SoC04 Tanzania tuitakayo: Kliniki mwendo (mobile clinic): Suluhisho ya vifo vya mama wajawazito, watoto, makundi maalum sehemu za pembeni na vijijini nchini

Tanzania Tuitakayo competition threads

KISHOMBO

JF-Expert Member
Jul 19, 2012
206
38
Kliniki mwendo (mobile clinic): Suluhisho ya vifo vya mama wajawazito, watoto,makundi maalum sehemu za pembeni na vijijini nchini

Utangulizi

WAKATI nchi nyingi duniani zikiendelea na mkakati wa kuboresha sekta ya afya ili kufikia agenda ya 2030 Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) lengo 3, kuna wasiwasi kwa lengo hili kufikiwa kutokana na uwekezaji usiyoridhisha katika sekta ya afya na serikali yetu

Lengo la 3 inalenga kuzuia mateso yasiyo ya lazima kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika na vifo vya mapema kwa kuzingatia shabaha kuu zinazoimarisha afya ya idadi ya watu kwa ujumla nchini. Katika malengo haya maeneo yenye changamoto kubwa ya magonjwa na makundi ya kimasikini ndiyo yamepewa kipaumbele. Tanzania tuko kwenye kundi hili la kipaumbele

Lengo la 3 pia linalenga kuhakikisha maisha ya afya na kukuza ustawi kwa wote, katika umri wote. Afya na ustawi ni muhimu katika kila hatua ya maisha ya mtu, kuanzia mwanzo. Lengo hili linashughulikia vipaumbele vyote vikuu vya afya: afya ya uzazi, uzazi, mtoto mchanga, afya ya mtoto na vijana; magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza; chanjo ya afya kwa wote; na upatikanaji wa wote wa dawa na chanjo salama, bora, bora na zinazomudu bei nafuu.

Nchini Tanzania pamoja na juhudi mbalimbali zinaofanywa na serikali bado kuna changamoto kubwa sana katika kutoa huduma za afya. Bado tuna vifo vingi visivyo vya lazima vya mama wajawazito, watoto na wasichana katika sehemu mbalimbali nchini

Miundombinu-ya afya na utoaji huduma iikiwemo hupatikanaji wa madawa bado ni changamoto kubwa sana hasa maeneo ya pembezoni mwa nchi. Kutokana na jiografia ya nchi kuna maeneo mengi hakuna hospitali wala vituo vya afya suala ambalo linakuwa changamoto kubwa katika ustawi wa jamii zetu

Changamoto mbalimbali ambazo taifa letu linakabiliwa nalo ni kuwepo kwa bajeti finyu, ubunifu katika kutoa huduma za afya, kukosekana kwa ushirikishwaji wenye tija kwa sekta binafsi kuhusu afya, kukosekana kwa mifumo ya kisekta inayoshirikiana kwa pamoja n.k

Kwa mfano maeneo mengi ya vijini na pembezoni mwa nchi hakuna umeme, maji, huduma za mawasiliano na barabara. Kukosekana kwa huduma hizi za kijamii kunapelekea wananchi kukosa huduma ya afya na kukimbilia kwa waganga wa kienyeji na kutumia dawa za kienyeji ambazo nyingine si salama kwa usalama wa binadamu

Pia katika maeneo mengine hasa maeneo ya wafugaji mpangilio wa maboma (nyumba) zimetawanyika sana jambo ambalo linaletea changamoto namna ya kuhudumia maeneo haya. Changamoto kubwa ni umbali wa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kutafuta kituo cha afya. Katika maeneo haya bado changamoto ya barabara ni kubwa muno hivyo kunapelekea wananchi wa maeneo haya kukosa huduma ya matibabu ya dharula

Madhara-Kukosekana kwa miundombinu muhimu ya afya katika maeneo haya kunapelekea kuendelea kuongezeka kwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano, vifo vya wajawazito,vitendo vya ukeketaji, kuendelea kuongeza kwa imani za kishirikina, magonjwa ya ngono, lishe duni kukotokana na kukosekana kwa elimu ya lishe, na pia ni kumnyima haki mwananchi kupata haki yake ya kimsingi ya afya.

Nini kifanyike

Katika kuhakikisha tunafikia lengo 3 la SDGs, serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi wanahitaki kuja na ubunifu wa kupeleka Kliniki mwendo nyingi hasa maeneo ya vijijini kama jambo la haraka huku juhudi nyingine za ujenzi wa hospitali, zahanati na vituo vya afya ukiendelea

Kliniki mwendo hizi zitakuwa na wakunga, madaktari, wauguzi, watu wa ustawi wa jamii ambazo zinaweza kuwa zinatembelea maeneo mbalimbali hasa magulio, minada, mashuleni n.k kwa kutoa huduma ya afya ikiwemo kufanya vipimo vya mimba mashule, kipimo cha virusi vya HPV, chanjo za polio,ukimwi na kutoa elimu ya ukeketaji kwa maeneo yenye changamoto hiyo, kufanya tohara kwa watoto wa kiume, pia zitatumika kama jukwaa la kutoa elimu kuhusu afya na lishe na elimu kuhusu mila potofu kuhusu magonjwa kwenye jamii. Pia kwa kuwa Kliniki mwendo hizi ni magari kama malori makubwa au mabasi yenye nguvu, yatakuwa yanavuta matenki ya maji yenye matairi kwa ajili ya huduma ya maji kwenye kliniki hizo

Aidha kwa kutumia kliniki mwendo hizi kunatoa fursa kwa sekta bianfsi kushirikiana na serikali katika kutoa hudma za afya. Wawekezaji katika sekta ya afya kutoka sekta binafsi watanufaika pia kwa kuleta magari na serikali inaweza kutoa huduma ya nguvu kazi ya wataalamu. Pia Kliniki hizi pia zitaongeza wigo wa ajira kwa kuongeza idadi ya kada nyingine ya madereva. Pia zitasaidia sana katika kutoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) ambao wanatembea mwendo mrefu kutafuta huduma za afya

Kwa nyongeza, ni muhimu pia kwa wadau na wahisani wa kimataifa na taasisi zake wakati wanapofikiria kuleta ruzuku kwenye sekta ya afya kupitia serikali, pamoja na mambo mengine wafikirie kuleta kliniki mwendo zaidi kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwenye maeneo yaa pembezoni hasa vijijini kwenye jamii za kimasikini

Mwandishi

Deogratias Kishombo


Picha kwa hisani ya mtandao wa Children's Health Fund
1714725423324.png
 
Mwandishi

Deogratias Kishombo


1714725423324.png
Nimekapenda haka, kinaweza hata kuwa mobile mgahawa, mobile pharmacy, mobile game centre, mobile supermarket nzuri sana.


Kliniki mwendo hizi zitakuwa na wakunga, madaktari, wauguzi, watu wa ustawi wa jamii ambazo zinaweza kuwa zinatembelea maeneo mbalimbali hasa magulio, minada n.k mashule kwa kutoa huduma ya afya ikiwemo kufanya vipimo vya mimba mashule, kipimo cha virusi vya HPV, chanjo za polio,ukimwi na kutoa elimu ya ukeketaji kwa maeneo yenye changamoto hiyo, kufanya tohara kwa watoto wa kiume, pia zitatumika kama jukwaa la kutoa elimu kuhusu afya na lishe na elimu kuhusu mila potofu kuhusu magonjwa kwenye jamii.
Kama ulivyoeleza kliniki hizi zinafaa kwa zile huduma za kuonana mara moja moja tu mfano upimaji 'screening'.

Au kuna utaratibu upi mleta mada unaweza kupendekeza kwa watu kuhudhuria kliniki labda ya uzazi, moyo nk.

Hata hivyo haikatai walio katika kliniki mwendo wanaweza kuwarufaa wateja kuanza kuhudhuria kliniki katika vituo vyao vya karibu.
 
Back
Top Bottom