Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nimekutana na post inasambaa mtandaoni Tundu Lissu akisema anaunga mkono ushoga na video ina maneno yanayosema "Lissu akiri kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja" je post hii ina ukweli wowote?


 
Tunachokijua
Tundu Lissu ni makamu mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia kitaaluma ni mwanasheria ambapo mwaka 2017 Alikuwa ni Rais wa chama cha wanasheria Tanzania (TLS) kwa miezi mitano kabla ya kushambuliwa kwa risasi. Mwaka 2010 mpaka 2020 alikuwa ni mwakilishi wa wananchi Bungeni wa jimbo la Singida Mashariki. Tundu Lissu amekuwa ni miongoni mwa wanasiasa walio mstari wa mbele katika kukosoa serikali. Moja ya tukio lisilosahaulika alilowahi kukumbana nalo ni kupigwa risasi mnamo septemba 7 2017 ambapo watu waliotekeleza tukio hilo bado hawajajulikana mpaka hii leo

Januari 21 2019 Tundu Lissu alifanya mahojiano na mwandishi Stephen Sackur katika kipindi kijulikanacho kama Hard talk cha Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC alipotakiwa kusema juu ya sheria inayotoa adhabu ya miaka 30 jela dhidi ya wanaojihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ambapo Lissu alijibu kwa kusema kila mmoja ana haki ya kuwa na faragha, na haitakiwi kuiruhusu serikali kuingia mpaka ndani ya vyumba vya watu, na kwamba kama sheria zinaingilia faragha za watu, basi sheria hizo hazifuati misingi ya kikatiba.

Kumekuwepo na Video inayosambaa mtandaoni ikiwa na maneno yanayoonesha Tundu Lissu kukiri juu ya kuunga mkono mapenzi ya jinsia moja huku Video hiyo ikianza kwa Kumuonesha Lissu akisema naunga mkono mapenzi ya jinsia moja.

Uhalisia wa Video hiyo inayosambaa mtandaoni upoje?

Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia Google reverse image search ulibaini kuwa video hiyo imepotoshwa kutoka kwenye video halisi ambayo ilihusisha mahojiano ya Tundu Lissu na kituo cha Televisheni cha Clouds TV, ambapo katika mahojiano hayo Lissu alisema hajawahi kusema mahali popote kwamba anaunga mkono mapenzi ya jinsia moja, Video hiyo iliyopotoshwa iliondoa “maneno sijawahi kusema popote” badala yake ikaanzia “naunga mkono mapenzi ya jinsia moja” maneno ambayo aliyasema kwa pamoja ili kukanusha.

Video halisi ilichapishwa katika mtandao wa youtube na Clouds media mnamo februari 04 2023 ambapo Tundu Lissu pamoja na kukanusha kuhusu kuhusishwa kwake na kuunga mkono dhidi ya mapenzi ya jinsia moja Lissu aliongeza kuwa watu wenye utamaduni wa ushoga waendelee lakini tamaduni na sheria zetu haziruhusu ushoga na yeye haungi mkono ushoga.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…