SoC04 Tanzania ya Viwanda tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Edson Eagle

Member
Apr 20, 2024
26
11
Mambo yakutekerezwa katika miaka ijayo ndani ya sekta ya viwanda.
1. Kuboresha miundombinu (barabara, umeme, usafiri na maji) pamoja nakufufua viwanda vyote vilivyokufa katika maeneo mbalimbali.
2. Kuwa na sera inayosimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha waajiriwa katika viwanda wanapata ujira unaoendana na ugumu wa kazi zao na sio kuwanyonya.
3. Kuongeza uzalishaji wa malighafi(raw materials) katika maeneo mbalimbali zinazoendana na viwanda vilivyopo katika maeneo hayo, lengo ni kuvihudumia viwanda husika nasio kinajengwa kiwanda hata marighafi hazijulikani zitatoka wapi na mwisho viwanda vinakufa.
4. Kuboresha nakuongeza viwanda vinavyozalisha bidhaa zenye uhitaji mkubwa kwa Watanzania hususani viwanda vya sukari. Lengo nikukidhi mahitaji ya watu nasio kufikia hatua ya kusubiri sukari kutoka nje ya nchi.
5. Kuendelea kutenga maeneo kwaajiri ya viwanda tu mbali na makazi ya watu kiusalama zaidi.
6. Kuangalia namna nzuri yakupunguza madhara yatokanayo na viwanda ikiwa ni pamoja na matumizi ya mitambo ya kisasa isiyozalisha taka nyingi lakini pia upandaji wa miti uongezeke kwa kiwango kikubwa.
7. Kuenderea Kuruhusu uwekezaji toka nje wenye manufaa zaidi kwa Watanzania (yaani ajira na mapato kwa Taifa) na kwa kiwango kisicho na madhara.
8. Kutengeneza fursa za ajira kwa Watanzania wasomi na wasiosoma kwa kadri ya uhitaji katika sekta hii ya viwanda, na sio kiwanda kinahitaji wafanyakazi 250 lakini waliopo ni 140 hapo hatuendi mbele bali tunarudi nyuma.
9. Kuboresha teknolojia viwandani ili kuongeza uzalishaji wenye kasi zaidi ya speed ya 4G.

Lakini pia naishukuru serikali kwa hatua iliyopiga katika sekta ya viwanda mpaka sasa. Na izidi kuboresha zaidi na zaidi kama nilivyopendekeza hapo juu katika baadhi ya mambo ili tupige hatua zaidi ya tulipo.
Screenshot_20240504-083947.png
 
2. Kuwa na sera inayosimamiwa kikamilifu ili kuhakikisha waajiriwa katika viwanda wanapata ujira unaoendana na ugumu wa ka
Ewaah, tusije kuwa watumwa katika nchi yetu tena. Kila mtendakazi anastahili ujira wake stahili

Kuangalia namna nzuri yakupunguza madhara yatokanayo na viwanda ikiwa ni pamoja na matumizi ya mitambo ya kisasa isiyozalisha taka nyingi lakini pia upandaji wa miti uongezeke kwa kiwango kikubwa.
Au hata ile 'zero waste' yaani taka inayotoka kwenye kiwanda hiki inakuwa malighafi ya kiwanda kingine.

Lakini pia naishukuru serikali kwa hatua iliyopiga katika sekta ya viwanda mpaka sasa. Na izidi kuboresha zaidi na zaidi kama nilivyopendekeza hapo juu katika baadhi ya mambo ili tupige hatua zaidi ya tulipo.
Tunasonga mbele, hata kama ni mdogo mdogo ila tunajongea
 
Back
Top Bottom