Mwaka 2002 kuelekea 2003, mabadiliko makubwa na ya kihistoria yalifanyika katika simu na yakabadilisha kabisa muonekano na matumizi ya simu
1. Vioo vikubwa vya "colored screen" vilivanza kutumika rasmi
2. Camera zilianza kuwa sehemu muhimu ya simu ya mkononi
3. Intanet ilianza kukamata kwenye simu
Hizi ni baadhi ya simu zilizojizolea umaarufu mkubwa kipindi kile..
1. Sony Ericsson P900: Hii simu ilitoka mwaka 2003. Lengo la kuiweka namba 1 sio kwamba ilikua maarufu sana, (maana enzi zile nadhani ilikua inauzwa 800,000!!) bali ni kuonyesha jinsi ilivyokuwa mbele ya wakati. Simu hii ilikua na kioo kikubwa sana kwa wakati ule (2.9 inches, 65,000colors, 132ppi), Ilikua na internal memory kubwa (16Mb), Ilikua inasapoti memory card (128Mb), 156Mhz Cpu, VGA camera, MP4/MP3 player, na STYLUS! Ilikua ni simu kali sanaa..
2. NOKIA 6230/6320 n.k: Hivi visimu pia vilijipatia umaarufu mkubwa. Vilikua na polyphonic ringtones, mp3 player na camera.. Nilivitamani sana ila uchumi haukuruhusu maana vilikua na bei..
3. NOKIA 3100: Hii simu ilitokea kupendwa sana enzi zile, ilikua nzuri na simple, pia bei yake haikua kubwa saana kwahiyo watu wengi waliimudu. Iliuza zaidi ya nakala milioni 50 dunia nzima
4. Sony Ericsson T100/105: Hii simu ilipendwa sana miaka ile ya 2003. Ilikua nyembamba ndefu na watu walivutiwa nayo sana..
5. MOTOROLA RAZR V3: Ni kati ya simu zilizouza sana miaka ya 2003/4 kiasi cha kufikia mauzo ya nakala milioni 130! Simu hii ilikua nzuri sana na ilibadilisha muonekano wa simu kutoka kwenye simu nene na kuwa mwanzo wa simu nyembamba na zenye mvuto.
6. SONY ERICSSON T610: Kama wewe ulikua brazameni au sistaduu miaka ya 2003/4 lazima utakua unaifahamu hii simu. Ilikua na milio flani yenye stereo yaani ni full mchicha..! Na housing yake ilikua aluminium.
7. NOKIA 6600: Simu hii ilikua inauzwa 600,000 mwaka 2003. Na bado iliuza nakala milioni 150. Kwa sasa hivi unaweza kuiona kama haina ishu ila kwa enzi zile ukiwa nayo wewe ni noma. Ilikua na kioo kikubwa sanaaaa.. inchi 2.1.
8. MOTOROLA SLVR L6/L7: Hizi simu ziliuza mbayaa.. karibu kila mtu alikua nayo.. na zilikua kali.
9. SONY ERICSSON K750: Kiuhalisia, miaka ya 2003 - 2006 Ilitawaliwa na makampuni matatu tu - Sony Ericsson, Nokia na Motorolla. K750 ilipendwa sana kwasababu ya kuwa na internal memory kubwa (38 Mb) na Camera yenye kiwango, ya 2Mp.
10. NOKIA N70: Ni "Jiwe" lililoachiwa na Nokia mwaka 2005. Simu hii hadi leo kuna watu wanayo na inapiga kazi kama kawaida.. Simu hii ina kila kitu.. internet (3g), memory card, Camera mbili, Bluetooth, FM radio.. yaani we chochote unachokijua kwenye simu kipo humu.
Daah.. Kipindi hiki simu zilikua nyingi saana ila kwa leo tuishie hapo. Kama kuna uliyoipenda na hapo kwenye listi basi tupia hapo chini..
Kuna wimbo wa dully unaitwa julieta nakupenda kwa dhati, kuna kipande kataja simu aina ya siemens aisee kwa kipindi kile kumiliki simu ilikuwa ni anasa halafu simu zenyewe kioo hakikuwa cha rangi!!
Siemens C35. Simu hizi zilikuwa na umbo la kuvutia. Inasikitisha Siemens wamejitoa katika kutengeneza simu za mkononi. Nilidondosha hii kwenye daladala Dar es Salaam mwaka 2002
Samsung SGH R225. Hizi simu zilikuwa na mwanga wa kuvutia wa bluu kwenye screen. Wezi walikata wavu wa dirisha Sinza, Dar es Salaam, wakaniibia hii mwaka 2004.
Dah.. Mkuu hizi simu zilikua ghali sana..! Ila ni kati ya simu imara sana kutoka NOKIA. Nadhani hadi sasa kuna watu wanazo hizi simu.. Hizo 8800 huwezi amini hadi leo bei yake sio chini ya $200 (Brand New original from Finland)!
Dah.. Mkuu hizi simu zilikua ghali sana..! Ila ni kati ya simu imara sana kutoka NOKIA. Nadhani hadi sasa kuna watu wanazo hizi simu.. Hizo 8800 huwezi amini hadi leo bei yake sio chini ya $200 (Brand New original from Finland)!
Hahahaaaaa Aiseeee shule nzima mwaka 2001 kulikuwa na simu tatu tu,c25 mbili na Nokia 3210 moja,tulikuwa tunajazana kwa jamaa kwenda kuomba kutuma message!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.