Headcorner
Senior Member
- Nov 26, 2020
- 199
- 291
- Thread starter
- #21
gharama za mchezo ml 22??
Watu wanajenga kupitia mechi za derby mkuu hapo mlolongo wa watu wanaopiga hela ni mkubwa sana na ni ngumu kuwakamata.Ukweli ni kwamba hata kama Simba au Yanga angekua na uwanja wake hapa angeokoa milioni 47 tu.
Vat ingelipwa hiyo hiyo, BMT wangechukua kiasi hiko hiko, Hapo kwenye gharama za ticket kungebaki hivyo hivyo, gharama za mchezo na mambo mengine yote.
Ni wakati wa kuuliza maswali sahihi
1 ) BMT wanachukua hela za nini wakati wao ni serikali na serikali imeshachukua pesa pale kwenye VAT
2) Gharama za ticket zinafikaje milion 22 wakati ticket ni za electronic
3) Gharama za mchezo mchanganuo wake upoje? Wanalipwa wakina nani? Kwa nini?
4) TFF, TPLB, FA tofauti yake ni nini maana viongozi ni wale wale wanabadili kofia tu kubeba maokoto
5) Gharama za kukodi uwanja zinakaribiaje milioni hamsini na unakwenda unakuta uwanja mchafu, viti vichafu, vyoo vichafu na hakuna huduma yoyote zaidi ya kukaa tu?
Imefikia pahala limeshakuwa chaka la maokoto na hatuwezi kusogea kwa style hiyo.
Hizo nadhani ni siti maalumu zisizolipiwa ( Hela inaingia Simba moja kwa moja).Halafu mbona kwenye huu mchanganuo hakuna ticket za platinum ( 150,000/=) na executive ambayo ni sh 40,000/=
Inamaana Simba walizitangaza lakini hazikupata mteja hata mmoja au inakuaje. Hapa upigaji ni kupita kiwango aisee
Viongozi wa Yanga na simba miaka nenda wamejawa na siasa, ubabaishaji na porojo tu. Uwezo wa kujenga viwanja vyao wanao (hata kwa awamu)! Lakini miaka nenda utekelezeji 0!Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023, wadau mbalimbali wametoa maoni yao kufuatia timu mwenyeji (Simba)kuambulia sh 188,987,181.10 tu katika mapato yote yaliyopatikana, kuna haja ya timu hizi kuwa na Viwanja vyao kukwepa Unyonyaji huu.
Shirikisho la mpira wa miguu hapa nchini limetoa taarifa ya mapato ya Mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga ambao ulifanyika jumapili iliyopita tarehe 16/4/2023, wadau mbalimbali wametoa maoni yao kufuatia timu mwenyeji (Simba)kuambulia sh 188,987,181.10 tu katika mapato yote yaliyopatikana, kuna haja ya timu hizi kuwa na Viwanja vyao kukwepa Unyonyaji huu.
BMT (Baraza la michezo Tanzania) wanachukua mgao kwa kipi wakati tayari kuna VAT?
TFF na TPLB zote ni taasisi inayofanya kazi pamoja, kwanini ela zigawanyike kwa taasisi zote mbili badala ya kuingia upande wa TPLB peke yake?
Kama kulikuwa na gharama ya uwanja na gharama ya mchezo, FA mkoa wanapewa ela kwaajili ya lipi?
Gharama ya kutengeneza tiketi ni mil 22+ mh haya watu wenye fani zao wanaweza kujua kama ni sahihi au sio sahihi.
Kwa mgawanyo huo, hata kama timu ikijenga uwanja wake, kitachoongezeka kwenye gawio la team ni pesa za uwanja pekee. VAT, BMT, TPLB, TFF na sijui kina nani wengine wataendelea tu kuchukua chao.