Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,904
- 31,974
Tarehe 17 April 1953 ulifanyika mkutano wa mwaka wa TAA Ukumbi wa Arnautoglo, Dar es Salaam.
Mkutano wa mwisho wa TAA ulifanyika mwaka wa 1950 na katika mkutano huu uongozi wa wazee wasomi wa enzi ya utawala wa Wajerumani, Mwalimu Thomas Saudtz Plantan aliyekuwa President na Clement Mohamed Mtamila, Secretary uliondolewa madarakani na viongozi vijana Dr. Vedasto Kyaruzi, President na Abdulwahid Sykes, Secretary uliingia madarakani kuongoza TAA.
Kwa nini ilichukua miaka minne kwa TAA kuitisha kile walichokuwa wakikiita ‘’Delegates Conference?’’
Swali hili nilimuuliza Tewa Said Tewa.
Jibu lake lilikuwa, ‘’Abdul Sykes aliyekuwa akitakiwa kuitisha mkutano huo alikuwa akisema tusubirini kwanza.’’
Mimi nilikamuuliza, ‘’Inakuwaje Abdul Sykes mtu mmoja ndiye aamue lini mkutano wa TAA uitishwe na akauchelewesha kwa miaka minne?’’
Mzee Tewa alinijibu kuwa, ‘’Sisi tukimtegemea sana Abdul katika kuendesha TAA hasa katika kutoa fedha za kuendesha chama hivyo tusingeweza peke yetu wanachama kufanya lolote bila ya yeye.’’
Mzee Tewa aliendelea na kunambia, ‘’Laiti kama Abdul angeliitisha mkutano mapema baada ya mkutano wa 1950 sisi tungeasisi TANU na Julius Nyerere asingeiwahi TANU.’’
Mazungumzo haya nimefanya na Mzee Tewa sasa miaka 40 iliyopita.
Abdul Sykes akiwa Act. President kuanzia 1951 na Secretary wa TAA aliitisha ‘’Delegates Conference,’’ tarehe 17 April, 1953 katika Ukumbi wa Arnautoglo.
Agenda kuu ya mkutano ule ilikuwa uchagiuzi wa viongozi.
Uchaguzi huu ni muhimu sana katika historia ya Tanganyika na katika historia ya Julius Nyerere.
Kabla ya uchaguzi huu mwanzoni mwa mwaka wa 1953 Abdul Sykes akiongozana na Ali Mwinyi Tambwe, Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) alifunga safari kwenda Nansio, Ukerewe kuonana na Hamza Mwapachu kupata kauli yake kuhusu suala la uchaguzi.
Katika suala hili la uchaguzi aliyekuwa anazungumzwa kuhusu kuchukua nafasi ya President wa TAA alikuwa Julius Kambarage Nyerere lakini palikuwa na tatizo.
Tatizo alikuwa yeye Abdul Sykes.
Ikiwa Abdul Sykes atagombea nafasi ya President na kusimama dhidi ya Julius Nyerere, Nyerere hatoshinda uchaguzi ule na sababu ni ule umaarufu wa akina Sykes katika siasa za Dar es Salaam ya 1950.
Mbali na hili chama chenyewe, yaani African Association (AA) kilianzishwa na baba yake mwaka wa 1929 na wamekiongoza na kuifadhili AA kutoka wakati huo.
Hamza Mwapachu alimwambia Abdul Sykes kuwa kwa kuwa kusudio ni kuunda chama cha siasa kilicho dhahir kudai uhuru wa Tanganyika, Julius Nyerere anafaa zaidi kuongoza harakati za za kudai uhuru chini ya TANU.
Usiku wa kuamkia uchaguzi Abdul Sykes alikwenda nyumbani kwa Tewa Tewa Said.
Tewa Said alikuwa anaishi Mtaa wa Stanley na Swahili jirani sana na nyumba ya Abdul Sykes Mtaa huo huo wa
Stanley nyumba ya Abdul ikiwa kwenye kona na Mtaa wa Sikukuu.
Abdul alimwambia Tewa kuwa, "Tewa kesho tunakwenda kumpa Nyerere chama na tukishampa hatutoweza tena kumnyang'anya. Mimi simjui vizuri huyu mtu lakini nategemea In Shaa Allah mambo yote yatakuwa sawa."
Kilichotokea katika uchaguzi ule pale Arnautoglo tarehe 17 Aprili, 1953 ni kuwa Julius Nyerere alishinda uchaguzi ule kwa kura chache sana akawa TAA Territorial President na Abdul Sykes Vice President.
Umuhimu wa uchaguzi huu ni kuwa historia ya Julius Nyerere katika TANU na kudai uhuru wa Tanganyika inaanza siku hii ya tarehe 17 Aprili, 1953 ndani ya Ukumbi wa Arnautoglo.
TANU ilipokuja kuandika historia yake na kuchapa kitabu mwaka wa 1981 jina la Abdul Sykes halikuwemo kitabuni.
Imekuwaje historia hii muhimu haijaandikwa na wanahistoria wote walioandika kuhusu historia ya Julius Nyerere, TANU na harakati za kudai uhuru?
Inawezekana hawakupata kuisikia?
Au ni kwa sababu waandishi wote walioandika historia ya TANU hakuwapata fursa ya kusoma Nyaraza za Sykes?
Lakini swali litakuja kwa nini wanahistoria hawa hawakuonekana kuvutiwa na historia ya ukoo wa Sykes lau kama mchango wao katika TANU ulikuwa unafahamika sana?
Utasikia inasemwa kuwa Nyerere alichukua uongozi wa TAA mwaka wa 1953.
Ilikuwaje akachukua uongozi huo hili halisemwi na Nyerere mwenyewe hajapata kueleza hadi anaingia kaburini.
Picha: Picha ya Kwanza Ukumbi wa Arnautoglo, ya pili kulia ni Lawi Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz katika dhifa Ukumbi wa Arnautoglo ya kumuaga Nyerere safari ya pili UNO 1957.
(Dhifa ya safari ya kwanza UNO 1955 ilifanyika kwenye jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika).
Picha ya tatu ni Tewa Said Tewa mmoja katika wazalendo 17 walioasisi TANU 1954.