Hbr wana JF,
Mwaka jana nilipata binti mmoja ambae tulifahamiana kwa muda kidogo tukaanza mahusiano. Nilimpenda sana, nikajitahidi kumtimizia kila analohitaji. Nilijifunza kwenye mahusiano yangu ya awali, nikasema huyu nifanye tofauti sasa na mimi niwe na familia. Mwanzo mapenzi yalikua motomoto, tukaanza kupanga mipango ya ndoa kabisa huu mwaka tuwe mume na mke.
Baada ya miezi kadhaa, akaanza kubadilika. Nakumbuka alianza kununa tukiwa vacation Zanzibar. Akawa kama ana moods hivi, ukimuuliza kuna changamoto gani hasemi. Nikaona mambo ya kike labda nitulie. Basi kuanzia hapo akawa kama anani dharau na hanijali tena kama mwanzo. Nilikua naumia ila nikawa navumilia. Lakini kwa tabia zile alizoanzisha ikanilazimisha baadhi ya mambo tulipanga kufanya - kama kwenda kujitambulisha kwao tusitishe kwanza maana sikua namuelewa, anasahau mpaka tarehe muhimu kwenye mahusiano yetu kitu ambacho sio cha kawaida. Baada ya muda nikaenda nje ya nchi kikazi, katika nchi ambayo tulikua tunapishana masaa na hapo ndio mapicha picha yakazidi akawa hapokei simu kabisa akidai yuko busy etc. Kwa muda wote niliokua nje ya nchi kama miezi miwili hatukuwahi kuongea kwenye simu, kila nikijaribu kumtafuta anasema yuko busy atanicheki lakini hafanyi hivyo. Basi nikaanza kufanya maamuzi magumu, nikaacha kumpa monthly allowance na kumnunulia zawadi kama nilivyokua nafanya mwanzo. Nilivyorudi nchini, bado nikamtafuta kujua tatizo ni nini na nakumbuka pamoja na tofauti tulizokua nazo bado nilitoka ulaya na zawadi kadhaa nimemchukulia nikampa. Kikao hakikuenda sawa, binti akaniambia hana feelings na mimi na nikitaka kuwasiliana nae lazima nifanye appointment au nitafute mwanamke mwingine wa kua nae. Aisee, kikao kiliishia hapo. To cut the story short, mahusiano yaliisha pia.
Hii ni case moja tu kati ya nyingi ambazo nimeshakumbana nazo. Katika miaka 10 iliyopita nishakua kwenye mahusiano mengi sana na yamekwama kwa sababu tofauti tofauti, ingawa hii ya juzi iliniuma maana nilijitahidi kufanya kila kitu inavyotakiwa na mhusika mwenyewe pia nilijua anajitambua maana at 31 ni mtu mzima sio mtoto mdogo ni mwanamke aliepitia mengi. Mwaka umeanza nimekata tamaa kama naweza kweli na mimi siku moja kupata mke, nikaanzisha familia na kua na watoto. Kila kitu ninacho - kazi nzuri, kipato kizuri yani ni mke tu ndio imekua changamoto. Kuna wakati najilaumu labda ningekua nakunywa pombe & mtu wa starehe huenda ingekua rahisi kwangu maana haya maisha ya kua busy na kazi muda wote nayo ni changamoto sikutani na watu ila ndio nafanyaje sasa na pesa naitaka pia.
Naomba ushauri wadau, nifanyeje?!
NB:
Niliwahi kuandika uzi humu wa kutafuta : A wife is needed