SoC03 Tulipokuwa tukiwacheka watoto wa mitaani, hatukujua kuwa tutakuja kuwa wasomi wa mitaani

Stories of Change - 2023 Competition

Sweya Makungu

JF-Expert Member
Jun 11, 2023
481
560
Tulipokuwa Tukiwacheka Watoto wa Mitaani, Hatukujua Kuwa Tutakuja Kuwa Wasomi wa Mitaani..
💫💫💫💫💫

©️Mwl. Makungu m.s
0743781910

Unaikumbuka ile miaka ya 90 kuja juu kidogo wakati miji mikubwa ilipoanza kupata tatizo la kuongezeka kwa watoto wa Mitaani?

Unayakumbuka majina mabaya tuliyokuwa tukiwapa watoto wa Mitaani na kuwahukumu bila kujua historia zao na tabia zao ?

Lilikuwa ni Jambo geni miongoni mwa jamii zetu wakati huo . Kuwa mtoto wa Mitaani ilikuwa ni Kama laana aliyojitakia mtoto mwenyewe.

Hatukujiuliza juu ya changamoto za wazazi wao Wala sababu zao za kuwa Mitaani. Tulichojua ni kuwa wale ni waasi waliotoroka kwny familia zao kuja kuwa vibaka.

HATUKUJUA:

Wakati shule na wazazi wakitulea kwa huruma na upendo , Mitaa iliwalea kwa chuki bila huruma.

Wakati shule zikitupa maadili maarifa na ujuzi wa kinadharia , Mitaa iliwafunza uharamia , maarifa ya kujiokoa na kifo na ujuzi wa vitendo.

Wakati shule zilipotupa uhuru na ujasiri wa kuhoji maarifa na kuheshimu mfumo , Mitaa iliwapa ujasiri wa kuheshimu na kutumia maarifa na kuupinga mfumo.

Wakati shule zilipotupa heshima ya vyeti na kutunyima uthubutu wa kujaribu kusimama wenyewe bila kufikiria ajira , Mitaa iliwanyima heshima na kuwapa ujasiri wa kuthubutu kusimama wenyewe kujiajiri kiubunifu.

Wakati shule zikitugawa kimatabaka ya kiuchumi na kutufanya tuwe na roho ya ubinafsi , Mitaa iliwaweka pamoja na kuwajaza upendo wa kusaidiana wao kwa wao vichochoroni, vibarazani na madarajani.

Wakati shule zikitufundisha historia yetu , uzalendo na amani, Mitaa iliwafunza historia ya maumivu yao ya kutengwa, chuki kwa waliofanikiwa na unyama kwa yyt atakayeingia anga zao.

Tulipowaepuka na kuwaogopa km vibaka , walijivika roho mbaya na kutusumbua km mateka.

Tulipowachukia na kuwasaka kuwatokomeza , walijigeuza wakapotea ktk sura za kuigiza .

Wachache wao walipopata bahati ya kurudi shule tuliwatenga tuliwasema na kuwasengenya kimya kimya huku tukiwaogopa km vibaka..

Serikali ilitupenda na kutulea km mayai , wakati ikiwasaka na kuwakamata km wazururaji na waharifu Mitaani.

HATUKUTEGEMEA
Kuwachukia kwetu kuliwakomaza na kuwatengenezea dunia ya peke yao .

Mitaa ilikuwa ni shule kwao . Na Kama vile sisi tulivyo hitimu vyuoni na wao pia walihitimu chuo kikuu cha mtaani.

Kama vile sisi tulivyofeli ktk hatua mbalimbali za elimu na kuishia njiani na wao pia wapo waliofeli wakauwawa km vibaka ,wakafungwa gerezani ,wakawa panya road na majambazi sugu.

Kwa wale tuliofaulu na kuhitimu vyuo vikuu
Wachache wenzetu wamebahatika kupata ajira . Lakini kundi la wengi lipo linazunguka Mitaani na bahasha za kaki likisaka ajira bila mafanikio. Na yale mahusiano yao ya chuoni yamevunjikia njiani kwa sbb ya Hali ngumu na ulevi . Siyo kosa lao . Ni kosa la ile elimu ya nadharia iliyowafundisha kuhoji maarifa na kuheshimu mfumo .

Wamegeuka kuwa Wasomi wa mitaani

Kwa wale waliofaulu na kuhitimu elimu ya mitaani

Wamegeuka kuwa wajasiriamali ,wafanyabiashara, wasanii, wanamichezo,manabii, motivational speakers, n.k wenye mafanikio na wanaishi kwa maadili na nidhamu.

Wamegeuka kuwa wahamasishaji wa mfano wa Mitaani.

Tuache kudharau watu na kuwahukumu bila kujua historia zao na changamoto za familia zao .

Tuchukue hatua mapema juu ya
bomu la watoto wa Mitaani na Wasomi wa Mitaani.

Ili ujiondoe mwenyewe kwenye kundi la wasomi wa Mitaani kabla serikali haijategua Hilo bomu jiongeze ndugu yangu . Tumia elimu uliyoipata kufanya ubunifu wa kuigeuza ikuletee pesa. Ikibidi Jivue usomi jivike umtaa. Tumia vipaji ulivyopewa na Mungu ambavyo havitolewi shuleni . Vipaji vinanolewa shuleni lakini vinatolewa na Mungu .

Ukipata bahati ya kufika kuzimu ukiwa ndotoni kawaulize mainjinia waliojenga mapiramidi ya Misri walisomea wapi uinjinia na waliwezaje kunyanyua mawe makubwa km yale mpk juu angani nyakati ambazo hakukuwa na mashine duniani!!!
Hapo ndipo utakikumbuka kipaji chako alichokupa Mungu..
Kama ambavyo mm natumia kipaji changu cha uandishi...

Jamii inapaswa kutambua kuwa, watoto wa mitaani hawakuzaliwa na mitaa . Wana wazazi wao ndugu na jamaa zao. Isipokuwa ni changamoto nyingi na ngumu za migogoro ya kifamilia ndizo huwafanya watoto wakimbilie mitaani na kuwageuza kuwa watoto wa mitaani..
Watoto Hawa huwa na ndoto zao na matamanio yao katika maisha lkn hujikuta wakibadili mitazamo yao juu ya maisha na kuingia katika mfumo mwingine wa kupambana na maisha baada ya Kupoteza njia za kufikia malengo ya ndoto zao.

Watoto wa mitaani wanahitaji faraja na tiba ya kisaikolojia ili kuwarejesha katika afya nzuri ya akili baada ya athari za manyanyaso katika familia na kutengwa na jamii husika.
Hatupaswi kuwatenga kuwadharau , kuwacheka wala kuwakejeli watoto wa mitaani kwa hali yao ya kuishi mitaani. Maana maisha yamebeba siri nzito ya mafanikio ya mwanadamu.
Unayemtegemea ndiye, siye . Lolote linaweza kubadilika muda wowote katika maisha ya mwanadamu.

Lakini pia ili kuepuka ongezeko la wasomi wa mitaani , serikali inapaswa kuweka mifumo mizuri ya elimu itakayoweza kuwafanya wahitimu wa elimu za darasani kuweza kujiajiri baada ya kuhitimu ngazi fulani ya elimu.
Mitaala ya elimu ijumuishe elimu za ujuzi mbalimbali mathalani ufundi wa aina tofauti tofauti , michezo , sanaa na muziki ili kuwafanya wahitimu wakitoka mashuleni na vyuoni kuanza kuvitumia vipaji vyao na ujuzi wao waliounoa au kuupata shuleni kujiingizia kipato na kuyaendesha maisha.

Makungu m.s
0743781910
 
Tulipokuwa Tukiwacheka Watoto wa Mitaani, Hatukujua Kuwa Tutakuja Kuwa Wasomi wa Mitaani..
💫💫💫💫💫

©️Mwl. Makungu m.s
0743781910

Unaikumbuka ile miaka ya 90 kuja juu kidogo wakati miji mikubwa ilipoanza kupata tatizo la kuongezeka kwa watoto wa Mitaani?

Unayakumbuka majina mabaya tuliyokuwa tukiwapa watoto wa Mitaani na kuwahukumu bila kujua historia zao na tabia zao ?

Lilikuwa ni Jambo geni miongoni mwa jamii zetu wakati huo . Kuwa mtoto wa Mitaani ilikuwa ni Kama laana aliyojitakia mtoto mwenyewe.

Hatukujiuliza juu ya changamoto za wazazi wao Wala sababu zao za kuwa Mitaani. Tulichojua ni kuwa wale ni waasi waliotoroka kwny familia zao kuja kuwa vibaka.

HATUKUJUA:

Wakati shule na wazazi wakitulea kwa huruma na upendo , Mitaa iliwalea kwa chuki bila huruma.

Wakati shule zikitupa maadili maarifa na ujuzi wa kinadharia , Mitaa iliwafunza uharamia , maarifa ya kujiokoa na kifo na ujuzi wa vitendo.

Wakati shule zilipotupa uhuru na ujasiri wa kuhoji maarifa na kuheshimu mfumo , Mitaa iliwapa ujasiri wa kuheshimu na kutumia maarifa na kuupinga mfumo.

Wakati shule zilipotupa heshima ya vyeti na kutunyima uthubutu wa kujaribu kusimama wenyewe bila kufikiria ajira , Mitaa iliwanyima heshima na kuwapa ujasiri wa kuthubutu kusimama wenyewe kujiajiri kiubunifu.

Wakati shule zikitugawa kimatabaka ya kiuchumi na kutufanya tuwe na roho ya ubinafsi , Mitaa iliwaweka pamoja na kuwajaza upendo wa kusaidiana wao kwa wao vichochoroni, vibarazani na madarajani.

Wakati shule zikitufundisha historia yetu , uzalendo na amani, Mitaa iliwafunza historia ya maumivu yao ya kutengwa, chuki kwa waliofanikiwa na unyama kwa yyt atakayeingia anga zao.

Tulipowaepuka na kuwaogopa km vibaka , walijivika roho mbaya na kutusumbua km mateka.

Tulipowachukia na kuwasaka kuwatokomeza , walijigeuza wakapotea ktk sura za kuigiza .

Wachache wao walipopata bahati ya kurudi shule tuliwatenga tuliwasema na kuwasengenya kimya kimya huku tukiwaogopa km vibaka..

Serikali ilitupenda na kutulea km mayai , wakati ikiwasaka na kuwakamata km wazururaji na waharifu Mitaani.

HATUKUTEGEMEA
Kuwachukia kwetu kuliwakomaza na kuwatengenezea dunia ya peke yao .

Mitaa ilikuwa ni shule kwao . Na Kama vile sisi tulivyo hitimu vyuoni na wao pia walihitimu chuo kikuu cha mtaani.

Kama vile sisi tulivyofeli ktk hatua mbalimbali za elimu na kuishia njiani na wao pia wapo waliofeli wakauwawa km vibaka ,wakafungwa gerezani ,wakawa panya road na majambazi sugu.

Kwa wale tuliofaulu na kuhitimu vyuo vikuu
Wachache wenzetu wamebahatika kupata ajira . Lakini kundi la wengi lipo linazunguka Mitaani na bahasha za kaki likisaka ajira bila mafanikio. Na yale mahusiano yao ya chuoni yamevunjikia njiani kwa sbb ya Hali ngumu na ulevi . Siyo kosa lao . Ni kosa la ile elimu ya nadharia iliyowafundisha kuhoji maarifa na kuheshimu mfumo .

Wamegeuka kuwa Wasomi wa mitaani

Kwa wale waliofaulu na kuhitimu elimu ya mitaani

Wamegeuka kuwa wajasiriamali ,wafanyabiashara, wasanii, wanamichezo,manabii, motivational speakers, n.k wenye mafanikio na wanaishi kwa maadili na nidhamu.

Wamegeuka kuwa wahamasishaji wa mfano wa Mitaani.

Tuache kudharau watu na kuwahukumu bila kujua historia zao na changamoto za familia zao .

Tuchukue hatua mapema juu ya
bomu la watoto wa Mitaani na Wasomi wa Mitaani.

Ili ujiondoe mwenyewe kwenye kundi la wasomi wa Mitaani kabla serikali haijategua Hilo bomu jiongeze ndugu yangu . Tumia elimu uliyoipata kufanya ubunifu wa kuigeuza ikuletee pesa. Ikibidi Jivue usomi jivike umtaa. Tumia vipaji ulivyopewa na Mungu ambavyo havitolewi shuleni . Vipaji vinanolewa shuleni lakini vinatolewa na Mungu .

Ukipata bahati ya kufika kuzimu ukiwa ndotoni kawaulize mainjinia waliojenga mapiramidi ya Misri walisomea wapi uinjinia na waliwezaje kunyanyua mawe makubwa km yale mpk juu angani nyakati ambazo hakukuwa na mashine duniani!!!
Hapo ndipo utakikumbuka kipaji chako alichokupa Mungu..
Kama ambavyo mm natumia kipaji changu cha uandishi...

Makungu m.s
0743781910
Mtaa ni mama wa Kila kizazi, kipindi ndiyo mwamzi! Asante sana mwl. Makungu
 
Nice andiko
 
Back
Top Bottom