Simbachawene umetukosea sana Graduate tunaouza chai na kutembeza viungo mabarabarani, pia tunaokula chakula cha mjomba, hiyo kazi tunaitaka sana

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,770
7,122
Polisi, Uhamiaji, Magereza na Zimamoto. Wote ni wizara moja. Sayansi mliyotumia inashangaza.

Hivi mnajua kwamba tunao-graduates wanauza chai kwenye vihoteli vidogo?

Mnajua kwamba kuna graduates wanaendesha bodaboda? Mnajua kuwa form six leavers wanauza matunda stendi na wengine ni vibarua wa ujenzi?!

Hamjui kwamba ktk ukosefu wa ajira hatuchagui kazi?

Kwanini msingewafanyia usahili halafu mkawauliza na kuwapa masharti yenu, ili watakaokubali muwape nafasi?

Kujiendeleza ni fursa ambayo ikitokea kazini mtu anachukua maamuzi. Kuna graduate ni dreva wa tajiri mmoja hapa nilipo, cheti kaacha nyumbani ili familia ipate kula.

Serikali, kama hamtaki wasomi mnasomesha wa nini? Mnavijua vyanzo vya upotevu wa amani? Sikuipenda na sitaopenda kamwe

Mtoto hachagui mbeleko, hata uzi waweza kumfaa
 
Kaidhalilisha kazi ya polisi, kwamba msomi hawezi kubeba bunduki, ashindwe vipi kubeba bunduki wakati yupo kitaa anapiga kazi ya saidia fundi kubeba zege.
 
Kaidhalilisha kazi ya polisi, kwamba msomi hawezi kubeba bunduki...........ashindwe vipi kubeba bunduki wakati yupo kitaa anapiga kazi ya saidia fundi kubeba zege.
Point yake ni kwamba, ww uliemaliza chuo Una nafasi ya kujiendeleza mpaka ukawa na nyota, sasa je ukiwa na nyota utalinda bank?
 
Waziri Yuko sahihi kabisa, ww unasema hivyo Kwa sababu hauna hiyo kazi, Ila Leo ukienda CCP after six months Tu utaomba kwenda kusoma ili upande cheo
 
Point yake ni kwamba, ww uliemaliza chuo Una nafasi ya kujiendeleza mpaka ukawa na nyota, sasa je ukiwa na nyota utalinda bank ?
Sasa mkijikuta polisi wote mna nyota kwa nini usilinde benki, nyota yako inaathiri vipi utendaji wa majukumu yako ambayo yapo kisheria........kama hospitali imejaa madaktari kwa hiyo wasichome wagonjwa sindano kwa sababu manesi wanaotakiwa kufanya hiyo kazi hawapo......​
 
Sina uhakika kama wamefanya utafiti wa Jambo hili lakini pia wasine sema wanaihitaji waliofeli wangefanya usaili na kuchakua Kwa kadri ya mahitaji pia wangerekebisha bylaw zao hakuna haki ya kutopandishwa cheo.

Tatizo ni kukiuka MFUMO wa ajila na upandishwaji wa VYEO .
Ukiacha kusajili au kupandisha cheo Kwa mwaka mmoja unaharibu mtiririko kwasababu kila mwaka watumishi wanastaafu,wanakufa,wanaacha KAZI,wanafukuzwa nk lazima mnyororo wa ajila utembee.

Tatizo lingine ni Polisi Kufanya kazi nyingi kushinda uwezo wao issue ya kulinda unatakiwa ifanywe na taasisi mbalimbali zilizojipanga Kufanya kazi hizo na kubakiza sehemu nyeti tu. Kusindikiza mahabusu kwenda na KURUDI mahakamani siyo KAZI ya Polisi kisheria na kunakazi lukuki zimeachiwa jeshi la Polisi ambazo zinastahili kufanywa na watu wengine.

Hivyo basi hoja ya kwamba tunaajili waliofeli ili wasipandishwe VYEO ilitakiwa ifanyiwe utafiti ingawa waliofeli nao wanahaki lakini MUHIMU ni weledi na uwezo wa kufundishika tusije kujaza wavuta bhangi na wasiofundishika kwani Siku zote tunahitaji Polisi WETU wawe na angalau uwezo wa kuwa reasonable katika utendaji wao wa KAZI.
 
Sasa mkijikuta polisi wote mna nyota kwa nini usilinde benki, nyota yako inaathiri vipi utendaji wa majukumu yako ambayo yapo kisheria...​

Inaonekana haujui mambo mengi ya kijeshi,

Ukishakuwa na nyota means ww ni Afisa,

Umewahi kumuona Dereva wa Jeshi lolote ana nyota ? Hata CDF au IGP Haendeshwi na mtu mwenye nyota
 
Sina uhakika kama wamefanya utafiti wa Jambo hili lakini pia wasine sema wanaihitaji waliofeli wangefanya usaili na kuchakua Kwa kadri ya mahitaji pia wangerekebisha bylaw zao hakuna haki ya kutopandishwa cheo...
Point yako na waziri ziko Sawa tofauti yenu ni kuwa ww umeongea kisiasa na yy ameongea uhalisia
 
Point yake ni kwamba, ww uliemaliza chuo Una nafasi ya kujiendeleza mpaka ukawa na nyota, sasa je ukiwa na nyota utalinda bank ?
Tusiendekeze kuwa kuna kazi wanatakiwa kufanya failures.kuna kazi ambazo enzi ya Nyerere angefanya yeyote kwasababu wasomi hawakuwepo.

Enzi hizi watu wamesoma kiasi kwamba kuwa graduate siyo mjadala tena mtaani.Ni vizuri watu wapewe mazingatio tu kwamba mtu hata kama ni graduate,akipata hiyo post atatumikia muda kadhaa,kabla ya kujiendeleza zaidi.

Lakini kusema kigezo cha post fulani ni pamoja kufeli form 4,haijakaa vizuri Sana.
 
Inaonekana haujui mambo mengi ya kijeshi,
Ukishakuwa na nyota means ww ni Afisa,

Umewahi kumuona Dereva wa Jeshi lolote ana nyota ? Hata CDF au IGP Haendeshwi na mtu mwenye nyota
Uafisa una ngazi zake, hata huyo asiye na nyota ni afisa........kwa hiyo ukiwa na nyota yako moja na wapo waliokuzidi hizo nyota bado wataweza kukupangia kazi ya kulinda benki.

Huo uafisa ni added advantage ya kwamba hutafanya majukumu ambayo unaweza kuwapangia watu wa chini yako.

Ila siyo tiketi ya kukuondoa kufanya au kuwajibika kwa majukumu ya ambayo ni sehemu ya wajibu wako ambao ndiyo msingi wa ajira yako, kulinda mali na usalama wa raia.
 
Inaonekana haujui mambo mengi ya kijeshi,
Ukishakuwa na nyota means ww ni Afisa,

Umewahi kumuona Dereva wa Jeshi lolote ana nyota ? Hata CDF au IGP Haendeshwi na mtu mwenye nyota
Kwa hiyo polisi wote wakiwa vilaza si tutazalisha enterahamwe kwa kuwa wao wamefundishwa kudunda tu na kutia vilema
 
Uafisa una ngazi zake, hata huyo asiye na nyota ni afisa........kwa hiyo ukiwa na nyota yako moja na wapo waliokuzidi hizo nyota bado wataweza kukupangia kazi ya kulinda benki...
Ndio maana nimekwambia CDF na ukubwa wake hawez kuendeshwa na mtu mwenye nyota, ww unaleta mambo ya kiraia, mtu mwenye nyota hawez kwenda kulinda bank na hawez kupangiwa kulinda bank
 
Back
Top Bottom