
Hela ya bure hii hapa.. Lisu anaenda kuwa billine nyuma ya Mo
Huyu Mungu acha aitwe Mungu
Damu ya mtu haimwagiki bure.
Haijalishi imechukua mida hani lakini mwanga ume anza kuonekana.
Wale walio zuia kwenda kutoa sadska wakati Lissu akiwa hospitali wakasahau kumzuia yeye alivyo kwenda kutoa sadaka Singida sasaimekua aibu kwao. Sadaka ya Lissu ime pokelewa. Sasa tuna suburi wazee wa Tanga wapige dua watu waanguke. Dadadadek. Asante Mungu kwa kuiweka serikali ya Ccm uchi.
 
Tusimuhukumu, JPM, tusubili kwanza. Kwani haya yanoyoendelea si huenda kuna watendaji waliopewa dhamana ya kulinda raia na mali zao nao wanaweza pia kuwa wanajichukulia sheria mikononi bila ya kupew maagizo from the Top? Tusubilie undani utapatikana, at least TL amepata pa kuaniza, yote yataanikwa hadharani.
 
Hii kesi Nape na makamba wanaipenda sana kwasababu wabaya wao wakina Makonda hawana pa kukimbilia tena na kibaya zaidi inaelekea wale vijana wapigaji risasi wanajulikana sasa na team ya Lissu imeshapewa majina. Tukumbuke hii wizara ya mawasiliano ilikuwa chini ya Nape na yuko tayari kumsaidia Lissu inasemekana
 
Mkuu sikupingi, ila hivi vitu vina process na procedure zake. Sio kienyeji hivo
babu hapo hakuna cha kienyeji nimeelezea vyema tu isipokuwa baadhi ya watu wao kila kitu ni pingapinga haswa kikiwa ni kitu ambacho hakipo ktk mlengo wao!,msijifunike sana mtashindwa kuona shauli yenu...😂
 
au sio! hapo wanajisumbua tu hao wazungu wanawahadaa watu wasio na akili ipo hivi...

Hakuna serikali iwe inamamlaka za ulinzi(intelijensia),halafu isifatilie taarifa, taarifa ni muhimu ktk namna yoyote ile na moja kati ya vyanzo vya taarifa ni mitandao ya mawasiliano na mitandao yakijamii.
huku sisi wanatupigia kelele angalia huko mmiliki wa telegram wamemfanya nini na mpk amekubali kutoa ushirikiano na serikali yoyote endapo watahitaji taarifa za mtu yoyote telegram!.

kuhusu swala la serikali kutafuta taarifa za mtu fulani sio shida,shida ni kwamba hizo taarifa walizifanyia nini sasa wengi naona wanahangaika kulaumu serikali na tigo kwa kuchukua taarifa za lissu,pasipokujua walizifanyia nini maana hicho ndio kitu kinachoweza kuleta hatia!.

msidanganyike faragha ikizidi hata nchi inakuwa si salama so kufatiliwa lazima wakufatilie tu wakihitaji.
Watz wengi ni wafuata upepo tu wangejiuliza tu kwanini Snowden alikimbia baada ya kutoa siri za Marekani kuwafuatilia viongozi wa EU kupitia mitandao ya mawasiliano!!?
 
Back
Top Bottom