Sumaye: Tubadili utawala wa vitisho

Watu gani wa pwani waliomchangia hiyo pesa? acheni maigizo yenu na hii ndio inanifanya nichukie siasa na wanasiasa wa nchi hii kila kitu uwongo tu,
 
Vizuri lengo lako ni uraisi maana ulijaribu ccm ukaukosa
Hakiyako kujaribu na huko kama utaweza
Sio kudanganya uma eti unataka mabadiliko au kuiondoa ccm.
 
Ni Pwani hapo hapo (Bagamoyo) walijitokeza wachawi kumchangia Lowassa na kumfuata Dodoma eti agombee Urais. Naona tunguri inaendelea kwa ma PM waasi.
 
Hakuna mwenye hati miliki wa nchi hii,sumawe luwasa na masha hawakutegemea watakuwa ndani ya upinzani,wakati wao walikuwa wanawakandamiza wapinzani nakutumia lugha chafu nazarau kwahao wapinzani.leo wao ni sehemu ya upinzani.hi ni somo tosha kwa magufuli leo anawakandamiza wapinzani na demokrasia kesho ataibuka kiongozi mwngne atakuja nazake ref;malawi na zambia.mawaziri wa magufuli pateni somo kwa luwasa na sumawe,tendeni haki lindeni katiba mshaurini mkuu alete katiba ya warioba
 
Haha,sumaye alizaliwa,akakua akajiunga ccm na atazeeka atakufa na ataiacha ccm ikiwa,madarakani aache ndoto alinacha na abunuwasi
 
Maganga tayari, Sumaye tayari, Lowassa tayari ndiyo mwenye chama, wote hawa wamekijua chama chini ya mwaka mmoja sasa. Je Chadema bado ni ileile? Hii ni Chadema CCM tena CCM mbovu na ya hovyo kuliko tuliyonayo.
 
Akizungumza na wandishi wa habari Kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mwenyeketi wa Dar es Salam, , Kijijini kwake Tondoroni, Kiluvya Pwani, Sumaye, amesema kuwa ni wakati sasa wa kukipeleka chama hicho hadi katika ngazi za vitongiji ambako ndiko wanakoringia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema ni vema watawala wa kiafrika wakawaacha wananchi kutumia demokrasia yao katika kujiamulia kuchagua kiongozi wanayefikiria atatekeleza malengo yao wanayoyatarajia.

“Ndoto niliyo nayo ni ile ile iliyonitoa CCM, katika demokrasia kwa mfano ukienda Marekani huwezi kuona wamarekani wamekiacha CHAMA kimoja kikitawala miaka 30 hadi 40 kwaza hata miaka nane ni bahati sana kwa sababu chama kikitawala miaka nane huwa ni bahati kwasababu wanaju kikishatawala miaka hiyo kitakuwa kimepata fursa ya kutekeleza malengo yake,”amesema Semaye.

Amesema tatizo lilipo Tanzani ni chama kilichopo madarakani kutokubali kuviona vyama vingine vinainua pua ifike pali kwa chama tawala kukubali kushindwa pindi wananchi wanapoamua.

“Kwa kawaida chama chochote kikitawala muda mrefu hakiwezi kufanya vizuri na hiyo ni sawa na anayepiga maji wakati hajui kuogelea hali inayowanyima wananchi fursa ya maendeleo,”alisema Sumaye.

Sumaye, amesema ndoto yake nikuona Chadema ina wafikisha Watanzania kule wanakotaka na kuamini kwamba sasa demokrasia imechukua mkondo wke.

Akizungumzia uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Sumaye, amesema anawashukuru wanachama hao kwa kuonesha imani kwake na kuahidi kwamba yuko tayari kufanya kazi ya kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Amesema, ingawa ili awe mwenyekiti ni lazima achaguliwe lakini aliwaahidi wanachama hao kwamba Chadema inahitaji kuongoza dola kwa hiyo kazu kubwa iliyoko ni wanachama wa chama hicho kujipanga kuanzia sasa ikiwemo kujiepusha na migogoro isiyokuwa ya lazima.

Amesema haata inapotokea ni vema zikatumika busara katika kuipatia ufumbuzi ambayo matokeo yake ni kuwa na chama imara.

“Nawashukuru kwa kunichangia sh. 100000 ya kunichukulua fomu najuamefanya hivi kwa upendo wenu wala siyo kwa ubaya nami nasema nimekubali ombi lenu Bali naomba mnipigie kura msiishie hapa,”amesema Sumaye.

Naye mwanasheria wake Aidan Kitare amesema kwa vile kesho ndiyo siku ya mwisho atajitahidi pamoja na mgombea wake wanakamilisha utaratibu na kurusisha fomu hiyo kabla ya saa 6:00 mchana.

Mwita waitara mwenyekiti wa Dar es Salaam Kuu aliyekuwepo katika kumsindikiza kiongozi huyo, amesema wanachama hao waliyojitokeza kumchukulia fomu Sumaye walifanya hivyo wakiamini kwamba atakisaidia chama kwa vile anauzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi katika utumishi wa Umma.

SOURCE:Sumaye: Tubadili utawala wa vitisho
Lol kutoka waziri mkuu hadi mwenyekiti wa chama mkoa? Kweli huu uroho wa madaraka wa mwendo kasi
 
Chadema endeleeni kuzika chama .
Hivi mwenyekiti wa chadema nini kimemkwaza.
Mbona kimya kimezidi? Hata salamu tu hamna.
 
mara hii kashasahau kila kitu alichofanya alipokua PM. haridhiki tu kufukia nafasi hiyo ya upm? anatafuta nini tena kwenye siasa? kama sio uchu wa madaraka huu ni nini. kuna watu hawaridhiki aisee hapa duniani.
 
Shukrani mzee mkapa tungejuwaje kama upo afsa ugavi,ila serikali ya vitisho tuombe radhi watu wa mwembe chai kauli yako imenikumbusha ulipowatuma polisi waingie na mabuti yao!
Najubaliana na wewe Sumaye, lakini si wewe huyohuyo uliyewaambia wafanyabiashara wa Moshi kwamba ukitaka mambo yako yakunyookee tundika bendera ya CCM nje ya duka lako?
 
Kifupi makapi hayataleta mabadiliko sumaye ni makapi
Ni bora zile njia za zamani kukuza wapya kama kina myika zito nawengine walioanza na upinzani mojakwamoja hata kama miaka 10 tena kuliko hawa mwisho wake ni msuguano tu
 
Shukrani mzee mkapa tungejuwaje kama upo afsa ugavi,ila serikali ya vitisho tuombe radhi watu wa mwembe chai kauli yako imenikumbusha ulipowatuma polisi waingie na mabuti yao!
wewe ulitarajia wakati polisi FFU wanapopambana na magaidi wangevua butu kutawadha na kuingia msikitini??
 
Akubali kugombea Uenyekiti CHADEMA kanda ya Pwani.

Aomba wajumbe kumpigia kura.

FREDRICK Sumaye, Waziri Mkuu mstaafu amesema anatamani kuona ndoto yake inatimia kwa watanzania kubadili uongozi bila hofu na vitisho vinavyosababishwa na watawala kwa kutumia nguvu ya dola, anaandika Mwandishi Maalum.Sumaye ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Cha cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameyasema hayo kutoka na historia za baadhi ya viongozi wa Bara la Afrika pindi wanapoingia madarakani kutopenda hata kuwaona wengine wakiinua pua.

Akizungumza na wandishi wa habari Kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mwenyeketi wa Dar es Salam,Kijijini kwake Tondoroni, Kiluvya Pwani, Sumaye, amesema kuwa ni wakati sasa wa kukipeleka chama hicho hadi katika ngazi za vitongiji ambako ndiko wanakoringia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema ni vema watawala wa kiafrika wakawaacha wananchi kutumia demokrasia yao katika kujiamulia kuchagua kiongozi wanayefikiria atatekeleza malengo yao wanayoyatarajia.

“Ndoto niliyo nayo ni ile ile iliyonitoa CCM, katika demokrasia kwa mfano ukienda Marekani huwezi kuona wamarekani wamekiacha chama kimoja kikitawala miaka 30 hadi 40 kwaza hata miaka nane ni bahati sana kwa sababu chama kikitawala miaka nane huwa ni bahati kwasababu wanaju kikishatawala miaka hiyo kitakuwa kimepata fursa ya kutekeleza malengo yake,”amesema Semaye.

Amesema tatizo lilipo Tanzania ni chama kilichopo madarakani kutokubali kuviona vyama vingine vinainua pua ifike pali kwa chama tawala kukubali kushindwa pindi wananchi wanapoamua.

“Kwa kawaida chama chochote kikitawala muda mrefu hakiwezi kufanya vizuri na hiyo ni sawa na anayepiga maji wakati hajui kuogelea hali inayowanyima wananchi fursa ya maendeleo,”alisema Sumaye.

Sumaye, amesema ndoto yake nikuona CHADEMA ina wafikisha watanzania kule wanakotaka na kuamini kwamba sasa demokrasia imechukua mkondo wke.Akizungumzia uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Sumaye, amesema anawashukuru wanachama hao kwa kuonesha imani kwake na kuahidi kwamba yuko tayari kufanya kazi ya kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Amesema, ingawa ili awe mwenyekiti ni lazima achaguliwe lakini aliwaahidi wanachama hao kwamba CHADEMA inahitaji kuongoza dola kwa hiyo kazu kubwa iliyoko ni wanachama wa chama hicho kujipanga kuanzia sasa ikiwemo kujiepusha na migogoro isiyokuwa ya lazima.

Amesema haata inapotokea ni vema zikatumika busara katika kuipatia ufumbuzi ambayo matokeo yake ni kuwa na chama imara.

“Nawashukuru kwa kunichangia sh. 100000 ya kunichukulua fomu najuamefanya hivi kwa upendo wenu wala siyo kwa ubaya nami nasema nimekubali ombi lenu Bali naomba mnipigie kura msiishie hapa,”amesema Sumaye.

Naye mwanasheria wake Aidan Kitare amesema kwa vile kesho ndiyo siku ya mwisho atajitahidi pamoja na mgombea wake wanakamilisha utaratibu na kurusisha fomu hiyo kabla ya saa 6:00 mchana.

Mwita waitara mwenyekiti wa Dar es Salaam Kuu aliyekuwepo katika kumsindikiza kiongozi huyo, amesema wanachama hao waliyojitokeza kumchukulia fomu Sumaye walifanya hivyo wakiamini kwamba atakisaidia chama kwa vile anauzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi katika utumishi wa Umma.
HIYO SERIKALI YA VITISHO ANAYOISEMA KAMA NI KWELI BASI MZEE SUMAYE AIDHA AMECHOKA KISIASA AU AMESAHAU KUWA SERIKALI HII NI MUENDELEZO WA SERIKALI ILE ILE AMBAYO YEYE NDIYE ALIYE KUWA WAZIRI MKUU WAKE NA KATIKA KIPINDI CHAKE WENGI TUNAKUMBUKA MATUKIO YA KISIASA YALIVYO SHUGHULIKIWA NA KUPITIA CHAMA HICHO HICHO ALIOMBA KUTEULIWA KUWA MGOMBEA WA URAIS. IWEJE LEO???? AU NDIYO HADITHI YA SUNGURA ALIYEKOSA ZABIBU NA KUZIITA MBICHI???? 'MTU MZIMA AKIVUKWA NGUO HUCHUTAMA'
 
Kwa Magufuli kila goti litapigwa.

Pia hamna jiwe litakalobaki bila kugeuzwa
 
Back
Top Bottom