TRA yakusanya Trilioni 7.27 kwa kipindi cha miezi 6

Thaman ya shilingi yetu dhidi ya dola pia imeporomoka kwa kiasi kikubwa... So hilo ongezeko la madafu ukipeleka kwenye dola utakuta ni kama buku mbili tu imeongezeka


Mkuu kwani mwaka jana kipindi kama iko dola ilikuwa inauzwa tsh ngapi na sasa ni shilingi ngapi? Kama kweli unauakika naomba jibu. Kama haujui naomba unyamaze kulinda heshima yako.
 
Hayo ameyasema Leo mkurungezi wa tra amesema serikali kupitia tra imekusanya kiasi cha 7.27 trillion kwa nusu mwaka ameyasema Leo .

Chanzo. Mwananchi
 
Trilioni 7.27 kwa miezi 6.Makusanyo kwa mwaka tunakadiria 14.54.
Bajeti iliyopitishwa 2016/2017 ni 29.5. Deficit 29.5-14.54 baki 14.9 trilioni. Naona tuko katika hali ngumu kiasi sasa tunahitaji 'usalama wa raia' washiriki kuwakamua wenye magari na madereva. Mwisho wa siku tunagawana faida na serikali.(Hasa gari za biashara roli,daladala,basi,bajaji nk)
Of course hii haihusishi makusanyo ya polisi, ada mbali bali kwe secta ya utalii na misitu. Hata hivyo tutahitsji wahisani (ambao sina uhakika wameshaleta chochote) kutusaidia.
 
Mr. Magu alivyo ingia madarakani alianza na mikwara sana, ukweli kila mtu alijaa hofu, si wafanya biashara si watumishi. Kwa hiyo watu wamelipa malimbikizo yao kwa kuogopa, ila sikilizia mwaka huu kama TRA watatangaza tena.

Tafuta sababu nyingine hii ameishaivuka
 
Makadirio ya makusanyo ya TRA kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ni trilioni 17 ,mpaka kufikia nusu ya mwaka tumekusanya trillion 7.2 tuu sijui tutatumia miujiza gani kukusanya trillion 10 nusu inayofuata .
Kwa kifupi ni kusema tumetengeneza bajeti kwa makadirio ya makusanyo yasiyotekelezeka .
Labda turudi bungeni tukafanye mapitio ya bajeti yatakayozingatia uwezo halisi tukizingatia zile tulizotegemea toka nje nazo haijulikani tutazipata lini .
Pili TRA wanataka kutuaminisha kuwa kuna ongezeko la makusanyo ukilinganisha na mwaka wa fedha uliopita licha ya ukweli kwamba baadhi ya vyanzo vya mapato vilivyokuwa chini ya halmashauri mwaka wa fedha uliopita sasa ni sehemu ya vyanzo vya mapato ya TRA kwa mwaka huu wa fedha .
Wakitka kufanya ulinganifu mzuri waondoe fedha zote zinazotokana na vilivyokuwa vyanzo vya halmashauri kisha walinganishe tuone kwa kiasi gani wameongeza mapato .
Vinginevyo huo ulinganifu ni batili .


Mmmmmh labda umechanganya si hapa Tanzania hiyo bajeti.
 
TRA imetangaza makusanyo yake kwa kipindi cha miezi 6 ni trilioni 7.27 kwa 2016/2017 ukilinganisha na trilioni 6.44 ya mwaka 2015/2016.

Kwa mwezi Disemba 2016 TRA ilikusanya trilioni 1.41.

=======

MAKUSANYO YA KODI KIPINDI CHA NUSU MWAKA WA FEDHA 2016/17


Katika kipindi cha miezi sita ya mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Disemba 2016, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27 ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi kama hicho mwaka wa fedha 2015/16.

Ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74.

Mlinganisho wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
View attachment 460952
Jitihada mbalimbali zinafanywa ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya majengo.

TRA inaendelea kuhimiza wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.

Pamoja na hayo tunawakumbusha na kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa zao kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika mikoa mingine.

TRA inatoa wito kwa wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake kikamilifu.

Kwa wafanyabiashara wenye madeni ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na Wilaya kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.

Wamiliki wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari .

Pamoja Tunajenga Taifa Letu’

17/01/2016

Richard M. Kayombo

MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI
ivi hawa wataacha lini kutudanganya
 
Watanzani bana yani mnasikitisha,elimu yenu ndogo ndio maana ccm wanatumia mwanya kuwalaghai,
Hakuna cha makusanyo ya matilioni wala nini,ni mbinu ya serikali kuwaondoa kwenye mjadala wa njaa,TRA inatumika tu kutuondoa ili tujadili makusanyo na tusahau mijadala ya njaa,shame on u ccm.
Hawa jamaa siwaamini kama waketudanga kwamba wana akiba ya chakula tan 1.5 milion .kumbe hakuna kitu. Ngoja kesho wataalam wa mambo ya kodi watakuja na data nyingine. Naona na za Bukoba zimo
 
Ayamakusanyoyamewavuanguo Chadema. Sikizote wanaombea TRA ishindwe kukusanyamapato.Lakini Mungu huwahamfichi mnafiki. Kwasasa kaulizao zinawaweka Uchi.
JPM endeleakukaza, Makusanyo yanaonekana. Mifisadi na mijizi inaendelea kulalamika. Sisiuku mtaani tunasema: ukisikia wapinzani wanalialia ujue dawainaingia. JPM Endelea kuongezadawa, Walizoeakutuibia.Pigabakora kisawasawa. Watanzania tuponyumayako.

Asante Mungukwa JPM Chadema walimtukanasana JK Japo alijitahidi, akawakaribisha chai Ikulu. Lakini walipotoka lkulu, walimtukana katikakiwangochajuu.Nawe ukakizuia kinywachake asiwajibu.Nawe Mungu uliyehai,umewajibu. Umemleta mtumishiwako JPM na sasa anaifanyakazi uliyomtuma.
 
Sasa serikali inapaswa ku formalise informal sector/underground economy...hii sector ni kubwa sana na haipaswi kudharauliwa..naamini 'undergroun economy' ikiwekwa chini ya radar ya TRA tunaweza kuongeza mapato kwa 40 au 50 percent..
 
BAJETI YA TANZANIA KWA MWAKA 2016...2017 NI TRILLION 29.345

MAKUSANYO HAYO MIEZI 6 NI TRILLION 7.27 ×2=14.54


bado sana



swissme
 
BAJETI YA TANZANIA KWA MWAKA 2016...2017 NI TRILLION 29.345

MAKUSANYO HAYO MIEZI 6 NI TRILLION 7.27 ×2=14.54


bado sana



swissme
Haitegemei mapato ya TRA tu, kuna vyanzo vingine kama mikopo na misaada pia. Hata hivyo mapato hutegemeana na vipindi, sema ukame nao utatuathiri kidogo.
 
Haitegemei mapato ya TRA tu, kuna vyanzo vingine kama mikopo na misaada pia. Hata hivyo mapato hutegemeana na vipindi, sema ukame nao utatuathiri kidogo.
Hakuna ukame tz mkuu acha uchochezi
 
Naona Kuna watu hawajafurahishwa na hii taarifa ususani wale wanaofikiria kuferi kwa serikali ya CCM.. Basi wahathirika ni wamalawi
Walete takwimu ya mapato angainst monthly collection budget tuone nayo ipoje maana September mapato yalikuwa chini ya malengo
 
Back
Top Bottom