Tahadhari na ushauri wa ni msaada gani ninaoweza kupata kwa case ya muamala uliofanyika kama malipo ya deni

EP MEDICS COSMETICS STORE

JF-Expert Member
Oct 18, 2015
2,772
4,400
Wasalaamu wanajukwaaa.

Jana nimekutana na ujanja ujanja ambao kwangu ni mpya kabisa, sijui ninaweza kuita utapeli. Ila ninachoweza kusema ni udhaifu mkubwa sana wa mtandao wa vodacom vodacom upande wa miamala.

Ni ivi kuna mtu nilikuwa ninamdai kiasi kadhaa cha pesa, sasa tukapelekana mpaka polisi baada ya vuta nikuvute na kubanwa akakubali kunilipa kiasi cha tsh 900,000/= kwa njia ya kunitumia mpesa, akafanya hivyo akaomba kwa mgu mwingine kisha nikatumiwa 900k na meseji ya mumala ukasoma kwenye simu yangu, baada ya muamala kusoma nikatulia, kumbe baada ya dk 4 alireverse transaction na kuomba muamala urejeshwe na ikafanywa ivyo kweli (bila mimi kutumiwa text yeyote na voda ya kwamba muamala umesitishwa na kurudishwa ulikotoka).

Nilikuja kugundua baada ya kutaka kutoa pesa na kisha kuambiwa huna salio la kutosha ndipo kucheki salio nikakuta pesa ilirudishwa ilikotoka na muamala huko bado hewani kuthibitishwa ili kurudi ulikotoka.

Nimepambana sana kuwa huo muamala ni haki yangu hivyo usirudishwe uliko toka ila wapi mwisho wa siku voda wameurudisha.

Udhaifu wa mtandao wa voda ninaouona upande huu, ni mnamruhusu mtu vipi kuweza kureverse transaction kirahisirahisi namna hiyo ?, ni mnarudisha pesa vipi kirahisi namna hiyo hata baada ya muhusika kuwatafuta kuwaeleza hali halisi na kuwaambia kuwa pesa iliowekwa ilikuwa ni haki yake.

Na udhaifu mkubwa zaidi ni kwanini hamtumi meseji muda uleule wa muamala unapofanyiwa reverse, badala yake mnakuja kutuma meseji baadae sana muamala ukiwa umeishathibitishwa kurudi?

Mwisho naomba kujua je, iwapo nikienda polisi na ushahidi wa meseji za reverse transaction ninaweza kupata msaada? Angalizo alienitumia pesa, aliyenifanyia muhamala wa 900k sio yule ninaemdai ila yeye aliomba kwa mtu mwingine ndio akanitumia hiyo pesa.
 
Bado unamdai jamaa, maaana , fuata sheria , waambie ule muamala alionitumia umerudishwa , na mm sikupata pesa, , siku nyingine hamisha haraka au toa kwa wakala kabla hamjaachana,
 
Wasalaamu wanajukwaaa.

Jana nimekutana na ujanja ujanja ambao kwangu ni mpya kabisa, sijui ninaweza kuita utapeli. Ila ninachoweza kusema ni udhaifu mkubwa sana wa mtandao wa vodacom vodacom upande wa miamala.

Ni ivi kuna mtu nilikuwa ninamdai kiasi kadhaa cha pesa, sasa tukapelekana mpaka polisi baada ya vuta nikuvute na kubanwa akakubali kunilipa kiasi cha tsh 900,000/= kwa njia ya kunitumia mpesa, akafanya hivyo akaomba kwa mgu mwingine kisha nikatumiwa 900k na meseji ya mumala ukasoma kwenye simu yangu, baada ya muamala kusoma nikatulia, kumbe baada ya dk 4 alireverse transaction na kuomba muamala urejeshwe na ikafanywa ivyo kweli (bila mimi kutumiwa text yeyote na voda ya kwamba muamala umesitishwa na kurudishwa ulikotoka).

Nilikuja kugundua baada ya kutaka kutoa pesa na kisha kuambiwa huna salio la kutosha ndipo kucheki salio nikakuta pesa ilirudishwa ilikotoka na muamala huko bado hewani kuthibitishwa ili kurudi ulikotoka.

Nimepambana sana kuwa huo muamala ni haki yangu hivyo usirudishwe uliko toka ila wapi mwisho wa siku voda wameurudisha.

Udhaifu wa mtandao wa voda ninaouona upande huu, ni mnamruhusu mtu vipi kuweza kureverse transaction kirahisirahisi namna hiyo ?, ni mnarudisha pesa vipi kirahisi namna hiyo hata baada ya muhusika kuwatafuta kuwaeleza hali halisi na kuwaambia kuwa pesa iliowekwa ilikuwa ni haki yake.

Na udhaifu mkubwa zaidi ni kwanini hamtumi meseji muda uleule wa muamala unapofanyiwa reverse, badala yake mnakuja kutuma meseji baadae sana muamala ukiwa umeishathibitishwa kurudi?

Mwisho naomba kujua je, iwapo nikienda polisi na ushahidi wa meseji za reverse transaction ninaweza kupata msaada? Angalizo alienitumia pesa, aliyenifanyia muhamala wa 900k sio yule ninaemdai ila yeye aliomba kwa mtu mwingine ndio akanitumia hiyo pesa.

Huo ushahidi wa reverse trans ni ushahidi kwmba ujalipwa hela, sasa sijui swali ni nini? Na kama ujalipwa hela na ni halali yako Police watakusadia.
 
Back
Top Bottom