Tafakuri ya maisha: Ungefanya nini ikiwa umetambua bado miezi sita kuishi?

Kama ni mimi nitafanya yafuatayo, nitawatafuta wote niliowakosea na kuwataka radhi kama wangali hai, nitatubu dhambi zangu zote hadharani na kusamehe wote ili nipate amani ya moyo. Madeni kama ninayo nitalipa kwa kadri ya uwezo wangu. Kama nina watoto nitawafundisha hekima ili waishi vyema mara baada ya mimi kwenda kusiko julikana.

Nitamwomba mola anisamehe makosa yangu kama ambavyo mimi nimesha tubu na kusamehe. Baada ya hapo nitaitafuta njia ya kweli na kufanya kazi kwa bidii bila kusahau ibada.

Mkuu mtu anaweza kukuuliza kwa nini usifanye hayo sasa mpaka usubiri ukiwa na uhakika wa kufa?
 
Binafsi ntafanya kazi za kujitolea katika jamii, pili nitaandika historia yote ya maisha yangu kwa faida ya watoto wangu na mwisho ntajipereka kwa Wahindi wanao choma moto nipate utaratibu, ili nikifa nichomwe moto.
 
Ntafanya jitihada zote nitembee na watu wafuatao:
1.ZARI
2.WEMA
3.KAJALA
4.PENY
5.JOKATE
6.UWOYA
7.WOLPER
8.SNURA
9.SHILOLE
10.LINAH
11.RUBY
12.VANESSA
13.AUNT EZEKIEL
14.MADDAM RITA
15.SALAMA JABIR
16.ASHA
17.REHEMA
18.MWAJUMA
19.ZUHURA
20.SUZY
21.NANCY
22.MARIAM
23.SASHA
24.HAPPY.
 
Me hata kabla sijaambiwa hapa nilipo nimeshajinunulia sanda yangu iko kabatini nishawekeza na eneo la kuzikiwa karibu na ndugu zangu.ikitokea nimefia ktk mazingira tofauti basi ila nilishajiandaa!sababu uwezekano wa kufa ni mkubwa kuliko kuishi
 
Back
Top Bottom