Simbachawene awataka viongozi wa walimu wasiokuwa na ajira NETO kufika ofinini Dodoma kwa mazungumzo

The Watchman

JF-Expert Member
Nov 7, 2023
722
1,183
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene, amewaita ofisini kwake Dodoma kwa mazungumzo viongozi wa vijana waliojitambulisha kwenye andiko lao kuwa ni “Non Employed Teachers Organisation (NETO)” wenye umoja wao kupitia mitandao ya Kijamii.

“Nimesoma makala yao yenye kichwa cha habari "Ombi la Wahitimu wa Ualimu Vyuo mbalimbali Nchini kati ya mwaka 2015-2023 kwa Serikali, andiko lao ni zuri na linaeleweka ingawa linahitaji ufafanuzi zaidi, hivyo ninatoa wito kwa vijana hao kuja ofisini Dodoma kwa mazungumzo”

Pia soma: Walimu Wasio na Ajira (NETO) wanaongea na waandishi wa habari kuondoa dukuduku lao

 
Wakuu,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene, ameagiza viongozi wa Non Employed Teachers Organisation (NETO) kufika ofisini kwake Dodoma kwa mazungumzo,

Agizo hilo la Waziri Simbachwene linakuja siku chache tangu umoja huo kuongea na waandishi wa habari na kutoa mapendekezo yao kwa serikali.

“Nimesoma makala yao yenye kichwa cha habari 'Ombi la wahitimu wa ualimu vyuo mbalimbali Nchini kati ya mwaka 2015-2023 kwa Serikali, andiko lao ni zuri na linaeleweka ingawa linahitaji ufafanuzi zaidi, hivyo ninatoa wito kwa vijana hao kuja ofisini Dodoma kwa mazungumzo” alisisitiza Mhe. Simbachawene.

Aliongeza kuwa amewasiliana na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda na Viongozi wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI na wamekubalina kushiriki mazungumzo hayo wakati kundi hilo litakapokuwa tayari.

Mhe. Simbachawene amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaongozwa kwa kuzingatia misingi ya Falsafa ya 4R (Maridhiano, Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga Upya), hivyo kwa moyo wa upendo amewakaribisha ili kupata maridhiano katika jambo wanaloona haliko sawa.

Aidha, amesema kuwa kuanzia tarehe 14 Januari hadi terehe 24 Februari, 2025 Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (UTUMISHI), Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; Wizara ya Afya; Tume ya Utumishi wa Walimu, Ofisi za Wakuu wa Mikoa yote na wataalamu mbalimbali kutoka katika Taasisi za Umma inaendesha usaili wa kada za Ualimu.

“Usaili huu una lengo la kujaza nafasi elfu kumi na nne mia sita na arobaini na nane (14,648) zilizotolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kupunguza uhaba wa walimu nchini” alifafanua Mhe. Simbachawene.

simba.png

Source: Jambo TV
 
Kuweni makini vijana.....huyo simbachawene ana ukaribu sana na jeshi la polisi na ni miongoni mwa viongozi kutoka ccm ambao wapo tayari kumfanya mtu chochote kile pale Tu akiona ugali wake unataka kuchezewa..........Bora hata angekuwa ni mchengerwa kidoooooogo ana hofu ya MUNGU, nendeni japo kuweni makini sana....
 
Ni wapuuzi na hawana akili kuchakata mambo kwa upeo. Mpaka wanaunda NETO waliona ni lazima waajiriwe tu kwa kuwa wamesomea ualimu? Ni wapumbavu na wana fikra mgando kuhusu kuajiriwa
Umeongea kwa ukali Sana. Wazo langu kwao....kama wako laki tano (mfano tu)
500,000 x Tsh.10,000@=5,000,000,000 yaani Tsh. Bilioni Tano. Watafute namna ya kujiajiri. Ni hayo tu.
 
Simbachawene nilikuwa namuona ana utimamu ila hapa amefeli sana 😔 mkienda ndo mmekwisha
 
Wakati wanafeli kuendelea na taaluma zao walizokuwa wanazipenda wakakimbilia ualimu kwa kuona ni mserereko kupata ajira kwani hawakujua kuwa miaka hii kuna wahitimu wengi kuliko taaluma zingine? Wawe wavumilivu, serikali haiwezi kuwaajiri wote kwa wakati mmoja ni si lazima uajiriwe kwa kuwa ulisomea ualimu
 
Vipi umoja wa wahitimu wahandisi, madaktari, wahasibu, wafamasia nk nao wakatoa misimamo yao? Nao wataitwa?
 
Back
Top Bottom