BongoLocate
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 487
- 677
- Thread starter
- #21
Siwezi kuongopa ili kutengeneza ushawishi kwa kusema mita 200 wakati ni mita 700. Lakini walio wengi, ukweli kwao ni chungu na uongo ni tamu.Mbona mita 700 ni mbali Sana na ufukwe wa bahari? Lakini unavyoiekezea kana kwamba viko karibu na bahari?! Mita 700 ni zaidi ya nusu kilometa mjomba! Au Siyo! Fafanua vizuri ndugu. Biashara yako nzuri lakini toa maelezo sahiii..
Pia sikusema viwanja hivi ni vya ufukweni bali viko pwani ya bahari.
Ufukweni inaweza kuwa mita 0 - 200 lakini pwani ya bahari inaweza kuwa hata mpaka kilomita 1 kutegemeana na sifa za mazingira ya eneo husika.
Mfano, ukiwa Dar es Salaam, barabara ya Bagamoyo, kuna maeneo ya Mbezi beach ambayo yako karibu na barabara na mbali na bahari lakini kwa kuwa yana sifa moja kama mwinuko kutoka usawa wa bahari, uoto wa asili n.k, yanatambulika kuwa ni maeneo ya beach.
Labda na mimi ningetumia neno beach badala ya pwani ya bahari ndo ningeeleweka.