mwangalingimungu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 1,301
- 733
Nashukuru kunielewesha kwamba mnajifunza kutoka kwa marehemu!Yanga FC wana ' Uchawi ' wa Kipumbavu sana Mkuu yaani juzi ile bila juhudi za ' Kiganga ' ambazo zilifanywa mule ' Chumbani ' na yule Mganga wao Mkuu wa Bagamoyo almaarufu ' Babu Bingwa ' Simon Msuva leo angeshakuwa ' Marehemu '.
Wenzao Simba SC baada ya kujifunza kutoka kwa Marehemu Tindwa tuliachana kabisa na huo ' Uchawi ' na alipokuja Merehemu Mzee Bamchawi alituletea ' Uchawi ' mpya ambao kwa heshima na taadhima ya Klabu yangu sitouweka hadharani hapa ila ni Uchawi ambao haumdhuru Mchezaji na ni wa Kistaarabu sana.
Yanga FC badilikeni na aina hii ya Uchawi wenu na nawaomba sasa Wachezaji wote wa Yanga FC wakiwa wanapewa tu Jezi zao za Kuvaa katika mechi basi wawe Kwanza wanazikagua katika pindo za ama Jezi au Bukta zao kwani mara nyingi ' Hirizi ' ndiyo hushonewa huko. Na hili linafanyika baada ya kuonekana kuwa karibia Wachezaji wote wa Yanga FC ukiondoa tu Mchezaji Mpenda ' Ushirikina ' Yanga FC nzima Nahodha Nadir Haroub Cannavaro na mwenzake Juma Abdul hawapendi ' ushirikina ' hivyo hulazimika kuwashoneshea ' Hirizi ' kwakuwa kuna baadhi yao huwa na ' Nyota ' kali ya ushindi kwa Timu.
Bora hata ya Mshambuliaji wao Obren Chirwa yeye kaamua tu rasmi kubeba ' Hirizi ' yake ambayo mara nyingi huitumia katika kila mechi ya huiweka ' Kiganjani ' kisha anaifungia na ' Bandage ' ili ' kutuzuga ' kama vile ana matatizo ya mkono ILA ' Watoto ' wa mjini na tunaolijua Soka la Bongo mwanzo mwisho tunajua nini anachokifanya.
Pole sana mdogo wangu Simon H. Msuva siku nyingine uwe unaikagua vizuri ' Jezi ' yako ili ukikuta tu ' Hirizi ' imeshoneshewa ' ugome ' kucheza vinginevyo Yanga FC ' wataakua ' kwa ' Ushirikina ' wao waliouzoea.