Tafakuri ya maisha: Ungefanya nini ikiwa umetambua bado miezi sita kuishi?

Kama ni mimi nitafanya yafuatayo, nitawatafuta wote niliowakosea na kuwataka radhi kama wangali hai, nitatubu dhambi zangu zote hadharani na kusamehe wote ili nipate amani ya moyo. Madeni kama ninayo nitalipa kwa kadri ya uwezo wangu. Kama nina watoto nitawafundisha hekima ili waishi vyema mara baada ya mimi kwenda kusiko julikana.

Nitamwomba mola anisamehe makosa yangu kama ambavyo mimi nimesha tubu na kusamehe. Baada ya hapo nitaitafuta njia ya kweli na kufanya kazi kwa bidii bila kusahau ibada.

Mkuu unangoja nn usitekeleze hayo sasa?
 
NNingetumia huo kumrudia Mungu wangu nakutubu dhambi zangu ili nikamuone Yesu.
 
Back
Top Bottom