Toa neno lolote kuhusu michango ya Harusi

amadala

JF-Expert Member
Aug 20, 2017
4,265
12,236
Hello Wadau!!

Naenda Moja kwa Moja kwenye topic.

Mimi binafsi naenda kwenye style ya uombaji michango, Jana mishale ya mchana ghafla najikuta nimeungwa kwenye group la kuchangia mchango wa harusi ya classmate wangu ambae sijaongea nae Toka mwaka Jana japo Kila mtu ananamba ya mwenzake, naona ni pledges Tu zikiendelea.

Nimeamua nijikalie kimya Tu kama kashindwa kunipigia simu atajijua mwenyewe naona kanipunguzia mzigo maana michango ya Harusi ni mingi kuliko ada tunazolipia watoto Shule.

Mimi langu ni Hilo Tu, kwenye michango ya Harusi, ulikutana na Nini tujuze mdau..............

Tiririka.......
Any opinions kuhusu michango ya Harusi.
Uzi tayariiii!!!
 
Daaaa.....michango hii inakera wakati nikitaka kuoa nilikuwa mzito sana kuomba michango kwa washkaji .ila nikajikaza nikawacheki wanangu kama wawili hivi ..oyaa mwenenu nataka kuchukua chombo nipeni support yenu ila kiukweli nlikuwa najua kabisa wana hawana mishe za kueleweka nlitaka tu wajue kuwa nimewaomba michango ila sikuzingatia sana......ila wengine wote niliwaambia tu naoa lakin sikuomba mchango kwa mtu wala ndugu...na budget yangu ya harusi ilikuwa 120k tu......

Nilijipanga kwa hilo sikutaka show off.hata ndugu kwenye vikao vyao niliulizwa bwana harusi unachangia ngapi katika budget nikasema hali mbaya lakin sio kweli.sikutaka mambo mengi.Na chakushangaza tunaishi gheto watu wanne na jamaa hawajui jamaa akioa tutaishi vipi.kumbe kuna kimjengo pemben nlishajenga kimya kimya na hela za kubutua .........

Harusi sio michango

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Hello Wadau!!
Naenda Moja kwa Moja kwenye topic.
Mimi binafsi naenda kwenye style ya uombaji michango, Jana mishale ya mchana ghafla najikuta nimeungwa kwenye group la kuchangia mchango wa harusi ya classmate wangu ambae sijaongea nae Toka mwaka Jana japo Kila mtu ananamba ya mwenzake, naona ni pledges Tu zikiendelea.
Nimeamua nijikalie kimya Tu kama kashindwa kunipigia simu atajijua mwenyewe naona kanipunguzia mzigo maana michango ya Harusi ni mingi kuliko ada tunazolipia watoto Shule.
Mimi langu ni Hilo Tu, kwenye michango ya Harusi, ulikutana na Nini tujuze mdau..............
Tiririka.......
Any opinions kuhusu michango ya Harusi.
Uzi tayariiii!!!
Kwenye suala la michango ya harusi nimegundua mambo kadhaa:

1. Uhusiano wako na watu wanaokuzunguka, kama ni mzuri hawatasita kukuchangia ukiwashirikisha jambo lako.

2. Status yako/uwezo wako kiuchumi(hili lipo sambamba na namba 1), nimeona jamaa katoa 1.2M kwa ajili ya harusi yake, sambamba na kulipia mambo mengine mbalimbali, halafu wadau wakamuunga mkono kwa kumchangia pia.

3. Kama wewe ni kapuku, huwezi kuwa na nguvu ya kuomba michango na watu hawawezi kukuchangia(ila kidogo tu) endapo ukiwaomba.

Niliwahi kusema hivi Kuna haja gani ya kuchangisha michango ya harusi ilihali una uwezo? Mnaumiza sana wasiokuwa na uwezo.
 
Nakuunga mkono hizo point zote 3, siku hizi ni mwendo wa nipe nikupe, ukitoa undugu na mahusiano ya karibu kama hauna Cha kuongeza katika maisha ya wanaokuzunguka ni mwendo wa kupotezeana Tu.
 
Michango ya Harusi na michango makanisani ni chanzo kingine cha Umasikini kuliko hata kuhonga Malaya..
Umenikumbusha michango ya Kanisani ha ha ha sisi tupo kwenye ujenzi wa kanisa🙌
 
Back
Top Bottom