mwandende
JF-Expert Member
- Feb 16, 2017
- 10,844
- 20,524
Habari wakuu,
Mimi nina eneo langu kibaha ,maeneo ya serikali ya mtaa viziwaziwa shuleni,, Ukubwa wa eneo ni nusu hekta..
Shida niliyonayo ni kwamba ,,nimekuta TANESCO KIBAHA wamepitisha wire za umeme shambani kwangu ili kumpatia jirani nafasi ya kujenga eneo lake bila kunishirikisha wala kunijulisha suala hili..
Ipo hivi
Kuna jirani alikuwa anajenga kwenye eneo lake chini ya wire za umeme,, alikuwa na eneo dogo sana, wire wa umeme wa TANESCO ulikuwa unapita juu ya bati lake huyo jirani..
Baada ya kusikia nimesafiri wakaongea na VUSHOKA WA TANESCO wakaja usiku wakahamisha nguzo na kusogeza shambani kwangu na kuipitisha kati kati ya eneo langu bila kunishirikisha.
Walichofanya TANESCO ni uhuni au kuna harufu ya rushwa kwa jambo hili,, itawezekana vp kuhamisha nguzo kuweka kwa mtu mwingiine ili kumpatia nafasi ya mwingiine kufanya ujenzi?
Mbaya Zaidi ni kwamba, kiwanja changu kimefinywa kwa mbele na nyuma kote wamepitisha nguzo na wire za umeme, TANESCO wameniweka mazingira magumu ya kufanya ujenzi kwenye eneo langu..
Je, ni halali TANESCO kuhamisha nguzo ya umeme ili kupitisha kwenye eneo la mtu bila kumshirikisha mwingiine?
Mwenye kuelewa nini cha kufanya ili TANESCO waondowe nguzo tafadhali.
Pia soma:KERO - Waziri Biteko, kwanini nguzo moja ya umeme ilipiwe Tsh 515,000/ wakati ni mali ya shirika? Huu unyanyasaji mpaka lini?