Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 64,538
- 116,187
Nawasalimu kwa jina la jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Elimu ya sekondari imekua ni muhimu kwa watu wote (elimu msingi), lengo ni kuwa kila mtu walau afike kidato cha nne. Ni jambo jema....lakini kumekua na changamoto nyingi kiasi cha kushindwa kufikia malengo kwani pamoja na kwamba kila mtu ahitimu kidato cha nne lakini pia elimu hiyo inapaswa kumnufaisha.
Kwa kuzingatia shule za kata, hizi shule ni msaada kwa watoto wengi kwani kumekua na nafasi kubwa kwao kuchaguliwa na kuendelea kupata elimu ya sekondari. Lakini shule hizi zinachangamoto ambazo inahitaji maboresho makubwa ili kufikia malengo
1: Idadi kubwa sana ya wanafunzi ambayo haina uwiano na idadi ya walimu, mfano shule hizi ni kawaida kukuta zina wanafunzi 2000+ na walimu wasiozidi 40 kwa haraka tu hakuna kabisa uwiano.
2: Wanafunzi wasiojua kusoma wala kuandika (najua inashangaza ni vipi mwanafunzi anafika sekondari hajui kusoma wala kuandika) alishindwaje zile KKK na amewezaje kufaulu kupangiwa sekondari. Hii inaweza kuwa inachangiwa pia na mitihani ya kushade kiuhalisia inapunguza uwezo wa wanafunzi akifanikwa kuangalizia basi anafaulu wakati hajui chochote. Na hili ni tatizo serious mwanafunzi yupo sekondari lakini hata jina lake tu hajui kuandika, je mwanafunzi huyu atawezaje kujua masomo anayofundishwa?? Ukizingatia na hapa anafundishwa kwa kiingereza? Tofauti na lugha ya kiswahili aliyokua anafundishiwa shule ya msingi. Ataelewa masomo? Chemistry, Mathematics? Etc ni ngumu....
3: Idadi kubwa ya wanafunzi katika darasa moja ambayo inaathiri zoezi la ufundishaji...darasa moja lina wanafunzi 100+ na kama ambavyo inasisitizwa katika "competence based curriculum" ushiriki wa wanafunzi especially groups discussion. Kwa idadi hii group discussion ni haiwezekani kwa sababu ya wingi wa wanafunzi, hata nafasi yenyewe ya kukaa groups hakuna kwani hata ukaaji wao ni kubanana sana.
4: Idadi kubwa inayofanya idadi ya mikondo kuwa mingi kiasi kushindwa kumaliza syllabus kwa wakati. Kuna shule zina mikondo mitatu tu au ikizidi ni minne A,B,C....katika shule za kata hali ni tofauti mikondo ni A hadi G au H. Mikondo 7 au 8 ngumu hata mwalimu kumaliza syllabus kwa wakati.
Nini kifanyike/ Maboresho
1: Katika hizi shule yaanzishwe masomo ya ufundi ambayo yatawasaidia kwa kiasi kikubwa.
Kama nilivoandika hapo juu kuna tatizo la wanafunzi kufika sekondari lakini hawajui kusoma na kuandika, kukiwa na masomo ya ufundi itakua ni msaada kwao tofauti na sasa wanavofundishwa vitu vizito vizito ambavyo kiuhalisia ni kanyaga twende tu ili amalize miaka yake minne aondoke na division zero au four ya mwisho ambayo bado huyu mwanafunzi hajasaidika.
Kuwe na mikondo miwili au mitatu kwa hao walau cream watakaokua wanajifunza masomo kama kawaida. Na mikondo mingine wajifunze masomo ya ufundi mfano. Welding, ushonaji wa nguo kwa kutumia cherehani, utengenezaji wa viatu, wafundishwe mapambo, urembo, mapishi, muziki, ufugaji n.k n.k huku wakisoma masomo basic machache kama vile English, Kiswahili n.k
Kwa miaka minne atakayojifunza ufundi ni bora sana kuliko kukaa miaka minne akisoma vitu ambavyo hata havielewi.
Nawasilisha.