Kuwa serious na mambo yakoduuh kwa miezi miwili hii jumla 200k imepotea
Kuwa serious na mambo yako
Kwenye suala la michango ya harusi nimegundua mambo kadhaa:Hello Wadau!!
Naenda Moja kwa Moja kwenye topic.
Mimi binafsi naenda kwenye style ya uombaji michango, Jana mishale ya mchana ghafla najikuta nimeungwa kwenye group la kuchangia mchango wa harusi ya classmate wangu ambae sijaongea nae Toka mwaka Jana japo Kila mtu ananamba ya mwenzake, naona ni pledges Tu zikiendelea.
Nimeamua nijikalie kimya Tu kama kashindwa kunipigia simu atajijua mwenyewe naona kanipunguzia mzigo maana michango ya Harusi ni mingi kuliko ada tunazolipia watoto Shule.
Mimi langu ni Hilo Tu, kwenye michango ya Harusi, ulikutana na Nini tujuze mdau..............
Tiririka.......
Any opinions kuhusu michango ya Harusi.
Uzi tayariiii!!!
Kweli inakeraMtu anataka kuoa mzigo unawaangukia wengine , insane.
Especially Birthday mtu anawakusanya then anataka mjilipie au akijitahidi anawalisha mishikaki miwilimiwili na keki mnaondoka.Harusi,birthday aisee michango inakera sana kama uwezi kumudu garama za party kubwa why ujisumbue na michango??mbaya zaidi usipochangia unaonekana mbaya
Ha ha ha Mimi nawapa watoto wachezeeHivi bado kuna watu wanatoa hii michango? Mi nikiletewa kadi naweka kwenye droo tu!! Mwingine amesosomola huko na Manzi wake mpaka wamezaa mitoto kibao,Eti wanakuletea kadi wanafunga ndoa,Aibu sana hawajishtukii tu.
Nakuunga mkono hizo point zote 3, siku hizi ni mwendo wa nipe nikupe, ukitoa undugu na mahusiano ya karibu kama hauna Cha kuongeza katika maisha ya wanaokuzunguka ni mwendo wa kupotezeana Tu.Kwenye suala la michango ya harusi nimegundua mambo kadhaa:
1. Uhusiano wako na watu wanaokuzunguka, kama ni mzuri hawatasita kukuchangia ukiwashirikisha jambo lako.
2. Status yako/uwezo wako kiuchumi(hili lipo sambamba na namba 1), nimeona jamaa katoa 1.2M kwa ajili ya harusi yake, sambamba na kulipia mambo mengine mbalimbali, halafu wadau wakamuunga mkono kwa kumchangia pia.
3. Kama wewe ni kapuku, huwezi kuwa na nguvu ya kuomba michango na watu hawawezi kukuchangia(ila kidogo tu) endapo ukiwaomba.
Niliwahi kusema hivi Kuna haja gani ya kuchangisha michango ya harusi ilihali una uwezo? Mnaumiza sana wasiokuwa na uwezo.