Tume ya Uchaguzi Uganda yamtangaza Museveni mshindi, Besigye apinga matokeo

Pole xana kamanda dr.Kizza,ardhi inaandika historia ya mchango wako kwa jasho na damu na sauti yako imepenya kwenye maskio ya anga..africa hakuna demokrasi ila kuna democrasi ya matumbo..next time wanamageuzi wa africa wasishiriki uchaguzi usio uwanja sawa kuokoa mda,rasilimali na kuepusha sufferings badala yake uanaharakati wa demokrasia na haki za binadamu kama Martin Luther Jr,ikifeli na hiyo basi tutalazimika kunyonya upanga kuweka rehani uhai..we sympathise with you and our fellow ugandans,sie pia tunaganga upuuzi kama huo uliofanywa na Mafisiem tofauti na huko huku yanabadilishana yenyewe kwenye lichama lao..the struggle is long and hard,aluta continua
 
huyu kizza besigye naye hana tofauti na maalim seif wa uganda, yaan kila uchaguzi mkuu, anagombea yy tu, hv kwenye vyama vyao kuna demokrasia kwl? kwann asiachie na wengine wagombee, KAMA UNAGUNDU KWANN USIACHIE NA WENGINE WAJARIBU BAHATI ZAO?
 
Hakuna sababu ya kuwepo kwa uchaguzi kwa baadhi ya nchi za africa....huku ni kuhadaa watu na kupoteza pesa.....
 
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Alhamisi.
Rais Museveni alipata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume hiyo Dkt Badru Kiggundu.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye alipata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na asilimia 35.37%.
Museveni ametangazwa mshindi licha ya kwamba kuna vituo ambavyo bado matokeo hayajatangazwa. Dkt Kiggundu amesema matokeo ya vituo hivyo hayawezi kubadilisha mambo. Awali, waangilizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikuwa wamekosoa uchaguzi huo wakisema kulikuwa na kasoro nyingi.
Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.
chanzo : BBC
M7 hadi hapo atakapo kufa ndipo Kiza ataingia madarakani.
 
Ataondolewa kwa NGUVU ya UMMA, mpumbavu sana huyu!

Viongozi wa Afrika wamesahau kuwa kuna kifo, hivyo wanadhani watatawala milele.
 
Na the same itaenda kutokea Zanzibar....Nchi zenye viongozi wapenda uchu wa madara na wananchi waoga.
 
Afrika hakuna demokrasia ni uhuni mtupu, tunaiga vya kuiga hovyo kweli,binafsi namuunga mkono Prof Kitila Mkumbo,aliandika haya=>ilikuwa February 19 kabla ya uchaguzi Uganda.
Yanayoendelea Uganda na sehemu zingine katika bara letu, ikiwemo Zanzibar, itukumbushe tena kwamba Waafrika tuliupokea utamaduni wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kwa shinngo upande. Kuanzia tunavyoendesha mambo ndani ya vyama vyetu hadi katika ngazi ya taifa ni utani unaogeuka kuwa mateso kwa wanachama na wananchi. Bahati mbaya ni kwamba tumeiga mambo yetu karibu yote kutoka hukohuko tulikoiga demokrasia, ikiwemo maana ya maendeleo!! Sasa yatupasa tutambue kwamba hayo maendeleo ya kizungu tunayopigana kuyapata, ikiwemo dhana mpya ya uchumi wa kati, msingi wake ni demokrasia. Madamu tumeamua kuchezea demokrasia ya kimagharibi tusahau kabisa maendeleo ya kimagharibi. Hii ni Kwa sababu pasipo demokrasia ya magharibi haiwezekani kupata maendeleo ya kimagharibi. Kama hatutaki hii demokrasia tuachane kabisa na dhana yao ya maendeleo ya kimagharibi na tuanze kujenga dhana ya kiafrika isiyotegemea demokrasia hii tuliyoiga kishingo upande ili tuendelee kupata nidsaada yao.

Lakini nawaona vijana wetu walivyojipanga kupata maendeleo ya kimagharibi na siamini kwamba inawezekana kuwashawishi waachana na hii dhana ya maendeleo. Basi Nawakumbusha hawa vijana kwamba hawatafanikiwa sana kupata maendeleo ya kimagharibi kama hawatapigania demokrasia ya kweli ya kimagharibi. Hivyo basi nawasihi vijana popote mlipo, wakati mkiendelea kupigania maendeleo ya kimagharibi msiache kamwe kupigania demokrasia yake Kwa sababu ndiyo msingi wa hayo maendeleo myatakayo. Na tena muanze kupigania demokrasia kuanzia katika vyama vyenu. Amini nawaambieni hatuwezi kamwe kujenga demokrasia ya kimagharibi katika nchi bila kwanza kueneza utamaduni wa kidemokrasia ndani ya vyama vyetu. Msingi wa demokrasia katika taifa ni demokrasia katika vyama vya siasa. wanachama wanaokumbatia vyama visivyo vya kidemokrasia hawana uhalali wa kiroho wa kudai demokrasia katika nchi. Huu ndiyo ujumbe wangu wa leo.
 
Trump tunakusubiria kwa hamu kubwa, hawa Marais madikteta wengi wa Africa lazima UWASHIKISHE ADABU... damn
 
Back
Top Bottom