Simulizi: Kurudi Kwa Moza

SEHEMU YA 21


Rose alipotoka kwenye shughuli zake kama alivyopanga alimpitia mwanae na kwenda nae mahali,
“Tunaenda wapi mama?”
“Kwa babu”
“Babu yupi?”
“Yule anayefanya tuwe na nguvu”
“Mbona mimi simjui huyo?”
“Utamjua tu, yeye ndio kiboko alinisaidia hata kupata mimba na kukuzaa wewe. Yeye ndiye aliyenisaidia hata kumfanya Yule mzee ndani anisikilize mimi tu. Wewe mwanangu una nguvu za ziada ila huyu babu ndio atakupa nguvu zaidi maana ndio anayejua kuhusu wewe vizuri”
Walivyofika kwa Yule babu, walisikia sauti ya Yule babu ikiwaambia,
“Mmeshachelewa tayari”
“Tumechelewa kivipi?”
“Ndani ya nyumba yenu mlikuwa mnaishi na mtu wa hatari sana”
“Bado sijaelewa, hebu nieleweshe vizuri babu”
“Fanyeni hima mkamzike Yule mtu”
“Nani tena?”
“Kwani hujui? Yule msichana wako ameshakufa”
Rose na mwanae Ana walishikwa na bumbuwazi, na kujikuta wakiuliza kwa pamoja tena kwa mshangao,
“Amekufa!”
“Ndio amekufa, yani hakuna cha Moza tena wala mdudu wa Moza”
“Ila mbona ulisema tumechelewa? Na amekufaje kufaje?”
“Mngewahi tungemmaliza wenyewe mtu huyu”
“Kwahiyo kamalizwa na nani?”
“Kamalizwa na mpira wa maajabu”
“Kheee kautoa wapi huo mpira?”
“Si mliuweka kwenye bustani, sasa ameuchukua wakati wa kumwagilia”
“Kheee mpira wangu, sasa itakuwaje babu”
“Hakuna namna, cha msingi ameshakufa. Cha kufanya nyie muwe wa kwanza kuioana maiti yake, kisha ule mpira msiutoe mikononi mwake, hakikisheni mnamzika nao. Kisha mimi nitawatengenezea mpira mwingine, yani hakikisheni ule mpira mnamzika nao. Msiutoe kabisa mikononi mwake”
“Sasa tusipotangulia sisi kumuona itakuwaje?”
“Jitahidini muwe wa kwanza nyinyi sababu nitawapa dawa ya watu wengine kutokuuona ule mpira, yani mtakuwa mnauona nyinyi tu. Jitahidini kesho muuzike. Mwisho wa Moza umefika tena kautafuta mwenyewe”
“Basi inabidi tufanye haraka maana watoto wangu nina mashaka nao wasije wakaenda kumtoa bure. Ngoja niwapigie simu niwaongezee majukumu ili wasirudi nyumbani”
Muda ule ule Rose akaanza kuwapigia watoto wake, akampa kila mtu majukumu ambapo kwa majukumu waliyopewa ilikuwa ni vigumu sana kurudi nyumbani yani ni lazima wangerudi kesho yake ambayo hata huyo Rose ndio alipanga kesho yake hiyo ndio amzike Moza. Ana akamuuliza mama yake,
“Kwani watakuja watu kwenye huo msiba?”
“Watu watoke wapi? Kwanza ndugu wa Moza hatuwafahamu yani hapa tutaongea na vijana tukamzike na ikiwezekana sijui tukiwahi tumzike usiku huu”
Yule mganga akawaambia,
“Hapana Yule si wa kuzikwa usiku, anatakiwa kuzikwa mchana kwenye jua kali kabisa sababu ndio itakuwa uthibitisho wa kifo chake na hakika hatawasumbua tena kwani hata kumbukumbu yake haitakuwepo”
“Sasa si watu wa serikali watatushtukia?”
“Kuna dawa nitakupa ya kumwaga getini kwako pindi tu ukirudi kisha kila kitu kitakuwa shwari kabisa. Hakuna mtu atakayejua chochote”
“Utakuwa umetusaidia sana, yani Yule msichana loh nilitokea tu kutokumpenda ila cha kushangaza kumfukuza nilikuwa siwezi ila kajiua mwenyewe bora maana hata kwa Mungu sina dhambi juu yake. Kajimaliza mwenyewe”
“Nawapa na dawa ya kuoga yani baada ya maziko ya Moza mkaoge, ila baada ya wiki mje tena kuna tambiko inabidi tulifanye, Yule Moza hakuwa mtu wa kawaida Yule kama wengine”
Basi Rose na Ana wakaondoka zao huku Ana akimuhoji mama yake,
“Moza hakuwa mtu wa kawaida kweli mama maana tukipanga hivi yeye anafanya vile, ila kufa sijui ndio kafaje kafaje”
“Tutajua huko huko nyumbani tukifika”
Njiani gari yao ikapata pancha, ikabidi Rose atafute watu wa kuziba pancha ya gari yake.

 
SEHEMU YA 22


Leo Salome akiwa nyumbani kwao na mama yake, akamueleza kuhusu alivyokutana na Moza na jinsi alivyompeleka hadi anapoishi,
“Jamani kumbe kasharudi hapa mjini”
“Ndio mama”
“Naomba kesho unipeleke nikaonane nae maana nina mengi ya kuzungumza nae”
“Sawa mama nitakupeleka”
“Unajua Yule Moza alikuwa na utambuzi wa hali ya juu yani alikuwa anatambua mambo sana, natumaini nikikaa kyzungumza nae basi tutazungumza mambo mengi sana. Halafu kuna kitu nataka anisaidie”
“Kitu gani hicho mama”
“Salome, wewe bado mwanangu ila ukikua utaelewa yote ambayo mwanawake yanatupata. Kuna dawa alishawahi nidokeza ipo kwa bibi yake”
“Huyo bibi yake ameshakufa”
“Kheee amekufa! Maskini jamani yani yeye alikuwa anasema amebakiwa na bibi yake tu, kumbe alikufa masikini dah! Ila natumai hiyo dawa atakuwa anaijua”
Basi Neema na mtoto wake wakapanga kuwa kesho yake waende huko anapoishi Moza ili Neema akazungumze nae bila ya kujua kuwa huyo Moza ameshapatwa na majanga kule nyumbani.

Kwa upande wa Sara nae alipopigiwa na mama yake simu na kuambiwa kuwa aende Morogoro na airudi nyumbani siku hiyo hadi kesho yake kwakweli moyo wake ulikuwa mzito sana kufanya hivyo,
“kwakweli mama nae amezidi, kwanini asiniambie tangu asubuhi kuwa niende Morogoro? Yani anakuja kuniambia jioni hii hapana kwakweli, sijisikii kabisa kwenda Morogoro muda huu. Nitaenda tu kesho asubuhi, ngoja nirudi nyumbani nitamwambia tu nyumbani kuwa nimeshindwa kwenda Morogoro saa hizi”
Wakati anapanga hayo akapigiwa simu na namba mpya na kuipokea,
“Nani mwenzangu?”
“Ommy anaongea hapa”
“Kheee Ommy jamani, ulivyonifanyia sio vizuri Ommy unajua name nina moyo”
“Naelewa Sara, ila nataka kuzungumza na wewe kwanza”
“Sasa muda huu naenda nyumbani, labda uje nyumbani au unasemaje?”
“Sawa, hata mimi nipo mitaa karibu na kwenu. Basi wewe ukifika tu nishtue nije”
“Sawa”
Akakata simu, yani hapo ndio wazo la kwenda Morogoro kwa wakati huo likakatika kabisa kwani mawazo yake yote alikuwa akitaka kumsikia Ommy atasema nini baada ya kutokuonana nae kwa kipindi kirefu sana.
Safari yake muda huo ilikuwa ni moja kwa moja nyumbani kwao.

 
SEHEMU YA 23


Kwakweli lile swala la pancha liliwakosesha sana raha Rose na mtoto wake Ana, huku wakijiuliza kilichopelekea hali hiyo. Ana akamuuliza mama yake,
“Hivi kwa mfano wakina kaka na dada warudi nyumbani na wao wawe wa kwanza kumuona Moza amekufa itakuwaje?”
“Kwanza swala la kurudi nyumbani bila ruhusa yangu hawawezi kufanya hivyo. Wananisikiliza sana wale na nimewaambia kazi ya Morogoro ni ya le oleo sio ya kulala ile”
“Sawa mama, lakini watoto wako hawajielewagi wale haswa dada Sara na kaka Kulwa”
“Hata kama wakiona wao kwanza hakuharibiki kitu, najua Sara ni muoga sana kwahiyo akiona cha kwanza atanipigia simu na nitamwmbia asifanye chochote yani wale wasikutishe mwanangu yani Moza lazima tumzike na asahaulike katika dunia hii. Kwani kuna kosa tumefanya hapo? Kifo si amekitaka mwenyewe! Mwache afe”
Rose bado alikuwa anashughulika na vijana wazibe ile pncha hata alishangaa ni kwanini imechelewa vile kwani hakudhania kabisa kama itachukua muda mrefu hivyo.
Ila fundi aliyekuwa anatengeza alimuhakikishia muda huo kuwa ndani ya masaa machache atakuwa ameshamaliza.

Ilikuwa ni saa kumi na mbili jioni ikienda saa moja, mlinzi pale getini alishangaa sana siku hiyo bila kumuona Moza hata mara moja,
“Mmmh sio kawaida yake, tuseme amekosa cha kuniuliza kabisa leo? Ila mbona sijasikia kelele zozote za mapishi ndani? Ila ni sababu mimi sili chakula cha ndani humo ila nina wasiwasi, sijui Moza ni mzima!”
Muda kidogo alifika Sara akiwa ameongozana na huyo mgeni wake aitwaye Ommy, na kumkaribisha ila wakati wanaenda ndani huyu mlinzi akamwambia,
“Sara, mwambie Moza sio vizuri kunichunia leo”
“Mmh umeanza kumpenda nini Moza!”
“Hapana ila sio kawaida yake”
“Sema ukweli bhana, au kumtongoza unaogopa. Mmmh! Kwanini hizo salamu zako usimuagize Ana”
“Bado hajarudi”
“Mpaka saa hizi duh!”
“Yani wewe ndio wa kwanza kurudi”
“Labda anarudi na mama yake Yule”
Kisha Sara akawa anamkaribisha mgeni wake ndani hadi ameingia nae sebleni,
“Yani leo mama alikuwa anataka niende Morogoro”
“Sasa hujaenda na leo mmh si ndio atanichukia mimi?”
“Hapana bhana, nilighairi kwenda kabla hata hujanipigia simu”
Kisha Sara akaanza kumuita Moza ili amletee kinywaji mgeni, aliita na kuita ila Moza hakumuitikia,
“Huyu Moza vipi? Sio kawaida yake kukaa kimya akiitwa au alilala jioni ndio kalala hadi saa hizi”
“Nenda kamuangalie, usimlaumu tu labda anaumwa”
Sara akaenda moja kwa moja chumbani kwa Moza, akagonga ila hakuitikiwa akaamua kufungua mlango, akashangaa kumuona Moza amelala chini. Alimsogelea na kumtikisa,
“Weee wewe Moza weeee”
Ila Moza hakumuitikia na kumfanya Rose ashikwe na mashaka na kwenda kumuita Ommy,
“Njoo unisaidie kumuangalia sijui kapatwa na nini maana hasemi chochote”
Ommy akaenda na Sara hadi chumbani kwa Moza, alivyomshika tu Ommy akagundua na kumwambia Sara,
“Huyu mtu ni wa baridi, inaonyesha amekufa muda mrefu sana”
“Amekufa!”
“Ndio amekufa”
Sara aliishiwa nguvu kabisa na kujikuta akikaa chini, alihisi kama akili yake inaruka huku akisema
“Moza amekufa, hapana jamani. Moza amekufa!”
Akajikuta akipiga kelele za yowe na kufanya hata mlinzi aingie ndani ilia one kuna nini,
“Kuna nini Sara?”
“Eti Moza amekufa uwiiiii jamani Moza amka jamani, nyie niambieni ni uongo Moza hajafa. Jamani Moza amka jamani”
Mlinzi akamuangalia Ommy, naye Ommy alimuonyesha ishara kuwa amuangalie pia Moza nay eye alipomtazama aliona kweli amekufa yani hata yeye mlinzi ingawa alikuwa ni mwanaume ila machozi yalimlengalenga. Ommy akamuangalia saran a kumwambia,
“Kulia hakusaidii Sara, bora tumpeleke hospitali akahifadhiwe halafu wakirudi nyumbani hapa ipangwe mipango ya mazishi”
“Siwezi kujizuia Ommy, labda uniambie huko hospitali anaenda kupimwa vizuri ila Moza hajafa bhana”
“Sawa anaenda kupimwa vizuri, basi njoo uchukue kanga zake tumfunikize kisha tumpeleke hapo hospitali ya karibu”
Basi Yule mlinzi alipomuinamia Moza pale chini, alimuona na kile kimpira ambapo alikitoa kwenye mkono wa Moza na kukitupia pembeni ambapo kilikusanyika na nguo zingine chafu za Moza maana Moza mwenyewe alikuwa amepanga siku hiyo afue ila mauti ikamshika na kuzuia kufua kwake.
Sasa walikuwa wanawaza kumyanyua hapo kwani kwa kawaida za maiti huwa ni nzito sana ila ilikuwa tofauti kwa maiti ya Moza yani alikuwa ni mwepesi hadi mlinzi aliamua kumbeba mwenyewe, kisha Ommy akampigia simu dereva wa gari za kukodi ili wampeleke hospitali. Ila walipotoka nje na kutaka kwenda kumpakia kwenye gari, muda huo huo Rose na mwanae walifika kisha Rose akawauliza kwa mshangao,
“Kuna nini hapa?”
Sara akajibu kwa uchungu sana huku akilia,
“Moza amekufa mama”
“Kwahiyo kama amekufa ndio mnataka kufanyaje?”
Akajibu mlinzi,
“Tunataka kumpakia kwenye gari tumpeleke hospitali”
“Hivi nyie mna akili kweli? Mtu ameshakufa sasa hospitali akafanye nini?”
Ommy akajibu,
“Wakaupumzishe mwili wake”
“Ili iweje? Mlisikia wapi maiti anachoka hadi apumzishwe”
“Mmmh mama”
“Kelele na wewe Sara, huna akili hata moja wewe. Huko kupumzisha mwili hospitali mnadhani ni bure? Hubu rudisheni hiyo maiti chumbani kwake halafu tupange shughuli za mazishi kesho. Mnafikiri ni rahisi kuhifadhi maiti eeeh! Rudisha hiyo maiti upesi”
Alimfokea Yule mlinzi, ikabidi airudishe ile maiti ya Moza chumba kile alichokuwa analala Moza. Kila mmoja pale alibaki amestaajabu haswa Sara hakufikiria kama mama yake anaweza akawa katili kiasi kile tena kwa mtu ambaye ameshakufa.
Yule dereva wa gari za kukodi ilibidi aondoke kwani alipigwa na butwaa kwa maneno ya Yule mama, na ndio akaenda kusambaza maneno mtaani kuwa nyumba ile ina msiba.
 
SEHEMU YA 24



Walirudi sebleni ambako walikuwa wakimsikiliza mwenye nyumba kwa makini kabisa kuhusu taratibu za mazishi,
“Kesho saa saba mchana tutaenda kuzika”
“Khee mama hatuwatafuti ndugu wa Moza?”
“Hivi nani atafanya hiyo kazi ya kutafuta ndugu huku akiendelea kuhifadhi maiti kwenye nyumba yake? Kwanza nimemuhurumia tu, ilitakiwa nikamzike leoleo”
“Mmh mama jamani!”
“Kelele na wewe, wewe ndio mbaya. Hivi hamjui kuwa mambo mengine mnajitafutia kesi bure tu. Hata sitaki majirani wajue kama kuna msiba hapa. Na kulia kwako sitaki kusikia, unamlilia ndugu yako huyu? Alikuwa ni mfanyakazi tu, kwanza kwenye nyumba hii hana hata mwezi halafu anakufa unajifanya kulia lia, umemzoea lini. Hebu nitolee balaa mie.”
Rose akainuka na kumuinua mwanae Ana ili waende chumbani kuichunguza vizuri maiti ya Moza.

Waliingia chumbani kwa Moza na kuichunguza vizuri ila hawakumuona na kitu chochote mkononi, wakajaribu kupekua mule chumbani kwake ila hawakuona chochote,
“Sasa itakuwaje mama?”
“Yani hata sielewi hapa, inamaana ule mpira umeyeyuka au? Si Yule mganga amesema tuhakikishe anazikwa nao?”
“Ndio, sasa tutafanyaje mama?”
“Lakini ilimradi amekufa basi hakuna kitu kitakachoharibika, cha msingi tuhakikishe tu kesho tunamzika”
“Sawa mama, ila inabidi tufanye kitu ili Sara aache kulia kabisa watu wasije wakajua kama kuna msiba hapa”
“Usijali juu ya hilo, ngoja nikamtimue Sara aondoke na huyo Ommy wake”
Rose na Ana wakaelekea sebleni ila walipofika tu waliona jambo la kushangaza sana.

 
SEHEMU YA 25



Rose na Ana wakaelekea sebleni ila walipofika tu waliona jambo la kushangaza sana.
Walikuta watu wamejaa sebleni tayari kwa maombolezo, kwakweli hiki kilikuwa ni kitu cha kuwashangaza sana kuwa watu wote wale wametoka wapi kwa muda mfupi ule. Lakini kabla hajajiweka sawa kuwauliza maswali, wakafika wengine yani Rose alizidi kuchukia, nao wakawa wanamsogelea na kumpa pole kwa msiba.
Ikabidi Rose akae chini sasa na kuzungumza na waliokuwa karibu yake,
“Mmmh watu wa huku mna ushirikiano, hivi mmejuaje kama kuna msiba ikiwa hata sisi wenyewe tumejua muda huu”
“Kuna Yule dereva Juma, amepita mtaani na kutuambia wote nyumba baada ya nyumba kuwa huyu msichana wa hapa amekufa. Kwakweli tumesikitika sana, alikuwa mtu wa watu sana huyu msichana”
Rose akashangaa kuwa mtu wa watu kivipi wakati hata mwezi hana kwenye nyumba yake, ikabidi aulize tena,
“Kwani mlikuwa mnamfahamu?”
“Ndio, Moza tena tusimfahamu! Siku ya kwanza tu alikuja kujitambulisha kila nyumba kuwa anaitwa Moza na anaishi hapa. Tena mara zote alipokuwa akienda gengeni alikuja kutusalimia, kwakweli tumemfahamu kwa kipindi kifupi halafu amekufa. Inasikitisha sana, ndiomana unaona watu wote hawa wamekuja msibani, ni muda mfupi tumemfahamu Moza ila alikuwa ni mtu wa watu”
Rose akainuka na kwenda chumbani kwake akawaza kuwa Moza alikuwa anapata wapi muda wa kwenda kuwatembelea majirani na kuzungumza nao,
“Yani kuna wengine pale hadi mimi mwenyewe siwajui ila Moza wanamfahamu loh kweli huyu msichana kwa umbea alishindikana jamani”
Ana nae akafika chumbani kwa mama yake na kumuuliza,
“Sasa mama tutafanyaje?”
“Yani hapa nachanganyikiwa kabisa, yote haya kayasababisha Sara na kiburi chake, lile toto sijui nilibadilishiwa hospitali! Kwakweli sio toto langu lile”
“Sasa mama huu sio wakati wa kulumbana, unajua watu ni wengi na bado wanaendelea kuja huku kila mmoja akiulizia chanzo cha kifo cha marehemu. Sijui tufanyeje kuwatoa hapa nyumbani”
“Hebu kaniitie kwanza huyo Sara”
Ana akatoka na kwenda kumuita Sara.
 
SEHEMU YA 26


Alifika sebleni na kukuta watu wameongezeka kushinda wale wa mwanzo tena wengine walijaa nje, yani ilionyesha wazi majirani wa hapo walitaka siku tu wapate nafasi ya kwenda kwenye nyumba hiyo maana ni kitu cha kushangaza kuwa watu wamesikia msiba muda sio mrefu na washajaa nyumba yenye msiba, ni kwamba hawakuwa na majukumu mengine walikuwa wanasubiri tu msiba utokee au ni nini, ila Ana alihisi kuwa watu hao walikuwa wakitamani sana kuingia kwenye nyumba ile. Kwahiyo siku hiyo ilikuwa imetokea kama bahati hivi. Ana alienda kumuita Rose ambaye alikuwa katikati ya watu wakimuuliza chanzo cha kifo cha marehemu,
“Kwakweli hata hatujui ni nini labda aliumwa gafla maana tumerudi tu tumemkuta amekufa”
“Dada unaitwa na mama”
Sara alimwangalia mdogo wake kwa makini sana maana siku hiyo alimuita kwa heshima zote, kisha akainuka na kwenda chumbani alikoitwa na mama yake. Kufika kule Rose akaanza kumwambia mwanae,
“Fanya ufanyavyo hao watu waondoke kwenye nyumba yangu”
“Kheee mama wataondokaje na wamekuja msibani”
“Sara sitaki ujinga, msiba msiba, msiba huo vipi? Kwani hapa ni nyumbani kwakina Moza? Hapa ni kwao hadi waje hapa? Waambie waende kwakina Moza huko kijijini ndio wakafanye msiba, nyumbani kwangu siwataki, kwanza nataka kulala saa hizi”
“Kwakweli mama siwezi, labda uje kuwaambia mwenyewe ila mimi siwezi”
Sara alitoka chumbani kwa mama yake na kumfanya mama yake azidi kupatwa na hasira huku watu kwenye sebule yake wakizidi kumkera.
“Sikiliza mwanagu Ana, kachukue nguo zako kisha uje tulale huku wote. Naenda kuzima umeme wakae na giza hapo sebleni”
Ana akaenda kuchukua nguo na kwenda chumbani kwa mama yake ambapo mama yake akawasha taa ya kuchaji mule chumbani na kuzima umeme wa nyumba nzima kisha wao wakajifungia chumbani.
Sebule ilitawaliwa na giza totoro na kufanya ndani kutishe kiasi ila sababu watu walikuwa wengi na wengine wakawasha tochi za simu zao ikasaidia kufanya ndani kusitishe sana. Ila kulikuwa na matukio yaliyofanya watu wasipatwe na usingizi pale kwani kulikuwa kama kuna vitu vinawapitia kichwani, sema kwavile watu walikuwa wengi kwahiyo wasiwasi ukawa sio mkubwa.

 
SEHEMU YA 27


Kulipokucha, Rose alijua watu wameondoka. Akaoga na kuvaa vizuri kisha kumuandaa mtoto wake ila walipotoka sebleni walishangaa kuona watu wamejaa, huku wamama wawili wa makamo wakimfuata Rose na kumuuliza,
“Sasa asubuhi hii tutapika nini kuwapa watu hawa? Na je upo tayari tulete kuni tuanze mapishi?”
Rose akawaangalia kisha akawauliza,
“Kwani watu hawa hawana makwao?”
“Wanapo ila wamekuja msibani”
“Kwani msibani ndio sehemu ya kumaliza njaa zao? Wakale makwao”
“Makwao kupo, hata kulala hapa msibani ni heshima tu halafu ni utaratibu wetu waafrika mpaka pale tutakapozika”
“Sikia nikwambie, sina hela ya kulisha watu hao halafu nyumbani kwangu sitaki mpikie makuni. Waambieni wakale makwao”
“Dada jamani usiseme hivyo, watakususia msiba mwenyewe”
“Usitake kunichekesha na wewe, kwani wakisusa ndio nini, sitaweza kuzika au nini? Nitoleeni balaa mie”
Rose alikuwa na hasira sana na watu hawa, kisha akatoka na mwane Ana bila hata ya kumwambia Sara. Wale wamama ikabidi waende kumueleza Sara walichojibiwa na mama yake,
“Jamani Yule ndio mwenye nyumba, sina usemi mimi.”
“Mmmh makubwa ya leo, nimehudhuria misiba mingi tu lakini hakuna msiba wenye vimbwanga kama huu mara tuzimiwe taa usiku,mara tutembelewa na wadudu popo si popo sijui wadudu gani wale, haya kumekucha eti kila mtu akale nyumbani kwake mmmh sijawahi kusikia mie. Hata kuturuhusu tupike uji jamani!”
Ikabidi hawa wamama wafikishe ujumbe kwa wengine, lakini watu walisema wataondoka kidogo kidogo kwenda kula ili tu washuhudie mwisho wa msiba huo utaishia wapi.
Sara akaona vyema ampigie simu na baba mwenye nyumba ili ampe hizo taarifa maana wanadhalilika mtaani halafu akawapigia simu na wale mapacha ambao walikuwa tayari Morogoro,
“Kuna msiba huku?”
“Msiba? Wa nani tena? Au baba kafa?”
“Hapana sio baba, ni Moza amekufa”
“Kheee Moza amekufa jamani masikini, loh tunageuza tunakuja huko msibani”
“Sasa mama anavyofanya vihoja huku msibani yani anatudhalilisha mtaani haswaaa. Njooni kaka zangu bhana tusaidiane”
Halafu na Mr.Patrick nae akampa habari hizo ambaye alibaki anashangaa tu ila akakumbuka kuwa mkewe amemwambia jana yake kuwa asirudi kabisa nyumbani,
“Mmmh Sara kwakweli hiyo habari imenishtua sana, nakuja nyumbani muda sio mrefu”
Sara akapumua sasa baada ya kupiga simu hizo na kushukuru kwa kupiga kwani kidogo zimempa amani baada ya kuambiwa na ndugu zake kuwa wanakuja.


 
SEHEMU YA 28


Mr.Patrick akiwa na harakati za kuwahi nyumbani kwake, njiani akamuona mtu amesimama barabarani. Alikuwa ni mwanamke amejitanda khanga, ikabidi Patrick ashuke ili ajue huyo mwanamke amekumbwa na nini, alipotaka kumtazama Yule mwanamke aligeuka na kumwambia Patrick,
“Usinitazame”
Patrick akashtuka sana kwani sauti ilikuwa kama sauti ya Moza, Patrick alijikuta akimuuliza Yule mwanamke kwa wasiwasi sana,
“Mbona sauti kama ya Moza”
“Ndio, mimi ni Moza”
Kwakweli Patrick alipatwa na uoga zaidi na kuuliza kwa wasiwasi zaidi,
“Ila nimeambiwa kuwa Moza amekufa”
“Umeambiwa hivyo ila kiukweli mimi sijafa”
“Kwahiyo wewe ni Moza?”
“Ndio mimi ni Moza, unatakiwa kunisaidia kwani msaada wangu kwasasa ni wewe”
“Kheee sasa mimi nitafanya nini?”
“Nitakupa maelekezo ya kufanya ukifika nyumbani, halafu jitahidi nisiende kuzikwa saa saba kama alivyopanga mama bali nizikwe saa tisa”
Yani Patrick alikuwa anamsikiliza huku akitetemeka sana, Yule mtu alimpa malekezo mzee Patrick ila hakumuangalia usoni kabisa na wala mzee Patrick hakumuona kwahiyo alimuamini sababu tu ya sauti ilikuwa ni ya Moza.
Mzee Patrick aliondoka mahali pale huku akili yake ikiwa haipo kabisa kwenye muelekeo wa kawaida kwani jambo aliloliona halikuwa la kawaida kabisa kwake.

 
SEHEMU YA 29



Nyumbani kwa Rose, kwenye mida ya saa tano, Rose alirudi na mtoto wake Ana ila bado watu walikuwa wamejaa pale nyumbani kwake kwani wote walikuja kwa nia ya msiba, Rose akawaambia watu wale,
“Nishaongea na wachimba kaburi, kwahiyo saa saba tutaenda kuzika”
Wale wamama wa asubuhi wakauliza,
“Kwahiyo na ndugu wa Moza watakuwa wamefika muda huo?”
“Hivi nyie watu mnafikiria kwa akili gani, yani nitunze maiti kwenye nyumba yangu nikisubiria ndugu zake!”
“Si ungempeleka hospitali”
“Halafu hiyo hela ya kuhifadhia maiti mtatoa nyie?”
Wakawa kimya, ila wakaongezea lingine
“Basi turuhusu tukamsafishe marehemu kabla ya maziko. Na tuwaite watu wa dini kwaajili ya mazishi”
“Hivi nyie ndio mnamfahamu sana Moza kushinda mie, mnaijua dini ya Moza nyie? Kipindi hiki nilichoishi naye, sijawahi kumuona akienda kanisani wala msikitini. Hakuna siku aliyoongelea kanisa wala msikiti, sasa nyie mnataka kuita watu wa dini wafanye nini wakati mtu huyu alikuwa mpagani. Hebu niondoleeni ujinga mie”
“Basi tukamsafishe”
“Hivi mbona mnakazania sana au nyie wachawi? Maana sio kwa kukazania huko. Nitamsafisha mwenyewe”
Ikabidi wawe kimya na wangoje huo muda ambao amesema wa kuzika ufike, Rose na mwanae wakaingia ndani ila watu pale msibani yani kila mtu alikuwa akiongea lake kuhusu ule msiba na mwenendo wa pale msibani.
Kwenye saa sita na nusu, mzee Patrick nae alifika nyumbani kwake, ila muda huu mkewe alikuwa ndani kumbe alikuwa akijiandaa kwa maziko.
Moja kwa moja alionana na Sara kwanza ambapo alimuuliza,
“Maiti ya Moza iko wapi?”
“Chumbani kwake baba”
“Nahitaji kuiona”
Patrick aliongozana na Sara hadi chumbani kwa moza, ambapo Patrick alimuomba Sara akamletee maji, wakati Sara ameondoka Patrick akatumia muda huo kuipulizia ile maiti dawa aliyoambiwa na mtu aliyekutana nae huku akisema kama itafanya kazi sawa na hata isipofanya kazi hakuwa na namna zaidi kwani alifanya vile alivyoelekezwa. Kisha alienda kuifunua ile maiti na kumpaka ile dawa puani, Sara alikuwa amerudi na kumshangaa baba yake,
“Baba, unafanya nini tena?”
“Unajua nilikuwa siamini kabisa kama Moza amekufa kweli, ndio nikawa namuangalia hapa”
Wakasimama, muda kidogo akaja Rose ambapo alishangaa kumuona mume wake hapo,
“Mchezo gani huo umeanza wa kurudi bila kusema?”
“Nisamehe mke wangu, ila niliambiwa kuna msiba ndiomana nikarudi”
“Haya sasa mtoke nataka kuita vijana wambebe tukazike maana wachimba kaburi washanipigia simu kuwa tayari”
“Mmh mke wangu kwahiyo tunamzika kama hivyo tu?”
“Ndio, tunamviringisha nguo zake tunamzika”
“Mmmh mke wangu jamani, kwanini tusimwagizie jeneza!”
“Sina hela za mchezo, huyu msichana hana hata mwezi halafu nianze kumgharamikia hivyo. Siwezi kwakweli wanakuja kumchukua tukazike. Kwanza nimechoka kukaa na maiti yake humu ndani kwangu”
Patrick akawa anawaza ni njia gani atumie ili waweze kidogo kupeleka mbele muda wa kuzika kama alivyoombwa na Yule mtu, basi akajifanya amemuitikia pale mke wake kisha akawa anatoka akaanguka chini na kumfanya Rose aache kuwapigia simu vijana wa kuja kumbeba moza ili kuzika na kuanza kushughulika na mumewe,
“Vipi tena?”
"Mguu wang"
“Mguu wako! Umeteguka au?”
Ikabidi amshike na kumkongoja hadi chumbani kwao ambapo Patrick alionekana kulalamika kweli kuhusu mguu, ikabidi Rose amchue kwanza.
 
SEHEMU YA 30



Mapacha wa Rose nao walifika kwenye saa saba kwahiyo Sara alikuwa akiwapokea ndugu zake na kuwaeleza kinagaubaga kuhusu kifo cha Moza kwa uelewa wake,
“Kwahiyo ulimkuta tu ndani ameshakufa?”
“Ndio, ila mama kafanya vituko sana”
“Ila mama yetu tunamfahamu, na watu hawa walivyojaa hapa najua ndio amechefukwa balaa”
“Na amesema tunaenda kuzika muda sio mrefu”
“Ila hicho kifo nina mashaka nacho hata sio cha kawaida ila wengine tukisema midomo michafu, ngoja nikae kimya tu.”
Wakamsubiria mama yao pale, mzee Patrick nae alimpotezea muda Rose hadi alihakikisha saa nane inamfikia pale ndio akamuacha achukue vijana aende kuzika ila yeye alisema haendi sababu bado alikuwa na maagizo mengine aliyopewa na yule mtu kwahiyo alitaka kuyatekeleza wakienda makaburini na kubaki mwenyewe nyumbani.
Rose alitoka na kutaka watu waharakishe huku akiwaelekeza maeneo ya makaburi ili waanzage kwenda, basi alichukua na vijana wakumtoa Moza mule ndani ila hata wale vijana walimshangaa Moza kwakweli alikuwa mwepesi kabisa kama hawajabeba mtu vile ingawa aliviringishwa mashuka ila bado alikuwa mwepesi sana.
Wakati watu wanatoka ndio njiani wakakutana na Salome na mama yake ambao walikuwa wanaenda kwa Moza, walipoona watu wengi wengi wanatembea ikabidi waulize,
“Kuna nini kwani?”
“Kuna msiba, Yule msichana muongeaji. Mpenda watu amekufa”
“Nani huyo?”
“Anaitwa Moza”
Kwakweli nguvu ziliwaisha kabisa ila ilibidi waongozane na hao watu makaburini, lakini Salome alikuwa haamini kabisa.

 
SEHEMU YA 31


Walifika makaburini, na wale waliobeba maiti nao walifika makaburini. Wakataka kuzika sasa, ila Salome aliwafata na kuwaomba
“Naombeni hata mnionyeshe tu dada Moza nimuone kama kweli amekufa”
Wale vijana wakamuangalia Rose na kumuuliza,
“Eti tumruhusu amuone?”
“Ametoka wapi huyo, aone nini na yeye embu atutolee balaa huko. Hakuna cha kuona, zikeni na nyie tumalize watu waende zao maana wanataka tu kushuhudia moza anavyozikwa”
Kwa wakati huo Rose hakumtambua Salome kabisa kwani alikuwa na mawazo yake, kwanza kashachelewa muda wa kuzika.
Wale watu walimtumbukiza Moza kwenye shimo, ila bila kutegemea Salome nae aliingia kwenye lile shimo. Ndani ya muda huo kila mmoja akistaajabu tukio la Salome, walipoenda kumchungulia Salome kwenye kaburi la Moza alionekana amekauka kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme.


Wale watu walimtumbukiza Moza kwenye shimo, ila bila kutegemea Salome nae aliingia kwenye lile shimo. Ndani ya muda huo kila mmoja akistaajabu tukio la Salome, walipoenda kumchungulia Salome kwenye kaburi la Moza alionekana amekauka kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme.
Neema hakutegemea lile tukio la mtoto wake kabisa, akajikuta akipiga kelele za yowe, ilibidi vijana waingie kwenye lile kaburi kumtoa Salome na kumpeleka kwenye gari ili kumuwaishe hospitali ambapo mama yake naye alifatana nao hospitali ila kitu cha kushangaza kwenye kaburi la Moza haikuonekana maiti yoyote wala zile nguo walizokuwa wamemfungia yani kwa kifupi maiti ya Moza ilitoweka yani kila mmoja alipigwa na butwaa kwani ni kitu ambacho hakuna aliyekitarajia kabisa kwa wakati huo.
Pale kaburini kulikuwa na mzozo mkubwa kuwa maiti imeenda wapi, kila mtu hakuelewa kitu chochote kwani ilikuwa ni kwa muda mfupi sana kwa Salome kutumbukia kwenye kaburi na kutolewa halafu maiti ya Moza kutokuonekana, hakuna aliyejua kuwa maiti iko wapi kila mtu alikumbwa na bumbuwazi.
Wakati wapo kwenye mshangao pale kaburini mara upepo mkali ulianza kuvuma huku vumbi jingi likipepea na kufanya watu wafunge macho na baada ya muda kila mtu alisambaratika na kujikuta pale kaburini wamebaki wale vijana na Rose.
Kwahiyo walijiona wenyewe baada ya upepo ule,
“Jamani, mbona mambo ya ajabu sana haya. Kwakweli mama kwaheri, kazi ya namna hii siiwezi tena”
Mmoja alisema hivyo, huku mwingine akisema
“Yani unasikia kabisa wengine wakikimbia na kuondoka ila sisi kama tumeshikiliwa na sumaku. Kuondoka hatuwezi”
Na walipojaribu kuondoka walishindwa kwenda, ikabidi mmoja atoe wazo kuwa wafukie kwanza kaburi, kwakweli Rose alikuwa kimya kabisa kwani hakutegemea kama ingekuwa vile.
Walifukia hadi walifanikiwa kumaliza, na walivyomaliza tu walijikuta wakiweza kuondoka, kwakweli walikimbia kutoka pale makaburini balaa.
Rose alienda kwenye gari yake huku akitafakari bila ya majibu, kwa wakati huo hata hakujiuliza kuwa mwanae Ana yuko wapi, wazo lililomjia kwa muda huo ni kwenda kwa Yule babu ili akapate ukweli wa mambo kuwa imekuwaje kuwaje maana hakuelewa.
 
SEHEMU YA 32


Nyumbani nako, Patrick alikuwa anafanya maelekezo aliyopewa na Moza bila kujua kuwa yale maelekezo yaliharibu kila kitu makaburini kwani yale maelekezo karibu yote ndio yaliyofanya yale yaliyotokea kule makaburini.
Kwani alitafuta kile kimpira kwenye ngui chafu kama alivyoambiwa, kisha akakibeba na zile nguo na kwenda nje ambapo alichimba shimo na kuingiza zile nguo pamoja na ule mpira kwenye shimo, halafu akakata ua aliloelekezwa na kulidumbukiza kwenye lile shimo, ua lile lilisinyaa gafla hata yeye mwenyewe alishtuka kwakweli maana kile kitu hakikutegemea kabisa. Basi akatoa zile nguo pamoja na lile ua, kisha akautupa ule mpira pembeni halafu akaviringisha lile ua kwenye nguo chafu akapeleka ndani, halafu alivyorudi ndio akamwagilizia mafuta ya taa na kuuchoma ule mpira huku akipepea moto, na ndio kitendo hicho kilichopeleka upepo kule makaburini, baada ya hapo ndio akatumbukiza majivu kwenye lile shimo na kulifukia, ndiomana kule makaburi wale wahusika waligandishwa mpaka watakapo fukia kaburi.
Alipomaliza alirudi ndani, alishangaa watoto wake wale wakirudi kwa kasi ya ajabu nyumbani, kila mtu alirudi kivyake ambapo walitangulia wale mapacha, kisha Sara na Ana walikuwa wanahema juu juu, ikabidi aulize kwa makini,
“Kwani imekuwaje tena?”
“Maajabu yametokea makaburini baba”
Sara alimjibu baba yao, Yule baba nae aliuliza kwa mshangao,
“Nini tena?”
“Kuna binti mmoja hivi sijui katokea wapi alikuwa anataka kumuangalia Moza mara ya mwisho wakamkatalia, sasa Moza alipotumbukizwa kaburini Yule mtoto nae alitumbukia. Sasa muda huohuo huyo mtoto alikauka gafla kama mtu aliyeungua, sasa mama yake akawa analia wamtoe mwanae. Walivyomtoa na kupanda kwenye gari kwenda hospitali, muda huo huo kwenye shimo nako hakionekana maiti ya Moza wala nini, mara upepo mkali wenye mavumbi ukaanza kuvuma kwakweli kila mtu pale kaburini alikimbia na njia yake. Ni maajabu makubwa kakweli.”
“Kheee ni maajabu sana, sasa mama yenu yuko wapi?”
“Atakuwa anakuja tu maana kila mtu alikimbia pale kaburini hakuna aliyebaki hata mmoja”
“Makubwa haya jamani”
Ila Ana akadakia na kumuuliza baba yake,
“Kwanini wewe hukwenda? Hukutaka kumzika Moza?”
“Hapana mwanangu, niliteguka mguu”
“Sasa huo mguu saivi umeacha?”
“Saivi afadhali”
“Mmh nitajua tu”
“Utajua nini?”
Ana akawa kimya hakuwajibu tena, ila kila mtu alikuwa na maswali kwa kile alichokisema Ana kuwa kama kina ukweli ni mambo gani yanaendelea huku Patrick akiwa na mashaka kuwa inawezekana Ana ametambua alichokifanya na inawezekana aliyoyafanya ndio yamesababisha yote hayo ila akajisemea moyoni ni amri alipewa kwahiyo hakuwa na namna.
 
SEHEMU YA 33


Kwenye gari ambalo Neema alikuwa amepanda na mtoto wake Salome huku akimpeleka hospitali, machozi yalikuwa yanamtoka mfululizo kwani aliamini kuwa mwanae alikuwa amekufa ukizingatia alikuwa amekauka kabisa kama aliyepigwa na shoti ya umeme. Kijana aliyewabeba kwenye gari alikuwa anaendesha haraka haraka ili awahi hospitali kwani hata yeye alipatwa na huruma kwa mtoto Yule ila walipokuwa wanakaribia hospitali, ikawa kama miujiza kwani Salome aliamka gafla na kumfanya mama yake hata machozi yamkatike, kwani alipoamka tu alimwambia mama yake,
“Msinipeleke hospitali tafadhali, nirudisheni nyumbani”
Mama yake alimuangalia kwa kustaajabu sana,
“Ila mwanangu tunatakiwa tukupime kwanza”
“Nirudisheni nyumbani, sitaki kwenda hospitali. Huko mkinipeleka nitakufa”
Hata Yule dereva alipatwa na mshangao tu, Neema alimuangalia dereva na kuanza kumuelekeza ili waende nyumbani.
Kwahiyo safari ilibadilika haikuwa ya hospitali tena bali safari ya nyumbani, kwakweli Neema alikuwa anamuangalia mwanae bila ya kummaliza kwani alimuona kama amebadilika hivi. Mpaka wanafika nyumbani na kushuka,
WAkati wanashuka, Salome alimwambia mama yake,
“”Tafadhali usimwambie yeyote kilichonipata”
“Kwanini?”
“Sitaki wajue mama wataniogopa, tafadhali usimwambie yeyote”
“Nakuahidi sitamwambia yeyote mwanangu, uzima wako ndio furaha yangu”
“Niahidi tena mama kuwa hutomwambia yeyote”
“Nakuahidi kweli mwanangu, hakuna yeyote nitakayemwambia”
Salome alionekana akishangaa shangaa tu mazingira ya pale kwao, mpaka mama yake akamuuliza,
“Mbona unashangaa hivyo Salome?”
“Naona kumebadilika”
“Hapana hakujabadilika, ni huku huku ndio nyumbani kwetu”
Waliingia ndani na Ashura ndio alikuwepo nyumbani na wale mapacha wadogo zake Salome, ila Salome alipomuona Ashura alimwambia,
“Khee Ashura bado upo huku?”
Mama yake alishangaa na kumwambia kwa mshangao,
“Kheee wee Salome, toka lini mama yako mdogo umemuita kwa jina lake? Adabu ya wapi hiyo? Halafu unamuuliza bado upo huku, ulifikiri mamako mdogo atakuwa wapi! Yani usingekuwa umepatwa na matatizo leo ningekupiga sana”
“Nisamehe mama”
Ikabidi Ashura nae aulize,
“Matatizo, kwani amepatwa na matatizo gani?”
“Mwenzangu makubwa”
“Yapi hayo?”
Salome akamuangalia mama yake na kumwambia,
“Kumbuka umeniahidi mama”
“Naelewa mwanangu”
Sasa Ashura akabaki na bumbuwazi na kuzidi kuuliza kulikoni imekuwaje kuwaje,
“Aaah si huyu Salome, kagombana na wenzie shuleni huko ndio leo niliitwa shuleni kwao”
“Kheee kwahiyo muda ule mnaondoka hapa ilikuwa mnaenda shuleni kwakina Salome? Imekuwaje leo kwenye kesi zake amekuchukua wewe badala ya kunichukua mimi?”
“Anaelewa makosa yake, tuachane na hizo habari mdogo wangu. Hebu tufikirie leo tutakula nini?”
“Tumuulize huyo mpenda ugomvi, leo anataka kula nini?”
“Nataka ugali, mlenda wa kuchanganywa na ngoga na samaki”
Neema na Ashura wote waliangaliana na kumuuliza Salome kwa mshangao tena kwa pamoja,
“Wewe ngoga unaijua?”
“Ndio, si ndio nyanyachungu”
“Toka lini ukala ugali Salome? Mpenda wali wewe, leo hii unataka ugali makubwa!”
“Tena ugali na ngoga, mbona makubwa haya ya leo dada”
“Makubwa haswaaa, huyu Salome wangu wa leo ni kiboko”
Salome akainuka na kwenda chumbani, ambapo alifika na kujilaza.
Baada ya muda mama yake akawa anamtafuta,
“Salome kaenda wapi jamani?”
“Ila sijamuona akitoka”
Mara wakaja wale mapacha wawili na kumwambia mama yao,
“Kalala chumbani kwetu”
“Kheee kalala chumbani kwenu, hivi Salome mzima akili yake kweli leo? Ameshasahau kama analalaga na mamake mdogo”
Neema akainuka na kwenda kumuasha Salome, alipoamka alikaa nae na kuzungumza nae
“Hivi Salome umeanzaje kuja kulala huku? Tuseme hujui chumba unacholala au? Hujui kama unalala na mamako mdogo wewe? Halafu hata kuoga hujaoga, hivi yale mambo yaliyotokea unaona ni madogo yale mwanangu? Naomba uinuke ukaoge halafu kama kulala ukalale chumbani kwenu”
“Mama naomba unisaidie kitu”
“Kitu gani hicho?”
“naomba msaada wako ila usimshirikishe mtu yeyote”
“Wewe niambie tu, simwambii mtu mwanangu”
“Kwakifupi mama kuna vitu mimi nimesahau, vitu vingine naomba unipe maelekezo”
“Sasa mwanangu, lile tukio halikuwa la kawaida ndiomana nikakwambia twende hospitali wakakucheki”
“Mama nitakuwa sawa tu, naomba vitu vingine unielekezage na usimwambie mtu yeyote. Lile tukio lililonitokea mimi kweli halikuwa la kawaida na limehusika haswa na mambo ya kishirikina ndiomana sitaki unipeleke hospitali maana huko utanipoteza kabisa, je upo tayari mwanao nife?”
“Sipo tayari mwanangu, nitaumia sana”
“Basi naomba iwe siri yako, mtu yeyote asijue, hata mabadiliko yangu asijue mtu yeyote. Wewe ndio mama yangu nakutegemea, naomba unielekezage tu cha kufanya”
“Haya niambie unataka nikuelekeze nini”
“Nielekeze chumba ninacholalaga, nielekeze nguo zangu za kuvaa, nielekeze choo chetu kilipo nikaoge”
“Mmh mwanangu inamaana vyote hivyo umesahau? Mbona unanitisha?”
“Usiogope mama yangu, nifanyie hivyo tu”
Neema aliinuka na kuanza kumuelekeza mwanae, ambapo aliporudi sebleni na kumuacha Salome anaoga ndipo Ashura nae akauliza,
“Imekuwaje tena, mbona Salome kama haeleweki hivi!”
“Achana nae, akili yake inawaza kupigana tu hapo”
Ashura akawa kimya ila alihisi kuna kitu cha tofauti kimempata Salome ingawa hakujua ni kitu gani.


 
SEHEMU YA 34


Nyumbani kwa mr.Patrick, napo usiku ulifika bila ya Rose kurudi nyumbani ikabidi Patrick awaulize tena watoto wake,
“Jamani mna uhakika mama yenu alikuwa anakuja na yeye?”
Sara alijibu,
“kwakweli baba hatujui maana pale kila mtu alikimbia na lwake”
“Kwahiyo hata hamna wasiwasi na mama yenu?”
“Atarudi tu baba, mama ni mtu anayejielewa na uhakika atarudi”
“Hivi na huyo binti ambaye alianguka kwenye kburi la Moza mnajua hali yake?”
“Kwakweli hakuna aliyefatilia, hata sijui anaendeleaje na hatumjui kwakweli hata watu pale makaburini walisema hawamjui zaidi ya huyo aliyekuwa akilia na kudai ni mama yake”
Ni kweli hawakumtambua Salome kwani ilikuwa ni kitendo cha muda mfupi sana lakini bado mr.Patrick alijikuta akitaka kujua mengi kuhusu huyo binti, nab ado jibu lilikuwa vile vile hatujui.
“Sawa nimekubali, huyo binti sio ndugu yenu ndiomana hamjamfatilia. Haya mama yenu nae haonekani nyumbani. Kumfatilia nae inakuwaje?”
“Mmmh baba jamnai, kwahiyo tukashatki polisi kuwa mama haonekani?”
“Sio hivyo, ila ningeomba mnipeleke huko makaburini nikamtafute mke wangu”
“Hivi atakayekupeleka makaburini muda huu ni nani? Ukizingatia tumetoka kumzika mtu wa maajabu, kwakweli baba hapana. Kwanza kwenda makaburini usiku ni nuksi”
Patrick aliinuka na kwenda chumbani, kwa upande mwingine aliona ni afadhali mkewe hayupo muda huo ila kwa upande mwingine alimkumbuka kwani alishamzoea maana tayari ni mke wake na alikuwa akiishi nae, kwa muda huo aliamua kulala tu.
Kwa upande wa watoto, Rose aliwaomba wenzie wakae sebelni kwa siku hiyo kwani aliogopa kulala peke yake, ila Kulwa akatoa wazo,
“Si uende ukalale na Ana”
Doto akasema,
“Mmmh na Ana atakubali kweli?”
“Ndio hapo sasa Doto, hebu nitetee na wewe. Hivi Ana atakubali kweli kulala na mimi?”
“Hebu nenda kwanza tuone”
Sara aliinuka na kwenda chumbani kwa Ana ambapo alimkuta ameshalala, hivyo alirudi na kuwaaga kaka zake halafu akaenda chumbani kwa Ana na kulala pembeni yake kimya kimya.
 
SEHEMU YA 35


Kwa upande wa Rose sass, akili yake ilikuwa haisomi ramani kabisa kwa wakati huo alijikuta anaendesha gari hovyo hovyo ili awahi kwa Yule mganga, njiani kwasababu ya haraka zake alizokuwa nazo akagonga mtu ila hakutaka kusimamisha kwani alijua angesimamisha wananchi wangemsongasonga hivyobasi akaendelea mbele huku watu wakimpigia kelele ila yeye aliongeza mwendo, na kuenda moja kwa moja gereji.
Lengo lake alitaka kubadilisha gari ili watu wasimjue kuwa ni yeye aliyegonga, kwavile mwenye gereji hiyo alimzoea Rose na alimjua kwa pesa zake, akampa gari nyingine bila kinyongo kisha Rose akamuachia ile gari yake bila ya kumwambia kuwa aligonga.
Rose akaendelea na safari ya kwenda kwa Yule babu na hatimaye akafika, alikuta wagonjwa wengi tu wakimsubiri. Mke wa Yule babu akamsogelea Rose na kumwambia,
“Yani leo yupo busy kweli na kazi yako, yani hata saivi ameenda kufata dawa kwaajili ya kazi yako maana kashaonyeshwa kuwa mambo yameharibika huko”
“Ni kweli mambo yameharibika yani nimechanganyikiwa hapa, sijui itakuwaje”
“Hata usijali, hakuna kitu ambacho babu anashindwa. Nina uhakika mambo yote yataenda sawa kama inavyotakiwa”
Basi walikaa muda mrefu sana bila ya babu kurejea hadi giza liliingia ila babu hakurejea hata mkewe akapata mashaka kuwa babu amekumbwa na maswahibu gani.
Kwenye mida ya saa nne usiku, walifika vijana pale nyumbani kwa babu na kutoa taarifa iliyowashtua wengi sana,
“Babu, kapata ajali. Akiwa njiani, kagongwa na gari na kufa papohapo sababu ya kucheleweshwa hospitali kwa matibabu”
Kwakweli taarifa hii iliraluwa moyo wa Rose, na kujikuta akichanganyikiwa sana, na alipouliza zaidi kuhusu gari iliyomgonga wale vijana walimtajia na hapo hapo akagundua kuwa ndio ile gari yake, Rose akaanguka na kuzimia.

 
SEHEMU YA 36



Kwakweli taarifa hii iliraluwa moyo wa Rose, na kujikuta akichanganyikiwa sana, na alipouliza zaidi kuhusu gari iliyomgonga wale vijana walimtajia na hapo hapo akagundua kuwa ndio ile gari yake, Rose akaanguka na kuzimia.
Ikabidi waanze kumpepea pale, yani mke wa babu alichanganyikiwa na taarifa ile ila akajua Rose imdmchanganya kutokana na mambo yanayomsibu. Rose alipepewa pale hadi akazinduka na aliona watu wanaanza kusogea nyumbani pale, kwakweli Rose alijiona kama yupo ndotoni kwani kila kitu kilitokea kwake bila ya matarajio, akamuita tena Yule kijana aliyeleta taarifa mwanzoni ili amuulize vizuri maana alihisi kama sio kweli vile,
“Hebu niambie vizuri ilikuwaje?”
“Yani mimi nilikuwepo kabisa eneo la tukio, babu alikuwa anavuka barabara mara ikatokea gari sijui mwenye gari alikuwa amelewa Yule yani alimgonga babu na kuondoka, tulijaribu kumpigia kelele ili asimamishe hakufanya hivyo. Pale tulipokuwepo ni mbali na hospitali, na msaada ulipatikana badae kabisa tena tulimpeleka babu na baskeli mpaka hospitali na kufika alikata roho hapo hapo, daktari akasema ni kwavile tumemchelewesha”
Hapo ndio Rose akaelewa kabisa kuwa hiyo ajali ameisababisha yeye na kumfanya achanganyikiwe zaidi ila akaogopa kuropoka kuwa amesababisha ajali klwani alijua angezua mengine makubwa zaidi. Akawaza kimoyo moyo,
“Sijui hata nifanyeje? Sina la kufanya kwakweli ngoja tu nisubirie pakuche halafu nitajua cha kufanya”
Alikuwa na mawazo mengi sana.
 
SEHEMU YA 37


Kwakweli leo Sara ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulala pamoja na mdogo wake Ana, kwahiyo siku zote huwa hajui kinachoendelea kwa Ana. Usingizi kwa upande wa Sara kwa siku ya leo ulikuwa ni wa mang’amung’amu sana kwani bado taswira ya makaburini ilimjia kichwani, akiwa kwenye usingizi wa kuvizia akamuona Ana akinyanyuka kitandani lakini alihisi kuwa Ana anaenda chooni kujisaidia. Ila Ana huyu alienda moja kwa moja dirishani na kutokea kwenye dirisha, kitendo hiko kilimshtua sana Sara na kumuogopesha, akajikuta akitazama pale ambapo Ana alilala mwanzoni. Kwakweli alistaajabu zaidi kwani alimuona Ana akiwa bado amelala hajitambui, jasho la uoga lilianza kumtoka Sara, ni kweli Ana ni mdogo wake ila matendo ya namna hii hajawahi kuyashuhudia kabisa. Sara alikuwa anaogopa hadi alianza kutetemeka kwa uoga, aliinuka haraka haraka na kukimbilia nje ya chumba huku akipiga kelele ambapo kaka zake walitoka na kumuuliza kuna nini, lakini bado alikuwa akilia kwa kelele nyingi, hadi kaka zake wakamshtua na kumuuliza kwa makini,
“Sara, Sara una nini wewe?”
Mara gafla akaja na Ana, kwakweli Sara ndio alizidi kuchanganyikiwa baada ya kumuona Ana na alikuwa akimnyooshea kidole,
“Sasa mbona unamnyooshea kidole Ana kafanyaje?”
“Ana ni……”
Kabla hajamaliza sentensi yake, Ana alimuangalia kwa jicho kali sana dada yake na kumfanya dada yake azimie pale, wale mapacha wakamuangalia Ana na kumuuliza.
“Kwani kapatwa na mimi?”
“Jamani mi nitajuaje sasa!”
“Utajuaje kivipi wakati ulilala nae!”
“Nililala nae? Alilala na mimi muda gani?”
“Mbona alikuja kulala na wewe”
“Mi hata sijui kama alilala na mimi, kwanza ndio ustaarabu wa wapi unaenda kulala na mtu hata umwambii ili akukubalie au akukatalie. Hata sijui kilichompata kwani na mimi nilikuwa nimelala”
Ilibidi wamuinue na kwenda nae sebleni ambapo waliendelea kumpepea ili azinduke huku wakitumaini kuwa akizinduka atawaeleza jambo.
Mara Ana akawaambia,
“Mnajisumbua tu kumpepea huyo, nendeni kamlazeni kitandani kwake halafu asubuhi akiamka ndio mtaongea nae”
Walimpepea pale bila ya mafanikio ikabidi wachukue wazo la Ana, wakambeba Sara na kumpeleka chumbani kwake kumlaza kisha na wao wakarudi chumbani kwao.
 
SEHEMU YA 38


Kulipokucha asubuhi, hwa mapacha kabla hawajafanya lolote walienda kwanza kumuangalia dada yao ambapo walimuamsha ni kweli aliamka, ila walichomuuliza chochote hakuwajibu ndipo walipogundua kuwa dada yao amepoteza uwezo wa kuongea.
“Sara, kuongea huwezi?”
Alitingisha tu kichwa, kwa kifupi Sara hakuweza kusema chochote, walitoka na dada yao hadi sebleni wakijitahidi kumsaidi ya hapa na pale, Mr.Patrick alikuja na kushangaa huku akiuliza imekuwaje,
“Inamaana baba hujasikia makelele ya usiku wakati dada Sara analia?”
“Sijasikia chochote wanangu, yani leo nilijikuta nimelala hoi kabisa yani hoi sikujitambua mpaka kumekucha kwahiyo hakuna nilichosikia”
Basi wakamueleza kinagaubaga kilichotokea hata yeye alibakia anastaajabu tu kwani bado ukweli alikuwa nao Sara pekee ila kusema tu ndio alikuwa hawezi kwani aliondolewa uwezo wa kusema. Ana alitoka na kuwaaga kuwa anaenda shule, Patrick akamuuliza Ana,
“Kwahiyo huna hata mashaka na mama yako hajarudi hadi leo, na vipi dada yako aliyepatwa na ugonjwa wa gafla haongei. Hivi unapata wapi nguvu za kwenda shuleni Ana?”
“Elimu ndio ufunguo wa maisha, kama nyie mlikimbia shule shauri zenu ila mimi acha nisome kwa raha zangu”
“Laiti kama kusoma kungekuwa unavyosoma wewe basi walimu wote Tanzania wangeacha kazi”
“Unanikosea heshima baba”
“Naomba unisamehe, haya nenda shule mwanangu”
Ana aliondoka zake ila inaonyesha alikuwa amekasirika vilivyo. Kulwa alimuangalia baba yao na kumuuliza,
“Baba unafahamu nini kuhusu Ana?”
“Ni mengi tu nayafahamu, huyu mtoto mbaya sana. Ndiye anafanyaga nilale kama mzigo”
“Hebu tueleweshe baba”
Mara Ana akarudi ndani, kisha akamuangalia baba yao na kusema,
“Nimeghairi kwenda shule”
Wote walimtazama Ana kwani ni maamuzi ya gafla ameyafanya, ila hawakumuuliza tena wala hawakuendelea kumuuliza baba yao mabaya ya Ana kwani ni wazi asingeweza kuwaeleza wakati Ana yuko pale.
 
SEHEMU YA 39



Kulikucha sasa nyumbani kwakina Salome pia ila leo Salome aligoma kwenda shule,
“Kheee makubwa, mwanangu leo kwenda shule hutaki?”
“Siendi mama, ila ungeenda kuniomnbea nipumzike kwa muda najiona siko sawa, kwakweli siwezi kwenda shule kwasasa”
Ashura nae akaingilia kati,
“Dada, kama hataki kwenda shule achana nae. Sio lazima shule, mwache azulule zulule akipata mimba ndio ataelewa”
“Kheee Ashura ndio maneno gani hayo kwa mwanangu, badala umbembeleze na wewe ndio unamkandamiza”
“Namkandamiza kitu gani, kwanza mtu mwenyewe vitu vingine anaongea hata haeleweki kama sio msomi na ndiomana jana sijampikia hizo nyanyachungu zake”
“Kwanini?”
“Atasemaje tumpikie ngoga eti ndio nyanyachungu wakati zinaitwa ngogwe”
“Aaah kumbe ndio zinaitwa hivyo”
“Wewe hukujua kama amekupiga changa la macho huyu tujue anajua Kiswahili kumbe hajui lolote, eti nipikieni ugali, samaki na ngoga. Katafute hiyo ngoga kama utaipata, hata sijui kaongea kilugha cha wapi”
“Ila Ashura ni swala tu la kumuelekeza mtoto kuwa sio ngoga ni ngogwe, huyu bado mtoto anajifunza vitu. Ni kumuelekeza tu, mi mwenyewe mtu mzima sijui sembuse huyu mtoto jamani mmh!”
“Kuwa makini na mtoto wako dada, kuwa naye makini sana”
Ashura alitoka muda huo na kusema kuwa anawahi sokoni ili akanunue vitu, kwahiyo Neema alimuongeza na hela kidogo.
Nyumbani akabaki Salome na mama yake, ila leo Salome alimuuliza mama yake swali ambalo mama yake hajawahi kutegemea kama angeulizwa na Salome.
“Mama, hivi wewe na Ashura undugu wenu uko vipi?”
“Halafu nishakwambia kuwa na adabu, Yule ni mamako mdogo ni mdogo wangu. Usimwitage Ashura”
“Nisamehe kwa hilo mama, ila ningependa kujua huyu mamdogo na wewe ni mdogo wako kivipi? Na ndugu zako wengine wako wapi sijawahi kuwaona?”
“Mmmh Salome jamani, si mwezi uliopita tu nilikupeleka kwa kaka yangu, tuseme ushasahau!”
“Haya mama, tuachane na hayo ila huyu mamdogo ni ndugu yako kivipi kuna jambo nataka nikueleze niambie kwanza undugu wenu ndio nikueleze”
“Sikia, mimi baba yangu na mama yangu walikuwa hawaishi pamoja na kwa upande wa mama na baba, mimi ni mtoto wao wa pekee sana ila kumbe baba alikuwa na mtoto mwingine ila sio mtoto aliyezaa na mkewe waliyokuwa wanaishi nae. Mimi kwa mama tumezaliwa wawili tu, yani mimi na kaka yangu niliyekupeleka kwake mwezi uliopita. Hatuna mazoea ya karibu sababu Yule kaka alikulia nyumbani kwa baba yake. Ila mama ndio alinitambulisha kama ni kaka yangu. Sasa kwa upande wa Ashura ni mtoto wa baba kumbe naye alikuwa analelewa na mama yake, yeye ndio alinitafuta mimi kwakweli alipojitambulisha nilifurahi sana kwani nilipata ndugu hadi leo niko nae.”
“Mmmh kwahiyo ulimpeleka kwa baba yako akutambulishe?”
“Baba alishakufa kitambo sana, na laiti kama angekuwa hai basi ningempeleka”
“Na huyo mke wa babu si yupo, kwanini usimpeleke akutambulishe”
“Sasa huyo atakuwa anajua vinini, kwanza wanitambulishe nini wakati mtu alishajitambulisha na tunaishia nae hadi leo”
“Je shangazi zenu na baba zenu wakubwa au wadogo mnawatembeleaga”
“Wapo kijijini, kwakweli hatujawahi kupanga safari ya kuwatembelea. Inatia uvivu ujue halafu hatujawazoea”
“Mmmh na kaburi la baba yenu je mmewahi kwenda kulitembelea?”
“Tunapangaga kufanya hivyo ila hata sijui inatokeaga nini, tunajikuta hatujaenda”
“Mama, ngoja nikwambie kitu. Huyu unayemuita mdogo wako si ndugu yako”
“Salome, si ndugu yangu kivipi?”
“Wewe nielewe tu mama ila si ndugu yako na kama hujui shauri zako, atakapokufanyia kitu kibaya ndio utashtuka. Na angekuwa amekufanyia kitu kibaya mud asana, ila wewe unalindwa na mzimu wa baba yako. Huna kosa na wala hustahili kufanyiwa mambo mabaya, ila kwa kifupi huyu si ndugu yako, Tafakari, maswali niliyokuuliza na majibu uliyonipa halafu chukua hatua”
Salome aliinuka na kwenda kuoga, muda huu Neema alibaki kwenye lindi la mawazo kwani hajawahi kufikiria hata mara moja kuwa Ashura anaweza akawa si ndugu yake,
“Jamani huyu Salome mbona ananitisha, halafu yeye kajuaje kama huyu si ndugu yangu? Hivi inawezekana kweli nimeishi siku zote na mtu asiye ndugu yangu huku nikiamini ni ndugu yangu! Haiwezekani jamani”
Neema aliwaza sana bila ya kupata jibu la aina yoyote ile, ingawa kuna mashaka aliyapata kwa jinsi alivyoambiwa na Salome.
Akajikuta akimsubiria kwa hamu Ashura atakaporudi ili amuulize baadhi ya maswali,
“Lakini hata hivyo, kama ni kweli si ndugu yangu ni kwanini amenidanganya? Hivi inawezekana kweli! Hapana nahisi Salome kachanganyikiwa tu”
Muda kidogo Ashura nae alirudi, na Neema alijikuta akimuuliza,
“Hivi Yule mke aliyekuwa anaishi na baba ulikuwa unamfahamu?”
“Aah ndio, hapana hata sikumbuki”
“Mbona sijakuelewa hapo, ulikuwa unamfahamu au la”
“Nilikuwa mdogo sana, hata sikumbuki kama namfahamu au la”
“Basi tupange siku tukamsalimie”
“Mmmh umekumbuka kitu gani?”
“Nimemkumbuka tu basi, najua atafurahi sana”
“Sawa tutapanga”
Ila Ashura alionekana kukosa furaha tangu Neema amuulize kuhusu mke wa baba yao.

 
SEHEMU YA 40


Rose alikuwa kwenye wakati mgumu sana na siku hii hakuweza kuendelea kuwepo tena pale msibani, aliamua kuwaaga kuwa anaenda kwanza nyumbani kwake halafu atarudi tena. Kiukweli alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa hivi, alijiona kama ameonewa kwa wakati huo. Mke wa babu alimfata Rose wakati anataka kuondoka,
“Jamani, kweli unataka kutuacha wenyewe kweli kwenye wakati mgumu kama huu”
“Hapana bibi, hujui tu jinsi msiba huu ulivyonichanganya hapa, nakosa hata uelekeo. Nina matatizo mzigo hata sijui naanzia wapi na kuishia wapi”
“Naelewa kama una matatizo ila tafadhali usiondoke hadi tutakapozika”
“Kwani mazishi ni lini?”
“Ni leo, halafu kesho utaondoka. Tafadhali sana naomba usiondoke”
Rose akajifikiria ila ikabidi apige simu nyumbani kwake kwani alijua ni wazi watakuwa na wasiwasi, na alimpigia simu Sara kwani anajuaga ndio kiherehere wa wasiwasi ila simu ya Sara iliita mara nyingi bila kupokelewa ikabidi ampigie simu mume wake,
“Mbona Sara hapokei simu, au kaenda kazini leo?”
“Hapana, Sara yupo ndani ila hawezi kuongea”
“Hawezi kuongea kivipi?”
“Sijui nikuelezeaje ila uwezo wa kuongea wa Sara umekatika gafla”
“kheee jamani, mambo gani hayo? Ngoja nirudi le oleo”
Rose akakata simu kisha akaenda tena kwa mke wa babu na kumpa taarifa za nyumbani kwake huku akimueleza kuwa anapaswa aende maana mwanae ni mgonjwa. Yule bibi hakuwa na namna nyingine zaidi ya kumruhusu tu.
Rose akapanda gari na kuondoka zake, alikuwa na mawazo mengi sana kushinda yale mawazo ya kwanza maana aliona kama matatizo yanamzidia ingawa kiuhalisia yeye ndiye chanzo cha matatizo yote.
Wakati anaendesha gari akasikia sauti,
“Rose, umenigonga nimekufa halafu kwenye maizshi yangu unakimbia!”
Rose alishtuka na kusimamisha gari kwa haraka huku akiwa amejawa na hofu iliyomfanya ashindwe hata kutazama nyuma ya gari kuwa hiyo sauti inatoka wapi. Akiwa amejawa na hofu zaidi, ile sauti ikajirudia tena, na kumfanya Rose ashuke kabisa kwenye gari ile, alipokuwa chini akatazama kwenye kioo cha gari gafla alimuona kama Yule babu yupo ndani ya lile gari.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom