Tume ya Uchaguzi Uganda yamtangaza Museveni mshindi, Besigye apinga matokeo

5fc9ebefa3792d6397355f2b21bb60c4.jpg

Mambo yamewiva......
 
Ile ni Nchi ya kimapinduz lazima mapinduzi yafanyike kama Zanzimbar ni Nchi ya kimapinduz lazima yafanyike kwenye box tutachelewa
 
Hii mirais ya Africa bana......
Preta afadhali umeliona hili. Mirais! Ndio maana mimi sishabikii anayoyafanya wa hapa maana yanaendana na kukuika to some extent haki za binadamu. Mfano kufungia gazeti kwa vile mmepishana msimamo ni hatari sana
 
Tunaomba mmarekani aje atutawale
Subirini "raisi"..wenu Triump..Chadema kabla ya uvamizi kilikuwa ni chama cha hoja chenye kushtaki serikali kwa wananchi kwa nguvu ya hoja...kwa sasa mnaishitaki serikali kwa wamarekani na magenge yake!...
 
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.
Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Museveni ametangazwa mshindi licha ya kwamba kuna vituo ambavyo bado matokeo hayajatangazwa. Dkt Kiggundu amesema matokeo ya vituo hivyo hayawezi kubadilisha mambo. Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.
Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.
chanzo : BBC
 
Hakuna haja ya kufanya Uchaguzi kwa nchi za Kiafrica kama Demokrasia yenyewe ndio hii. Ni vema tu tuwe na mfumo kama wa China watu wachache wanakaa wanateua Rais au Unajitangaza tu moja kwa moja kuwa ni Rais wa Maisha kuliko kupoteza Watu na pesa kwa kisingizio cha Demokrasia.
Ifike sasa Hii Demokrasia tuachane nayo tu maana imetushinda.
Shame on Museveni
 
Ujinga ujinga tu unawasumbua Waafrika, ipo siku tutaamka na kukataa uzandiki na hapo ndo tutachafukwa bara zima kudai haki zetu na kukataa upuuzi.
 
Back
Top Bottom