Simba itaingia fainali ikiwa huko Afrika kusini

Mkuu Hawa watu wamekua wakiitabiria Simba hii ya Fadlu kushindwa Kila siku lkn imekua ikiwaonesha maajqbu.

Tukianza na msemaji wa Yanga aliwahi kunukuliwa akijisifu kua katika timu zote za Tanzania zinazoshiriki michuano ya Afrika itabaki timu moja TU nayo ni Yanga,lakini matokeo yake Imebaki Simba.

Kuna wapo waliosema itaishia robo fainali ,lkn Leo IPO nusu fainali.

Kuna waliosema itatolewa na akina Mabululu lkn ikawatoa.

Kuna waliosema itashika mkia Katika kundi lake lkn ikaongoza kundi.

Kuna waliosema itatolewa na Al Masry lakini Al Masry ndio katika.

Kuna waliosema itafungaa na Stellenbosch lakini Simba ndio imemfunga Stellenbosch.
Sasa wamebaki kuhoji kwa Nini Simba imefungaa goli moja.

Wanasahau kwamba Stellenbosch nayo ni timu kama simba ilikua inacheza kujilinda ili sisifungwe magoli mengi,nayo Simba ikienda huko itacheza kuhakikisha haipotezi mchezo huo,na hata kupata goli jingine.
Simba hii ya Fadlu imekua ikidharauliwa lakini inaenda.

Pamoja na kua timu haijakaa muda mrefu wachezaji kuelewana lakini inaonesha maajqbu.
Ndio maana Kila mshabiki wa Simba ana kikosi chake kichwani tofauti na Fadlu ni Kwa sababu timu bado inajengwa lkn inafanya vizuri.
Wanasema hivyo kwa sababu ya Quality za wachezaji waliopo Simba.
Hii timu inafanikiwa kwasababu ya Hamasa na Upepo + kucheza na Timu ndogo zisizojulikana kabisa.

Wachezaji wa Simba wana ubora Mdogo sana, Haishangazi kufungwa na yanga 5 times.
Kukosa ubingwa 4 times.
Kukosa shirikisho 4 times.

Haiwezekani timu yetu kuzidiawa Ubora wa wachezaji na singida
 
Timu iliyoanzishwa 2016
Wachezaji wake kufanana na simba 1946 ni kitu cha Aibu sana.

Timu bora No 4 Africa kufanana na Stellabosch ni aibu mno nina uhakika Stellabosch haipo hata TIMU40 BORA za CAF.
Si unajua Simba nayo iliacha wachezaji wengi sana na ikaingiza wachezaji wengi wapya?
Kikosi bado hakijakaa vizuri.
 
Unaweza ukaona hivyo,lkn sio Kila Pesa ya azamu anqpeleka kwenye timu.
Sasa naona kuhusu nafasi ya nne ya ubora unataka kupingana na CAF.
Wao ndio wameiona Simba hii hii ya akina Ahoua ni Bora na wakaipandisha toka nafasi iliyokuwepo kabla Hadi nafasi ya nne.

Nyakati hazifanani ukisema kikosi Cha 2020 lilikua Bora kuliko hiki yapo mambo yanayosababisaha iwe hivyo,mojawao ni wachezaji wale kuachwa kwa sababu ya kushuka uwezo kutokana na umri na kitumika sana
Hii Simba ndio kwanza inajengwa na hunda usajili usajili ukianza watasajili wachezaji mahili.
Kumbuka Simba hii ni mpya bado inajengwa.
Basi wewe utakuwa Sio Muelewa.
Takwimu za CAF hazichukuliwi za Msimu mmoja.

Simba walipata Alama nyingi miaka 4 iliyopita Simba ya akina Chama, Miqueson, Mugalu, Lwanga wawa nk.

Tunahitaji wachezaji wanaofanana na Timu yya nne kwa Ubora Africa.
 
Si unajua Simba nayo iliacha wachezaji wengi sana na ikaingiza wachezaji wengi wapya?
Kikosi bado hakijakaa vizuri.
Usinibishie Mimi nakaa na kuishi na Viongozi.

Msimu ulipoanza tu nikawaambia Tuna shida Kubwa sana ya No 10 kiungo Mchezeshaji wa timu wakabisha weweeeee baadaye wakakubali.


Dirisha Dogo wakaahidi kuleta wachezaji watatu wa Maana.
Baadaye wakaleta mpanzu peke yake.

Sasa tunapowaambia simba inashida ya Quality unabisha
 
Basi wewe utakuwa Sio Muelewa.
Takwimu za CAF hazichukuliwi za Msimu mmoja.

Simba walipata Alama nyingi miaka 4 iliyopita Simba ya akina Chama, Miqueson, Mugalu, Lwanga wawa nk.

Tunahitaji wachezaji wanaofanana na Timu yya nne kwa Ubora Africa.
Sawa lakini nafasi ya nne wameingia baada ya kuitoa Al Masry na kutinga nusu fainali au nakosea?
Kwa hiyo hiyo nafasi ya nne imeingia Simba hii ya akina Ahoua baada ya kutinga nusu fainali.kwa hiyo nao Wana mchango wao,huenda huko mbele watakuja wachezaji wengine wakaiingiza Tatu Bora.
 
Usinibishie Mimi nakaa na kuishi na Viongozi.

Msimu ulipoanza tu nikawaambia Tuna shida Kubwa sana ya No 10 kiungo Mchezeshaji wa timu wakabisha weweeeee baadaye wakakubali.


Dirisha Dogo wakaahidi kuleta wachezaji watatu wa Maana.
Baadaye wakaleta mpanzu peke yake.

Sasa tunapowaambia simba inashida ya Quality unabisha
Tofautisha kubisha na maoni hayo ni maoni Yako na Mimi haya ni maoni yangu.
Mwisho wa siku tunaweza tukakubaliana ama tusikubaliane.
Bahati mbaya humu hatuonani,unaposema nisikubishie kwa sababu unakaa na Viongozi unajuaje pengine Mimi nimeajiliwa na club ya Simba katika nafasi Fulani?
Mie napenda maijadala ya kiungwana.
 
Wala Sina mashaka na haya niliyoyaandika.
Simba inaenda kufunzu kuingia fainali mbele ya Stellenbosch Tena akiwa kwao.
Ndugu zangu Tuache kukalili kua kucheza nyumbani ndio kigezo Cha ushindi.
Ukweli ni kwamba katika soka matokeo ni popote pale.
Hivyo mechi ya marudiano Simba anaenda kumtoa Stellenbosch kwa namna yoyote Ile,iwe ni kwa kumfunga goli jingine au magoli zaidi au hatua ya penati.
Siongei kama mtabiri Bali mtafiti.

Sababu zangu za Simba kusonga mbele ni hizi:

Kwa kuangalia harakaharaka hua tunaona kucheza nyumbani ni faida,lakini ukweli kucheza nyumbani pia ni hatari sana:

timu hua inatakiwa icheze kwa tahadhari sana isiruhusu goli na ipate magoli,Sasa hii hua sio rahisi na inapelekea kufanya makosa mengi na kusababisha timu kufungwa.
Stellenbosch anayo kazi hapa.

Hakuna ushahidi kua tumu ikicheza nyumbani ni lazima ishinde,Kuna timu nyingi zimefungwa ama zimetolewa kwao,mfano Yanga wametolewa juzi TU hapa.

Simba tulitolewa na Waydad hapa,
Simba tulitolewa na timu ya Botswana hapa.
Zamalek tuliitoa kwao,na Zamalek imetolewa na Stellenbosch kwao.

Kwa viwango vya Simba safari hii inao uwezo wa kuforce droo ya bila kufungana kwao.

Stellenbosch ni timu Bora saizi ya Simba,lkn sio timu ya ngumu na ya kutisha kiasi hicho,Simba wanawaweza.

Simba alikua ana kazi sana Jana ya kujilinda na kuhakikisha anapata ushidhi,hapa ameweza, akienda huko ni kama vile Hana Cha kupoteza,anauwezo wa kuwakeep bize Stellenbosch kwa kuwashambulia mfululizi na kujilinda,ambao muda wote nao watakua wanajilinda kuepuka kufungwa Tena.

Simba hii inauwezo wa kupata goli zaidi ya moja huko, huko,kosakosa zilizotokea Jana ni sababu ya Presha na inaonesha defense ya Stellenbosch inapenyeka na kosakosa hizi zinarekebishika.

Kama wao waliweza kuwafunga Zamalek kwao,kwa Nini Simba tushindwe kuwafunga wao kwao?
Kwani wao Wana ukubwa Gani wa kushindwa kufungwa kwao?

Simba mchezo huu wa marudiano wataucheza kama Fainali yenyewe, maana Wana akiba ya goli moja mikononi,mwenye Hali ngumu ni Stellenbosch.

Simba inauzoefu wa kucheza popote Afrika.
Zamani tulipokua tukizifunga kwa Mkapa timu za Kaskazini,walikua wakitufunga mengi kwa hila tukienda kwao.
Lakini Siku hivz timu zetu ziligundua fitina,njama na hujuma zote hizo. Tumejifunza na hii imetupa uzoefu.

Kuwa na kocha kutoka SA nayo ni faida nyingine Kwa Simba kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na hujuma nje ya uwanja,kuyajua mazingira na kuwatia moyo wachezaji wa Simba.
Haihitaji kupokelewa na wapinzani wa Stellenbosch wa huko,kama vile wanavyofanyaga wapinzani wa Simba pale timu za nje zikija kwetu, bali Fadlu na wasaidiIzi wake wanatosha.

Kumbuka Fadlu ana jamaa zake huko.
Bila kusahau Kuna Watanzania wengi wanaishi SA kwa ajili ya sapoti,hivyo Simba hawatakua wanyonge.

Nawaona maelfu ya Wanasimba wakiwa uwanja wa ndege wa Mwalimu JK Nyerere wakiipokea timu ya Simba wakitokea Afrika kusini kwa kishindo.

Wanasimba wenzangu hii tutasonga mbele.
Simba ndiyo hivyo tena.. kule south simba hatoboiiiii
 
Mambo yamebadilika Mkuu.
Hata wao wanaamini kwamba kwao watatutoa,lkn nakuhakikishia haitakua hivyo.
Uzuri Simba Ina akiba mikononi,droo yoyote tunasonga mbele,tukipata goli moja tutakua tumewapa mlima mkubwa wa kupanda na Simba anauwezo wa kupata magoli huko.

Viwango vya kiuchezaji vya Stellenbosch na Simba vinafanana,hivyo sioni Stellenbosch kuweza kumfunga Simba goli nyingi na Simba ana uwezo wa kupata goli.
hayo mambo yamebadilika lini! baada ya ushindi mwembamba wa zanzibar?! make baada ya kipigo cha misri mlisema watakuja kwa mkapa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom