SoC04 Timu za mpira wa miguu ziwe huru kibiashara

Tanzania Tuitakayo competition threads

pute kitogo

Member
Apr 26, 2024
5
2
TIMU ZA MPIRA WA MIGUU ZIWE HURU KIBIASHARA.

Kipindi cha wakoloni mataifa ya Afrika yalitawaliwa na nchi zilizoendelea hadi zenyewe zilishidwa kuendela, ukiangalia kwa macho ya kawaida utasema wakoloni walileta maendeleo kwa sababu walijenga barabara, Treni, Shule hadi baadhi ya wapigania uhuru kama Nyerere walisoma ila je walifanya yote kwa masilahi yetu au yao? na walifanya hayo kwa lengo la kuendelea nchi zetu au zao? na kwa nini tulipigania uhuru ingawa walifanya yote hayo??

Tujue walifanya yote kwa maslahi yao na sio yetu waliwasomesha baadhi ya Waafrika wenzetu ili wawasaidie kwenye kazi zao ingawa iliwatokea puani, pia lengo ni kuziendeleza nchi zao na sio zetu ndiyo maana hata Treni walizojenga walifanya hivyo kwenye sehemu ambazo watapitisha mizingo yao ya kibiashara ili wasafirishe kwa haraka kuelekea kwenye masoko mbalimbali duniani wauze kwa haraka na wapate pesa za kuziongoza nchi zao na ukiulizwa kwa nini tulipigania uhuru kwa sababu sisi hatukuwa huru kwa kila jambo ndio maana tulipigania uhuru wa mataifa yetu.

Tutoke huko turudi 2024 je wawekezaji, wadhamini na wamiliki wa timu zetu za mpira wa miguu tunasikiliza matakwa yao na sheria zao ni kwa ajili ya kuendeleza mpira wetu au wanatutumia kukuza tu biashara zao? Huku viongozi wakitajirika.

Ninazilenga timu zote zinazocheza kuanzia ligi kuu kushuka chini ila nitagusia hasa ligi kuu, kukosa uhuru lazima kuwepo na watu wawili anayefanya mwenzie kukosa na anayenyimwa huru je kwenye mpira sasa hivi watu hao ni wakina nani? Kuna wawekezaji/Mmiliki wa Timu na Klabu (Timu) anayenyimwa huru wa kibiashara.

Mwekezaji au Mmiliki wa Timu anaponunua timu, kuanzisha timu au kununua hiisa za timu na yeye akiwa na kampuni zake atalazimisha kampuni zake ziwe zinatangazwa na Timu hiyo husika aliyoinunua au kuanzisha ndipo panatokia kuminywa kwa uhuru wa kibiashara pale timu inaposhidwa kufanya biashara na kampuni zingine ambazo ni mshindani wa boss wa timu.

Hii mara yingi inatokea tajiri akiwa muwekezaji au muanzilishi wa timu ila akiwa mdhamini sio tatizo, kuna mtu atasema sasa ameanzisha timu si anayohaki ya kufanya chochote anachotaka sawa ila kwa maslahi ya nchi na yakisoka lazima tuweke sheria ili kuokoa biashara ndani ya timu zetu na wakufanya haya ni TFF kwa kushirikiana na serikali na viongozi wa timu.

Niweke kitu sawa kwanza kuna utofauti mkubwa kati ya mdhamini na muwekezaji/mmiliki wa timu, Mdhamini anaweza kuwa kampuni, Taasisi au mtu ambaye anatoa kiasi fulani cha pesa walichokubaliana kimkataba na Timu husika ili klabu hiyo itangaze biashara au bidhaa zake, Mmiliki ni aliyeinunua timu na mara nyingi timu hii haina umiliki wa wanachama labda wanahisa, muwekezaji ni anayewekeza pesa baada ya kununua hisa fulani kwenye klabu ili apate faida, kuna ulazima upi wa muwekezaji/mmiliki wa timu wawe wadhamini maana hili ni tatizo kubwa sana ambalo vinaipa wakati mgumu baadhi ya vilabu vya soka hapa nchini wanashidwa kujiendesha yenyewe kibiashara.

Kuminya uhuru wa kibiashara unatokea pale muwekezaji kuwekeza timu zaidi ya moja na mmiliki wa timu kumiliki timu zaidi ya moja au yeye kuwa mdhamini kwenye timu nyingine hapa kuna tokia kuminywa kwa uhuru wa kibiashara au unaweza sema ni ukoloni kwenye timu zetu za mpira wa miguu mambo haya yakome na wakufanya haya ni TFF, Serikali na viongozi wa Timu kwa kuweka sheria kali kukomesha haya kwa sababu yanatufanya tushidwe kuendelea na kufika mbali.

Mpira wa miguu sio mchezo wa kulipana fadhila hapana mchezo huu ni wa kukupa shukrani kwa uliyofanya ukisema ulipe fadhila utashidwa kuendelea mfano mzuri wa mambo haya kwa sasa hivi ni Simba, Azam, Singida na Yanga hasa Simba na Azam.

Mo pale simba ni muwekezaji na mdhamini wa timu lazima atoe hela yingi, atoe hela kama muwekezaji na mdhamini tunaona kila siku analalamika anatoa hela yingi je ajioni kama ameshikiria kofia mbili zote pekee yake swali la kujiuliza je anatoa pesa sawa kwenye udhamini wa bidhaa zake na Taasisi zake au ndiyo tunalipa fadhila kwa sababu ni muwekezaji basi bidhaa tangaza bure au tunakupunguzia.

Shabiki wa simba samahani ila hapa tunajenga sio kubomoa jiulize M-Bet inatoa kiasi gani simba na kwa miaka mingapi? Je Mo energy, Mo sabuni na Mo foundation wanatoa kiasi gani na kwa miaka mingapi? Kama anatoa angalia ni yingi au ndogo wametofautiana kiasi gani na M-Bet anachotoa ndiyo kinachostahili halafu rudi kwa Mo kiasi anachosema ametoa kwa simba tangu aingie Simba ni kikubwa kama anachosema au kidogo ndicho kinachostahili ?

Twende kwa Azam tajiri sawa ni timu yake lakini pesa anayotoa akitangaza bidhaa zake ndicho kinachostahili? Kuilipa klabu au ndiyo ile biashara ya kulipana au kujipa fadhila? Je tukiangalia timu kama timu inajiendesha yenyewe au bado kila siku hodi kwa mmiliki wa timu na je timu ya kisasa inatakiwa iwe kwa mtindo huo?

Singida Fc nayo mtihani mmiliki wa timu shabiki wa yanga kabla ya kuuzwa, je zikikutana timu hizi tutahisi vipi moja ikishinda tuache hilo mchezaji akitaka kuuzwa atauzwa kihaki? matatizo haya yanafanya timu isiwe huru kibiashara na matokeo yake timu moja inapata hasara mfano Simba inamtaka mchezaji singida wameweka million 100 na yanga wanamtaka wameweka 50 mchezaji huyo ataenda wapi?

TFF kwa kushirikiana na viongozi pamoja na Serikali wanatakiwa waweke sheria hizi ili kuifanya timu iwe huru kibiashara
•marufuku mtu anayetaka kudhamini au kuwa muwekezaji kwenye timu fulani hatakiwi kuwa shabiki au mwanachama wa timu yingine aidha awe wanachama au shabiki wa timu hiyo au asiwe shabiki au mwanachama wa timu yoyote
• kampuni, Taasisi na kadhalika akitaka kudhamini au kuwa muwekezaji anatakiwa mmiliki, wamiliki au moja wa wamiliki wa Kampuni au Taasisi hiyo hatakiwi kuwa shabiki au wanachama wa timu yingine unatakiwa uwe shabiki au mwanachama wa timu hiyo au usiwe wa timu yoyote
• kampuni yoyote haitakiwi kuwekeza au kudhamini timu zaidi ya moja
• mtu, kampuni, Taasisi na kadhalika unatakiwa uchangue kimoja kati ya udhamini au uwekezaji nasema hivi kwa sababu tumeona watu wakiingia kama wadhamini baadae wawekezaji na bado wadhamini na wengine waliingia kama wawekezaji baadae wanakuwa pia wadhamini halafu analalamika pesa anatoa nyingi na ukichangua kimoja kati ya hizo unatakiwa kuruhusu kampuni zingine ziwe muwekezaji au mdhamini hautaki kwa sababu anayeingia mshindani kibiashara basi wasaidie timu kupata mdhamini au muwekezaji wengine.

Tuondoe ukoloni uliyokithiri kwenye soka letu ili tuendele.
 
Mwekezaji au Mmiliki wa Timu anaponunua timu, kuanzisha timu au kununua hiisa za timu na yeye akiwa na kampuni zake atalazimisha kampuni zake ziwe zinatangazwa na Timu hiyo husika aliyoinunua au kuanzisha ndipo panatokia kuminywa kwa uhuru wa kibiashara pale timu inaposhidwa kufanya biashara na kampuni zingine ambazo ni mshindani wa boss wa timu
Ni biashara bro na anayedhamini anafanya hivyo kwa faida ya wote ya timu na ya kwake win win.


Tujue walifanya yote kwa maslahi yao na sio yetu waliwasomesha baadhi ya Waafrika wenzetu ili wawasaidie kwenye kazi zao ingawa iliwatokea puani, pia lengo ni kuziendeleza nchi zao na sio zetu
NIkikuiliza swali Je? Huoni kwamba ndani ya sentezi zako upo ushahidi kwamba wahusika wote walifaidika kwa kiasi fulani?
Singida Fc nayo mtihani mmiliki wa timu shabiki wa yanga kabla ya kuuzwa, je zikikutana timu hizi tutahisi vipi moja ikishinda tuache hilo mchezaji akitaka kuuzwa atauzwa kihaki? matatizo haya yanafanya timu isiwe huru kibiashara na matokeo yake timu moja inapata hasara mfano Simba inamtaka mchezaji singida wameweka million 100 na yanga wanamtaka wameweka 50 mchezaji huyo ataenda wapi?
Kweli hapo kuna muingiliano kimaslahi na matakwa binafsi.

Mwishoni umetoa pointi nzuri, tujitahidi tu sheria zimnufaishe yeyote anayehusika na wote wanaohusika. Na kama timu ikiona kuwekezwa inakula hasara basi ikatae ibakie tu kuwa na wadhamini.

Pointi moja tu ya kuchekesha ni kwamba, muwekezaji huyo mwenye hisa anapata hasara kama tu ambavyo timu inapoteza mapato maana ndiye mwenye timu, je unajuaje kama kwake ameshafanya mahesabu na kuona inamlipa? Hapo wa kukataa ni timu yenyewe kuona biashara na wadhamini VS wawekezaji ipi inailipa zaidi?

Hivi na sie, ni kwanini kusiwe tu na umilikaji wa pamoja kwenye timu (crowd funding)?
 
Ni biashara bro na anayedhamini anafanya hivyo kwa faida ya wote ya timu na ya kwake win win.



NIkikuiliza swali Je? Huoni kwamba ndani ya sentezi zako upo ushahidi kwamba wahusika wote walifaidika kwa kiasi fulani?

Kweli hapo kuna muingiliano kimaslahi na matakwa binafsi.

Mwishoni umetoa pointi nzuri, tujitahidi tu sheria zimnufaishe yeyote anayehusika na wote wanaohusika. Na kama timu ikiona kuwekezwa inakula hasara basi ikatae ibakie tu kuwa na wadhamini.

Pointi moja tu ya kuchekesha ni kwamba, muwekezaji huyo mwenye hisa anapata hasara kama tu ambavyo timu inapoteza mapato maana ndiye mwenye timu, je unajuaje kama kwake ameshafanya mahesabu na kuona inamlipa? Hapo wa kukataa ni timu yenyewe kuona biashara na wadhamini VS wawekezaji ipi inailipa zaidi?

Hivi na sie, ni kwanini kusiwe tu na umilikaji wa pamoja kwenye timu (crowd funding)?
Kuna moja atakandamizwa bro kuna ttz kubwa kwenye hili maana wengi hawajui biashara ya mpira inahitaji nn
 
Back
Top Bottom