Tunarudi kwenye enzi za mabosi wa Mashirika ya Umma kujaza watu wa makabila yao. Tiketi aliyotoa Rais inaenda kupiga mchujo wa kikabila kwenye ajira

G Tank

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
2,067
7,926
Niseme tu Mama ameshauriwa vibaya katika hili la leo kuruhusu mabosi wa kila shirika kuajiri badala ya kuwa na utaratibu uliopo wa chombo kimoja kusimamia ajira za mashirika yote.

Ikumbukwe wazo la chombo kimoja kusimamia ajira lilikuja baada ya upendeleo uliokuwepo wa wazi wazi katika ajira hapa nyuma, mtoto wa bosi akimaliza chuo anaambiwa kesho aanze kwenda kazini, ndugu wa bosi akiomba kazi ni chap chap, mabosi kuchuja watu wa makabila yao ndio ilikuwa pigo zito sana.

Kifuatacho kwa sasa, Mkuu wa shirika lolote atakaphiyaji kuajiri anaweza kupitisha majina ya watu wa kabila lake kwanza alafu ndio mambo ya vyeti yanafatatia, tena hata hivyo vyeti bosi anaweza kujua ni feki ila akampitisha.

CONCLUSION

Kimsingi tunahitaji reform ya chombo cha utumishi kifumuliwe upya, ni chombo ambacho kwa sasa kimeshuka kiutendaji hasa kwa kuchelewa kuita watu makazni, bado tunahitaji kuwa na chombo kimoja central cha kusimamia ajira.

Huu uamuzi uliofanywa leo unatupeleka nyuma kule ambako tulitoka.

Pia soma >

 
Hoja yako ni nzuri sana na niseme tu Mama anashauriwa vibaya hawa wajanja waliokuwepo nae wameshindwa kupitisha vi memo ,wamemuingiza King akakubali.

Kifuatacho Mkuu wa shirika lolote atakapohitaji kuajiri watu ambao anaowataka atapitia njia za mkato,kwa maana anaweza akatumia kigezo wanahitajika haraka.

Lakini pia Utumishi wajitathimini kwa sasa wanachelewa kutoa sana majibu,kuna harufu ya rushwa na maelekezo ndani yake .

Kimsingi tunahitaji reform,lakini mama anapotupeleka ni kuturudisha nyuma kule ambako tumetoka.
 
Mnamsingizia kuwa anashauriwa vibaya.

Fuatilia kwa kina yanayojjri nchini kwenye ajira na maeneo nyeti, kinachoendelea ndo picha halisi
 
Unapoteza muda wako kushauri watu wapumbavu ...tz tunatakiwa kutafuta dictator mzalendo kama jpm ila awe mkatiri zaidi siyo kama jpm alikuwa anacheza na kima ...mimi nili mdharau jpm kumwacha singasinga kuendelea kuishi hata week moja
 
Huyu naye huwa saa zingine anaropoka

Mfano kasema kuwa kampuni ikishachaguliwa, zilizoachwa zisiende pccb na ppra
 
Wabongo sijui nini mnataka yaani. Wakati ajira zinatoka utumishi malalamiko kila siku jinsi kulivyo na urasimu na kupotezeana muda/nauli sasa mchakato umeeahisishwa malalamiko tena!

Hivi nini mfanyiwe muwe na shukurani wazee?

Hivi unadhani utumishi ndio hakukuwa na ndugunaizesheni? Pole Sana
 
Unapoteza muda wako kushauri watu wapumbavu ...tz tunatakiwa kutafuta dictator mzalendo kama jpm ila awe mkatiri zaidi siyo kama jpm alikuwa anacheza na kima ...mimi nili mdharau jpm kumwacha singasinga kuendelea kuishi hata week moja
Na ukatiri wake ni kitu gani hasa cha maana alichokifanya?zaidi ya kuleta maafa tu kwa wananchi!!Eti mwananchi kulalamika maisha magumu nalo ni kosa akamatwe!!!ndugu akipotea eti ukitoa taarifa polisi na wewe ukamatwe!!tunachoweza kusema MUNGU FUNDI
 
Kivyovyote vile kama ipo ipo tu ,kutusua kupo pale pale. Hayo mambo sijui ya ukabila hata kujuana wengine hatuna time wao wanatujua ila sisi hatuwajui.

Kila mtu ashinde mechi zake kama wataajiri watu wa nyumbani kwao basi ni kheri pia kwao..Tatizo lipo wapi?

Yule marehemu mlikuwa mnamuona kichaa sasa hayupo pambaneni. Watu wanataja makabila kadhaa ila almost yote ya Tz Yana ule fovouritism
 
Wabongo sijui nini mnataka yaani. Wakati ajira zinatoka utumishi malalamiko kila siku jinsi kulivyo na urasimu na kupotezeana muda/nauli sasa mchakato umeeahisishwa malalamiko tena!

Hivi nini mfanyiwe muwe na shukurani wazee?

Hivi unadhani utumishi ndio hakukuwa na ndugunaizesheni? Pole Sana
Utumishi ndio walikuwa wa hovyo. Awamu ya tano walifanya vile kupunguza vibali vya ajira. Na kulikuwa na uhaba mkubwa sana wa ajira.

Walivyo na kiburi sasa eti nafasi 5 wanaita watu interview 1000. Huu ulikuwa ni unyanyasaji mkubwa wa kisaikolojia kwa watafuta ajira.
 
Back
Top Bottom