Mtasikia kuhusu vita vinanavyopiganwa na pia matetesi ya kuwapo vita vingine. Lakini msiogope. Mambo haya lazima yatokee na mwisho wenyewe hautafuata palepale. Mataifa yatapigana na mataifa mengine. Falme zitapigana na falme zingine. Utakuwepo wakati wa njaa ambapo watu watakosa chakula. Na kutakuwa matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali. Mambo haya ni mwanzo wa matatizo, kama uchungu wa kwanza mwanamke anapozaa.Lakini fahamu jambo hili: kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio na utakatifu; wasio na ubinadamu, wasiopenda kusuluhishwa, wachonganishi, walafi, wakatili, wasiopenda mema; wasaliti, wasiojali kitu, waliojaa majivuno, wapendao anasa badala ya kumpenda Mungu. Hao ni watu ambao kwa nje wataonekana kuwa wana dini, huku wakikana nguvu ya imani yao. Jiepushe na watu wa jinsi hiyo.
Maana miongoni mwao wamo wale waendao katika nyumba za watu na kuwateka wanawake dhaifu waliolemewa na dhambi na kuyumbishwa na tamaa za kila namna. Wao humsikiliza kila mtu lakini hawawezi kutambua kweli. Kama vile Yane na Yambre walivyopingana na Musa, kadhalika watu hawa nao wanapingana na ile kweli. Ni watu wenye akili potofu, wenye imani ya bandia. Lakini hawa tafika mbali, kwa sababu ujinga wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri ujinga wa hao watu wawili.