Mimi nakubaliana kabisa na wewe mkuu. Walikuwa wanamtafutia mazingira ya kuishi kabla ya kuanza kutajataja mambo yake ili asiwepo akitakiwa kukamatwa.
Hata hivyo bado naona giza kwa kauli kinzani toka Ikulu. Katibu Mkuu kiongozi anasema lazima uchunguzi kwanza ufanyike; Mkuu anasema atatoa majibu ndani ya wiki...bado kuna kusigisishana kwa hali ya juu kwa taarifa mbili tofauti toka ofisi moja. Naona jambo hili itabidi libebwe kichama zaidi kuokoa images za wakubwa. Hii inaweza kumaanisha kuwa waliokwapua walikwapua kwa niaba ya chama ndiyo maana ukiwa gamba hata bila kufikiria mara mbili unawatetea hawa jamaa na wizi wao.
udhaifu wa vyombo vya ulinzi
Na rangi ya kilemba....
Vipi Katiba Mpya imeishia wapi?
Na kisha mkuu "atamteua" mwingine kuendeleza biashara kiaina. Nchi yetu shamba la bibi bana!Ndo maana walikuwa wanapinga asikamatwe ili atoroke kwanza
Imeripotiwa kuwa Singasinga wa IPTL ametoweka kwa kuogopa mkono wa dola(Raia Mwema,leo 10.09.2014).
Je,unafikiri kuna uhusiano wowote kati ya kusuasua kutekelezwa kwa maazimio ya bunge na kutoweka kwa bwana Seth Singh?
Na baada ya kutoweka anaweza kurudi tena nchini au atafuata nyayo za homeboy wake Daudi Balali?
==============================
Nasubiri wa kumwadabisha Chenge kama yupo Hapa Tanzania!
Harbinder Singh ni mfanya biashara hawezi kuvunja safari zake alizokwisha panga nje ya nchi bila sababu ya maana, kwasasa yupo huru wapi umeiona Arrest Warrant ya kumkamata. Maagizo unayosema ya bunge hao viongozi waliotajwa kwa majina.
,wamesimamishwa kazi? wamefanywa nini? Raisi amesema suala hili bado linachunguzwa Wakati watuhumiwa wanaendelea kuwa kazini. Hii imetoka tusahau huu uchunguzi hauna mwisho.