Simiyu: Mwanafunzi adaiwa kufariki kwa kuchapwa viboko na kukanyagwa kichwani na mwalimu shuleni

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
1,013
1,634
Waalimu wa siku hizi hata sijui wapo vp maana ni tofauti na wale wa zamani,sasa sijui ni stress za maisha au vp na sijui hii kadhia itaisha lini kwa waalimu maana imekuwa too much
 
Mwanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari Mwasamba iliyoko Kata ya Lutubiga, Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu, Mhoja Maduhu (15) amefariki Dunia, huku chanzo cha kifo chake kikidaiwa kuwa ni adhabu kali aliyopewa na Mwalimu katika shule hiyo kwa kuchapwa fimbo 10 sehemu tofauti za mwili ikiwemo kichwani.

Mwanafunzi huyo alikuwa anasoma Kidato cha Pili katika shule hiyo, ambapo inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Januari 26, 2025, baada ya Mwalimu huyo kutoa adhabu hiyo na kwa Wanafunzi wengine 30.

Baadhi ya Wanafunzi ambao nao walipewa adhabu hiyo na Mwalimu, wamedai kuwa mwalimu huyo alikuwa anawapiga fimbo 10 kila mwanafunzi na alipofikiwa Mhoja baada ya kupigwa alianguka chini kisha kukimbizwa hospitali.

Wanafunzi hao wanadai kuwa chanzo cha adhabu hiyo ni wao kushindwa kufanya kazi ya majaribio kwa njia ya vikundi aliyokuwa amewapatia siku moja kabla ya tukio hilo kutokea.

Chanzo: Global TV
 
Daah
Inasikitisha sana
Huyo mwalimu hakua na majukum mengine ya familia yake mpaka achape watoto wa watu?
 
Waalimu wa siku hizi hata sijui wapo vp maana ni tofauti na wale wa zamani,sasa sijui ni stress za maisha au vp na sijui hii kadhia itaisha lini kwa waalimu maana imekuwa too much
Walimu wa zamani?... Ipi hiyo?
Tuliosoma miaka ya 80 Hadi 90 tunaijua shoo ya walimu wake linapokuja suala la mboko.
Mimi niliwahi pigwa mboko countless na mwalimu, Tena mtaani siku ya jumamosi, Wala siyo shuleni.

Anyway, walimu Wana mazingira magumu sana ya kazi.
 
K
Walimu wa zamani?... Ipi hiyo?
Tuliosoma miaka ya 80 Hadi 90 tunaijua shoo ya walimu wake linapokuja suala la mboko.
Mimi niliwahi pigwa mboko countless na mwalimu, Tena mtaani siku ya jumamosi, Wala siyo shuleni.

Anyway, walimu Wana mazingira magumu sana ya kazi.
Ukweli ni kwamba binadamu wa siku hizi wamekua delicate mno
Very soft tofauti na binadamu wa miongo kadhaa nyuma

Njia nzuri ya kuyaepuka haya ni kufanya yanayokuhusu pekee

Kwani hao wanafunzi wakifanya au wasipofanya homework mwalimu angepungukiwa na nini?
 
Halafu tukisema viboko vipigwe marufuku watu wanakataa bila sababu za msingi
Nidhamu sio viboko, kwani hata mbwa anafundishika bila fimbo, hata Punda anaweza kwenda bila mijeledi.

Sasa unaporuhusu kitu, haya ndio madhara yake
Hata mkisema ooh unaruhusiwa fimbo tatu ni sawa na kuruhusu zote

Mna vijitabia vya kuruhusu mambo ya kijinga sana
Unawaambia wafanyakazi wale kiasi
Au za kubrashia, ukijua fika watasomba zote na kazi yao itakuwa kuiba tu badala ya kutumika kazi walizoandikiwa

Wakati wote inatakiwa viongozi wenye Busara
 
Back
Top Bottom