Sumaye: Tubadili utawala wa vitisho

Kwani chadema kuna uchaguzi wa ndani au Sumaye katengenezewa tu uchochoro wa kupita
 
Nimesikia kwenye dondoo za magazeti hapa kisiwani kuwa Sumaye amesema kwamba ataiondoa CCM madarakani kabla hajafa. Amenifanya nimkumbuke mzee mmoja aliyeyasema maneno kama hayo kwamba CCM itakufa ndani ya mika mitatu, baada ya muda tukapata habari kwamba yule mzee kagongwa na gari na kufariki dunia. Mungu huwa ana mipango yake na yeye na sisi tuna ya kwetu!!!
 
Akizungumza na wandishi wa habari Kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mwenyeketi wa Dar es Salam, , Kijijini kwake Tondoroni, Kiluvya Pwani, Sumaye, amesema kuwa ni wakati sasa wa kukipeleka chama hicho hadi katika ngazi za vitongiji ambako ndiko wanakoringia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema ni vema watawala wa kiafrika wakawaacha wananchi kutumia demokrasia yao katika kujiamulia kuchagua kiongozi wanayefikiria atatekeleza malengo yao wanayoyatarajia.

“Ndoto niliyo nayo ni ile ile iliyonitoa CCM, katika demokrasia kwa mfano ukienda Marekani huwezi kuona wamarekani wamekiacha CHAMA kimoja kikitawala miaka 30 hadi 40 kwaza hata miaka nane ni bahati sana kwa sababu chama kikitawala miaka nane huwa ni bahati kwasababu wanaju kikishatawala miaka hiyo kitakuwa kimepata fursa ya kutekeleza malengo yake,”amesema Semaye.

Amesema tatizo lilipo Tanzani ni chama kilichopo madarakani kutokubali kuviona vyama vingine vinainua pua ifike pali kwa chama tawala kukubali kushindwa pindi wananchi wanapoamua.

“Kwa kawaida chama chochote kikitawala muda mrefu hakiwezi kufanya vizuri na hiyo ni sawa na anayepiga maji wakati hajui kuogelea hali inayowanyima wananchi fursa ya maendeleo,”alisema Sumaye.

Sumaye, amesema ndoto yake nikuona Chadema ina wafikisha Watanzania kule wanakotaka na kuamini kwamba sasa demokrasia imechukua mkondo wke.

Akizungumzia uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Sumaye, amesema anawashukuru wanachama hao kwa kuonesha imani kwake na kuahidi kwamba yuko tayari kufanya kazi ya kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Amesema, ingawa ili awe mwenyekiti ni lazima achaguliwe lakini aliwaahidi wanachama hao kwamba Chadema inahitaji kuongoza dola kwa hiyo kazu kubwa iliyoko ni wanachama wa chama hicho kujipanga kuanzia sasa ikiwemo kujiepusha na migogoro isiyokuwa ya lazima.

Amesema haata inapotokea ni vema zikatumika busara katika kuipatia ufumbuzi ambayo matokeo yake ni kuwa na chama imara.

“Nawashukuru kwa kunichangia sh. 100000 ya kunichukulua fomu najuamefanya hivi kwa upendo wenu wala siyo kwa ubaya nami nasema nimekubali ombi lenu Bali naomba mnipigie kura msiishie hapa,”amesema Sumaye.

Naye mwanasheria wake Aidan Kitare amesema kwa vile kesho ndiyo siku ya mwisho atajitahidi pamoja na mgombea wake wanakamilisha utaratibu na kurusisha fomu hiyo kabla ya saa 6:00 mchana.

Mwita waitara mwenyekiti wa Dar es Salaam Kuu aliyekuwepo katika kumsindikiza kiongozi huyo, amesema wanachama hao waliyojitokeza kumchukulia fomu Sumaye walifanya hivyo wakiamini kwamba atakisaidia chama kwa vile anauzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi katika utumishi wa Umma.

SOURCE:Sumaye: Tubadili utawala wa vitisho
Fredrick Tuluway Sumaye leo anaongea haya. angevuta kumbukumbu kidogo aina ya utawala alioufanya wakati akiwa PM ndani ya ccm. wale waislam kule mwembechai aliwafanya nini na alikuwa akisimamia wapi
 
Ila siasa dah.
Kutoka Pm hadi mwenyekiti wa mkoa?
Wewe hata Dunia inavyoenda huelewi. Hivi mkoa na kanda ni sawa? Watanzania wengi ni watu wa kukurupuka, wana masikko makubwa lakini hawaelewi wanachosikia, wana midomo mikubwa lakini inayonena hovyo, wana macho ya ukubwa tofauti lakini yanayofanana katika upofu.

Kama huwezi kuelewa, angalao ukariri - Sumaye hatagombea kuwa mwenyekiti wa mkoa bali kuwa mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, nadhani inajumuisha mkoa wa Dar, Pwani na Morogoro.
 
we ndo umekosea, hakunaga mwenyekiti wa kanda!! sumaye anagombea uenyekiti mkoa wa pwani!!
 
a political joke: Tanzania ni nchi pekee ambayo mtu unaweza fanya mambo ya aibu na bado jamii ikakuona kama mtu wa kipekee sana.
 
Naona mnamnadi Kaseja Mbeya City!, kumbukeni alikuwa Simba na Yanga katika ubora wake. Sasa hivi hata umri sio tena ule wa kuzuia michomo manake hata Ndanda wanajipigia 3. Sumaye alikuwa premier kwa miaka 10 huko huko CCM na aliviona vyama vya upinzani na wala hakutamani kuwapa dola leo ndio anageuka kurumbizi.

Nyie watu chukueni tahadhari kwa watu aina ya Sumaye, huyu ni miongoni mwa watu wasioamini unaweza kuishi bila ya kuwa mheshimiwa sasa wanatafuta kwa udi na uvumba uongozi ili hadhi zao zisishuke.
 
Fredrick Tuluway Sumaye leo anaongea haya. angevuta kumbukumbu kidogo aina ya utawala alioufanya wakati akiwa PM ndani ya ccm. wale waislam kule mwembechai aliwafanya nini na alikuwa akisimamia wapi

Mboa humtaji na Muu wa Mkoa wa DSM wakati ule naye alifanya nini pale Mwembechai.

Acha kupandikiza chuki za kidini wewe!!!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Naona mnamnadi Kaseja Mbeya City!, kumbukeni alikuwa Simba na Yanga katika ubora wake. Sasa hivi hata umri sio tena ule wa kuzuia michomo manake hata Ndanda wanajipigia 3. Sumaye alikuwa premier kwa miaka 10 huko huko CCM na aliviona vyama vya upinzani na wala hakutamani kuwapa dola leo ndio anageuka kurumbizi.

Nyie watu chukueni tahadhari kwa watu aina ya Sumaye, huyu ni miongoni mwa watu wasioamini unaweza kuishi bila ya kuwa mheshimiwa sasa wanatafuta kwa udi na uvumba uongozi ili hadhi zao zisishuke.

kwani ameshuka hadhi kivipi, je na viongozi wa CCM wanaong'ang'ania madaraka nao wanataka hadhi zisishuke???

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom