MwananchiOG
JF-Expert Member
- Apr 4, 2023
- 2,131
- 4,280
Habari za ndani zinaeleza, Uongozi wa club ya Young africans imeketi na kuamua kuipeleka TFF katika mahakama za juu za FIFA kufuatia shirikisho hilo kuufuta mchezo namba 148 wa Ligi kuu bila sababu za msingi kinyune na sheria na taratibu za Ligi kuu bara.
Kwa mujibu wa kanuni na taratibu za Ligi, sababu pekee zinazoweza kusababisha mchezo kuahirishwa ni kifo cha mchezaji, hali mbaya ya hewa, au sababu kubwa kulingana na itakavyobainika.
Soma Pia: Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba
Nje ya hapo kanuni zinalazimu mchezo kuchezwa kisha kama kuna dosari au changamoto yoyote hatua huchukuliwa baada ya mchezo husika ikiwemo kutozwa faini au wahusika kufungiwa.
Hii italeta doa kubwa katika Ligi ya Tanzania.