GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,424
- 120,762
- Thread starter
- #41
Kama Simba walikuwa wanayajua yote hayo kwanini walikaa kimya na kufumbia macho hayo unayoita madudu Siku zote hadi waone dalili Za kupokwa points ndio watishie kuyaanika?
Mpira wa Tanzania upuuzi mtupu!
Tulikuwa tunasubiri kuchokozwa ili tuwanyooshe vizuri. Si unaona sasa mkwara wetu Simba SC wa kuitisha Mkutano na Waandishi wa Habari umesababisha TFF watuogope na sasa nasikia wamehairisha tena Kikao cha kumjadili Fakhi na kuamua kuwa kwa sasa Simba SC ibaki na hizo points mpaka hapo watakapokutana tena. Mkuu Simba SC ni Chama lingine na kama TFF ya Jamal Malinzi na hao Watendaji wake wangeipokonya tu Simba SC points zake tungekinukisha CAF na FIFA madudu yote ya TFF ambayo bahati nzuri sana Watu wa ndani wa TFF na ambao pia ni Mnyama Mnyamani ( Wapenzi wa Simba wa Kufa Mtu ) wanayajua.
Sasa waambie Chura Churani ( Yanga FC ) wenzio kuwa watulize vipira vyao na waachane kabisa na Simba SC na wajikite sasa katika kuwalipa Mishahara Wachezaji wao na mmoja wapo leo Saa 5 nimemnunulia Chai ya jero maeneo ya Kariakoo na kainywa kwa pupa hadi kaungua Ulimi kwa njaa Kali na sidhani hata kama ataweza kufanya mazoezi.
Njaa zimewatawala tu mnang'ang'ania kushoboke mambo ya Mume wenu Simba SC. Na mwaka huu tuko radhi hata Kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa kufanya lolote ili mradi tu Simba SC tuwe Mabingwa. Tutaroga na tutahonga vibaya sana hadi Ndoo inyanyuliwe kudadadeki zenu Kandambili / Gongowazi nyie.