Tukutane hapa watumishi ambao hawategemei mishahara, tuelezane changamoto na mbinu

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,776
5,912
Nimefungua huu uzi kwa ajili ya kuwakutanisha watumishi wote wenye idea ya ujasiriamali, wanaofanya biashara,kilimo,ufugaji na wanaotarajia kufanya biashara, kilimo na ufugaji n.k

Kwa ugumu wa maisha jinsi ulivyo mfumuko wa bei ni ndoto kwa sisi watumishi wa halmashauri kutoboa, Kuna clip moja wasira alisema "mshahara unakupa pesa ya kula tu na kuvaa" na huo ndio ukweli. Bei ya mchele inapepea, sukari juu mafuta juu, Mwisho wa mwezi unabaki na madeni na kuishi kwa kuomba omba na kubangaiza kwanini tusidharaulike na waendesha bodaboda?

Nimetembea mazingira mengi kabla ya kuajiriwa kama Mwalimu na baada ya kuajiriwa, nimeona watumishi wengi waliofanikiwa humu humu kwenye ajira ya serikali, Nawasifu walimu na watumishi wengine waliopo mijini, Kuna Shule moja nilienda nikakuta magari yamepaki japo ni IST Lakini ni sign mojawapo ya kuanza kujikwamua kiuchumi, at the same time wewe unaenda kwenye kituo chako Cha kazi na baiskeli na sio kwamba umeamua kununua baiskeli kwa sababu ya mazoezi hapana ni kwa sababu ya ugumu wa maisha, kwanini bodaboda asitudharau?

Kwenye Maofisi huko unaona kabisa nyuso za watu zikiwa zimekata tamaa kabisa, furaha hakuna maisha Magumu, je ni kweli duniani tumekuja kuteseka? Je wenye biashara mijini/ vijijini ni smart sana kuliko sisi? Tunakwama wapi?

Unakuta mtumishi Kadi ameiacha kwenye hizi ofisi ndogo za kukopesha ambao hawajali 1/3 ya mashahara. Yoote ni ugumu wa maisha na pesa amechukua alichofanyia hakionekani, tunavaa na tunakaa kwenye nyumba kama vile hatulipwi mishahara.

Nafahamu humu Kuna watumishi ambao walijiongeza/ wanajiongeza je waliwezaje? Kipi kifanyike kwa mtumishi kujikwamua kiuchumi?. Wanawezaje kusimamia? Vipi kwa walioko halmashauri ya Kijijini wafanye nini!

Idea yangu ni hii kwa watumishi, Naanza na estimation ya mtaji wa million 5 ambayo Kila mtumishi anaweza kuimudu.

1. Kufungua duka la nafaka mbalimbali (5million unaweza Anza)
2. Duka la simu na vifaa vyake
3. MPESA, TIGOPESA, WAKALA WA BANK ZOTE (wengi wanafanya)
4. Duka la viatu vya kike aina zote za viatu
5. Duka la vinywaji baridi (it depend na location na mkoa ulipo)
6.kilimo (Kuna mabonde ambayo yana maji na hawategemei mvua ekari 300,000)....

Ongeza na za kwako na changamoto yako, action na implementation ni muhimu tuache ngojera, na tukimbie dharau ndogo ndogo.
 
Sikuhizi kilimo kinafanywa na kila mtu awe mwajiriwa au mjasilia mali...tusiache kulima wakuu..

Binafsi kilimo cha mpunga kimefanya nisahau lini nilimaliza chuo na ikitokea nimekosa ajira kwa miaka 3 ijayo,sitakubali kuajiriwa tena..
Sitaki kuhamishwa idea kiboya
 
Hongera sana
 
Safi sana, na ndugu yangu Yuko huko ubaruku anapiga pesa za kutisha
 
Duka la vifaa vya pikipiki hasa huko mikoani
Nunua canter uzoe watu kwenye magulio inalipa Sana unajioangia nauli ( ila uwe na elf kumi ya trafik)
Asikutishe mtu bodaboda hashindani na mtumishi!!achana na watoto
 
Naunga mkono hoja....sito changia Kwa Sasa 🚫 ntajikita kwenye kujifunza zaidi....

Nina mengi ya ku share hapa naomba Kwa Sasa niwe msoma comment...

Asante sana Kwa huu Uzi wa ki ujasiliamali..
 
Duka la vifaa vya pikipiki hasa huko mikoani
Nunua canter uzoe watu kwenye magulio inalipa Sana unajioangia nauli ( ila uwe na elf kumi ya trafik)
Asikutishe mtu bodaboda hashindani na mtumishi!!achana na watoto
Nzuri hii nimeziona sana minada ya manyara, kigoma huku hakuna minada, it depend na location pia
 
Issue ni management
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…