Symbion kuishitaki TANESCO Mahakamani nchini Ufaransa

Hata waende mahakama ya mbingu mtuachie nchi yetu hatuhitaji misaada yenu wala mikataba yenu mbuzi. Fisi kabisa symbion hahahahhhh Magu anabana huku na kule mnashindwa namna

USILAUMU SYMBION. SUALA HAPA NIKWANINI TANESCO WALIENDA KUSAINI MKTABA DEC 2015 WAKATI WAKUJUA SERIKALI NA MUELEKEO WA MH RAIS NIKUTOTAKA HABARI YA CAPACITY CHARGES.
 
Ukiangalia mtiririko wa matukio wakati wa mchakato wa kusaini huu mkataba utagundua kulikuwa na ujanja ujanja wa kifisadi. Mkataba ulisainiwa Desemba 10, 2015 - siku ambayo baraza jipya la mawaziri lilitangazwa. Ina maana mkataba ulifikiwa "fasta fasta" bila kuwepo kwa waziri wa nishati ambaye ndiye msimamizi mkuu wa masuala ya kisera. Lakini la kushangaza ni kwamba huu mkataba ulipata baraka zote za EWURA na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG). Je, inafikirika kweli AG aridhie mkataba mkubwa kama huu bila kushauriana na rais? Kwa nini mkataba ufikiwe katika mazingira ambayo waziri mwenye dhamana ya kisera hayupo? Kulikuwa na haraka gani? Kuna mchezo mchafu hapa!
 
Kwenye maslahi ya taifa unapoingiza siasa kama vile TANESCO ikilipishwa fidia wewe hautaathirika ndipo ninapopata mashaka na uwezo wako wa kufikiri, hii vita ni mmarekani anaiendesha kuanzia MCC huu ni muendelezo wake, maghu awe makini Sana kwa kuwa jk aliingia mikataba mingi mibovu inayoifanya tz leo iwe mtumwa wa mabepari
mikataba na mabeberu ilianza zamani sana tangu Mikataba ya Seyyid Sai na wazunu na Carl Peters na machifu wa kiafrika.
Okay tunaambiwa kina Chief mangungo hawakujua kizungu. Kule Ethiopia Waitaliano waliandika mikataba kwa Kiamhran na Kitaliano lakini content tofauti.
Lakini hivi sasa tunajua kizungu na tunajua penye hila sasa tutajiteteaje maana hatukulazimishwa kama wakati ule?
 
Kabla Symbion hawajaishitaki TANESCO, wenyewe kwanza inapaswa washitakiwe. Symbion iliwakopa suppliers wengi katika kutekeleza miradi yake ya umeme vijijini na inadaiwa mabilioni ya pesa kwa kipindi kirefu but haijawalipa mpaka leo na wakati MCC waliwalipa Syimbion pesa zote za mradi. Wao badala ya kulipa suppliers wao wakabeba pesa kwenda kufanya mtaji kwenye miradi yao mingine. Hawa jamaa sio waaminifu kabisa. Wacha tu huo mkataba uvunjwe...
 
Ahsante sana Mkuu umeona mbali sana.

CC: Richard

Mikataba inaingia serikali(wizara) kwa niaba ya TANESCO kisha mambo yakiharibika TANESCO ndio wanabebeshwa lawama. Serikali inaishinikiza TANESCO iingie kwenye mikataba, mambo yakienda kombo analaumiwa TANESCO.

TANESCO ndio walimpa mwaliko Mama Clinton aje kuzindua mradi na mitambo ya symbion?, TANESCO ndio walimualika Obama aje bongo? TANESCO inatolewa kafara tu ila wanaoliharibu shirika ni wanasiasa.
 
Mkuu kumbuka fisadi Mkapa aliwahi hata kuwaingiza makaburu kama management ya Tanesco tena kwa mtutu wa bunduki.

Matatizo yote ya TANESCO chanzo ni mafisadi Mkapa na Kikwete na mikataba chungu nzima ya kifisadi waliyoingia hata pale walipotahadharishwa na wataalamu wa Tanesco. Ukitaka kupata majina ya hawa sidhani kama itakuwa kazi kubwa sana.

U.S. firm seeks $561 million from Tanzania in power supply dispute

Chief ,

Unakumbuka Tanesco ilikuwa chini ya nani kipindi cha Mkapa na Kikwete?

Halafu habari yenyewe ni ya May 2016
 
Back
Top Bottom