Tanzania Tuitakayo competition threads
May 24, 2024
32
45
Tanzania ni nchi iliyojaliwa kudumisha amani ya muungano wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar tangu tarehe 26 Aprili, 1964 barani Afrika na kubarikiwa rasilimali za kipekee kutoka kwa mwenyezi Mungu zenye tija ya maendeleo. Mfano: madini ya tanzanite.
TANZANIA TUITAKAYO miaka 5-25 ijayo. Si rahisi kwa asilimia zote kufikia ubora tutakavyo kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi. Tanzania haijafanikiwa vizuri kutumia rasirimali watu kuleta maendeleo na miradi endelevu kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia pasipo kutegemea misaada inayosababishwa na upungufu wa bajeti kuu ya sarikali.
1719246265898.png

Wizara.ya.fedha,Hotuba.ya.waziri.wa.fedha 2024/25.(2024,juni.13),172.
Muhimu serikali na wananchi kuwa tayari kuboresha nyanja zinazogusa
rasirimali watu kwenye jamii. Nyanja muhimu zinazohitaji maboresho na usimamizi kwa TANZANIA TUITAKAYO ya miaka 5-25 ijayo ni kama ifuatavyo: -


MAFUNZO YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA.
Mtaala wa wizara ya elimu, sayansi na teknolojia Tanzania, unaunganisha kila mwenye ujuzi kuwa na chachu ya maendeleo endelevu. Ni vyema Tanzania kuweka maboresho mazuri kwenye taasisi za mafunzo ya Elimu.
Mfano: mitaala ya mabadiliko ya tabia ya nchi ya sayansi na teknolojia. Kujifunza kwa vitendo ili wanaomaliza masomo kuwa na wigo mkubwa wa ajira, pasipo kusoma nadharia pekee ambazo wakiwa kazini wanakutana na mifumo ya mitandao wasiyokuwa nayo msingi.
Kuhamasisha matumizi ya Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA): maendeleo ya sayansi na teknolojia yameiweka dunia kiganjani. cha ajabu mwanafunzi wa kidato cha sita tanzania hasa vijijini anahitimu masomo hafahamu pia hana mawasiliano ya barua pepe mpaka wakati wa kuomba mkopo ndio aanze kujikwamua kufahamu tovuti mitandaoni. vuta picha akiwa chuoni na ulimbukeni wa matumizi ya teknolojia; mfano: matumizi ya
kompyuta na projekta wakati wa kujifunza itampelekea kukosa umakini kwenye masomo yake.
1719246437759.png

Darasa.la.mafunzo.ya.compyuta.kwa.vitendo:
Kipaumbele cha mkopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu: taifa linahitaji wataalamu wenye ujuzi na weledi wa utendaji kazi; hivyo wanafunzi wawezeshwe kutimiza ndoto zao ili kuepuka vitendo vya uhalifu kama utapeli.
1719246511515.png

Jamiiforums.instagram.(2024,aprili.19).Imepatikana,juni.24,2024,https://www.instagram.com/p/C57dYm6ty1i/?igsh=bXNrdmZqd3RhejVx
Akili mnembe: matumizi ya akili bandia maarufu (AI) mfano “ChatGPT”. Ni vizuri watumiaji hasa wanafunzi wapewe elimu ya kutumia kama fursa ya kujiboresha kiuchumi. Mfano, kusoma mafunzo tofauti ili kupata ujuzi zaidi utakaowawezesha kujiajiri kwenye shughuli za uvumbuzi wa biashara na ujasiriamali.
1719246815685.png

Mfano,ujuzi.wa.kujifunza.ujasiriamali.Akili-bandia.

AFYA, JINSIA NA MALEZI.
Tanzania iweke maboresho kuyakabili magonjwa hatari ya mlipuko kwenye vituo vya kutolea huduma. mfano: wanafunzi shuleni wahimizwe kufanya mazoezi yanayowasaidia kupunguza
mihemko na magonjwa yanayoweza kuathiri masomo yao ili tupate wataalamu wenye afya njema.
1719247031103.png

Mazoezi.ya.kuimarisha.viungo:
Semina za afya ya akili kwa wanaopitia ugumu wa Maisha, ajali na mahusiano ili kupunguza
unyanyasaji na ukatili wa kijinsia.
IMG_7213.jpeg

Jamiiforums.instagram.(2024,mei.13).Imepatikana,juni.24,2024,https://www.instagram.com/p/C66XqNgtrTJ/?igsh=bGNzb2xpM3JkbHF2
Pia, wazazi na vituo vya malezi kudhibiti, kusimamia na kulinda ndoto za Watoto kwa taifa la kesho kuepuka athari za makundi hatarishi ya madawa ya kulevya na ushoga ili kulinda nguvu kazi ya taifa.
Tazama:MillardAyo.YouTube.(2024,februari.6).Imepatikana,juni.24,2024,https://youtu.be/AxIUmqZyPY4?si=RtEtKMxKksedRaeS


MAZINGIRA, UTALII NA UWEKEZAJI.
Mazingira ni kichocheo cha shughuli endelevu; mfano: shughuli za utalii na uwekezaji. tanzania imejihakikishia utajiri wa asili kutoka kwa mwenyezi mungu. Tanzania isimamie vyanzo vya Maji kwenye uzalishaji wa nishati ya umeme, shudhuli za uvuvi na usafirishaji, misitu na uoto wa asili kwenye maendeleo ya
utalii wa Wanyama pori, hewa safi na shughuli za ujenzi na samani. Pia, ardhi yenye rutuba kwa shughuli za kilimo na uwekezaji wa uchimbaji wa madini ya thamani kama dhahabu. Hivyo, Tanzania iboreshe mazingira rafiki kwa watalii na wawekezaji wanaochangia pato kubwa la taifa kutokana na ajira nyingi zinazowafanya waendelee kuaminika.
Tazama:WasafiMedia.YouTube.(2023,mei.27).Imepatikana,june.24,2024,https://youtu.be/wCLtWS9Dv6s?si=wXEJj-e4D7qilWvn


UCHUMI, MIUNDOMBINU NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA.
ni nguzo ya maendeleo ya kiuchumi Tanzania. Tanzania iboresheshe njia za uendeshaji shughuli za kiuchumi pasipo kuwepo kwa kodi kandamizi na rushwa. Mfano: mawasiliano na vibali kwenye Soko la biashara mtandaoni kimataifa ambalo limekuwa kwa kasi kutokana na mapinduzi ya mitandao ya kidijitali. Kuweka wigo mkubwa wa kudumisha uhusiano wa tanzania baina ya mataifa mengine hasa mashirika na sekta binafsi kiuchumi. Mfano: miundombinu ya bandari na viwanja vya ndege kwa usafirishaji wa malighafi na bidhaa kimataifa ili kuongeza uzalishaji viwandani.

Tazama:EastAfricaTV.YouTube.(2023,Agosti.10).Imepatikana,juni.24,2024,https://youtu.be/PE1I_WWeANI?si=U2HfJLqo2FDFE1Us

ULINZI, USALAMA NA MUUNGANO.
Tanzania iwaimarishie wananchi kupata usawa, haki na usalama wa mali zao hasa ulinzi mtandaoni. kumekuwepo udukuzi wa taarifa na utapeli kupitia viungo mtandaoni; hii ni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kila kitu kinafanyika na kuhifadhiwa mtandaoni. Pia, kusimamia na kudhibiti uchochezi unaovuruga amani ya muungano kupitia mitandao. Tanzania ilitazame kwa umakini na weledi mkubwa ili kujenga uaminifu kati ya vyombo vya usalama na wananchi wake.
IMG_7209.jpeg

Jamiiforums.instagram.(2024,Aprili.15).Imepatikana,juni.24,2024,https://www.instagram.com/p/C5xUAMUte0W/?igsh=eWkzdWppMDVyaTV5

SIASA, DEMOKRASIA NA UZALENDO.
Tanzania iboresha mbinu bora za kisiasa zilizo na masilahi ya haki za binadamu na uzalendo wa wananchi kwenye Taifa lao.
Mfano: mafunzo kwa vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa kuondoa dhana ya jukumu la ulinzi na usalama ni kazi ya vyombo vya usalama kama jeshi la polisi. Uwajibikaji kulijenga taifa la kesho kwa siasa tulivu zisizoleta
taharuki kwa kuleta sera za kizalendo zinazosimamia katiba ya nchi na si vinginevyo. Mfano: historia fupi ya Tanzania na muundo wa serikali na itifaki zake lihimizwe kwa vijana wengi kushiriki kwenye ujenzi wa taifa.
IMG_7210.jpeg
Jamiiforums.instagram.(2024,Aprili.22).Imepatikana,juni.24,2024,
View: https://www.instagram.com/p/C6DK8VEIDwA/?igsh=OHJkMWZvNHZ3Nzdv


SANAA, MICHEZO NA UTAMADUNI.
Tanzania iboreshe na kusimamia thamani ya ajira itokanayo na tasnia ya sanaa, michezo na utamaduni kukuza pato la taifa. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameibua michezo mingi ukiachana na michezo inayofahamika kwa wengi mfano mpira. Elimu kwenye michezo ya kubahatisha iwe fursa ya ajira tofauti na inavyotumika kujikimu matumizi madogo badala yake waitumie kama shughuli zingine za kiuchumi zilizo na hatari ya kupata na kukosa. Pia, utamaduni uwekewe kipaumbele kuongeza ajira kwa vijana wengi wa kitanzania; mfano: ngoma za asili kudumisha utamaduni na kipato.


HITIMISHO.
Tanzania tukubaliane na mabaliko ya dunia ya sayansi na teknolojia kwa maendeleo endelevu nchini kwani kila kitu kimerahisishwa duniani. Na kudumisha amani ya muungano kuipeleka Tanzania sehemu salama kwa vizazi vijavyo.
IMG_7211.jpeg

Jamiiforums.instagram.(2024,Aprili.23).Imepatikana,june.24,2024,

View: https://www.instagram.com/p/C6FxPeyttmk/?igsh=MWcxdzV2NW81ZmV1Zw==


MAREJELEO YA UBUNIFU WA CHAPISHO.

 

Attachments

  • 1719248490463.png
    1719248490463.png
    746 KB · Views: 4
  • 1719248681373.png
    1719248681373.png
    746 KB · Views: 2
  • 1719248966431.png
    1719248966431.png
    746 KB · Views: 4
Back
Top Bottom