Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,594
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepokea taarifa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuzuiya wimbo uitwao "Amkeni" uliopigwa na mwanamuziki Emmanuel Elibariki (Nay wa Mitego) kutopigwa katika mitandao ya kijamii na vombo vya habari.
Aidha, kwa mujibu wa BASATA, maudhui ya wimbo huo yana melekeo wa kutaka wananchi wasiwe na imani na Serikali, kuchochea wananchi kuwa na mapokeo hasi juu ya utekelezaji wa mipango ya Serikali yao kwa ujumla, na kuwa ni wimbo wa uchochezi baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi wake.
Hivyo, kwa barua hi, TCRA inaelekeza chombo chako cha habari kutopiga wimbo huo.
Tafadhali zingatia maelekezo.
Pia soma: Nay wa Mitego aitwa BASATA. Atuma Wanasheria wake