Torque vs HP
JF-Expert Member
- Jan 7, 2021
- 1,769
- 5,084
Unamuongelea mkapa aliyekua mpigaji na wale makaburu wa NBC au unamuongelea yupi huyo?Ngojea nikwambie kitu (sina hakika na umri wako ); enzi za Mkapa, tuliwahi kufanya kitu cha namna hi, tuliiweka Tanesco chini ya kampuni moja ya Africa kusini inaitwa Net group solution, managing director, director of finance and other senior officials wa Tanesco walikua Wazungu; je hakukua na kukatika kwa umeme? Tuweni wa kweli, tukiondoa siasa na kuweka mbinyo kwa watendaji wa mashirika yote ya umma, mambo yanaweza kwenda. Kwa umri wangu hu, tokea mwaka 1992 tuliaminishwa kwamba endapo mvua zitakua chache mwaka hu then mgao wa umeme ni la kawaida, Mwendazake kaingia madarakani (hapa tuwe tu wakweli, either unampenda mhe Magufuli au unamchukia ) umeme ulikua wa uhakika, before 2015 nilikua na generetor pamoja na mfumo mzima wa Televison kua wa solor; generator sielewi hata lilipotea vipi cause vitu hivyo vimekua sio muhimu cause mwendazake kwenye hili la umeme alifanya kazi na kazi imeonekana, kwenye maduka ya kuuzia simu, ilikua na power bank zipo before 2015 but tembelea maduka mengi sasa hivi, is either hakuna kabisa hizo power bank au zipo chache sana, why? Umeme umekua wa uhakika, hata ukikatika hauchukui muda mrefu umerudi. Hakuna zmungu pale Tanesco but enzi akiwepo mzungu mgao ulikuwepo na kukatika katika kulikuwepo pia.