round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 667
- 2,301
Sikuwahi hata siku moja maishani kufikiria kwenda kwa waganga wa kienyeji, NEVER !! ni awatu niliokuwa nawaona hawana hadhi hata theluthi ya mtu kupeleka matatizo yake na waliownda nilikuwa nawashangaa.
Fast forward 2020 mtoto alikuwa na matatizo flani ya kiafya, mama yake (mke wangu) alinishauri sana ywende kwa mganga, hilo nilimkatalia wazi wazi kabisa.
Wife aliniambia tatizo la mtoto huwa linatokea kwa baadhi ya watu kwenye ukoo wao, mdogo wake liliwahi kumkuta lakini alitibiwa kwa mganga akapona, lakini hata hivyo nilikataa kata kata mtoto wangu haendi kwa mganga wa kienyeji.
Nilitembea na kuzunguka hospitali nyingi sana nchini na kutumia kiasi kikubwa cha pesa kwa uchumi wangu wa kawaida bila mafanikio yoyote,
Peleka kwa wachungaji apigwe maombi, peleka kwa ma ustadhi kusomewa visomo lakini wapi, kuna ustadhi flani sikuweza kumtofautisha na mganga maana chumba hakina utofauti na kalumanzila nilimwambia nitakuja ndio ikawa imetoka hio,
Muda ulienda na hali ya mtoto ilikuwa inazidi ikbaidi for the sake of my child liwalo na liwe tu, tukafunga safari na wife hadi huko kwao.
Kesho yake tukapelekwa kwa mtaalam kumfanyia tiba mtoto, nakumbuka mtoto alifukizwa alifunikwa shuka moshi mzito analia "baba nakufa, mama wananiuaa"
kama mzazi nikiri kusema chozi lilinitoka pamoja na ujasiri wangu, acheni tu jamani !!
Mtoto akafukizwa mpaka akazimia, nili panick sana nilihisi amekufa, akili ilikuwa imeniruka ila niliambiwa ndio process.
baada ya kuamka alipewa dawa ya kunywa akapigwa na vichale.
Mtoto anaendelea vizuri mpaka leo ndicho kitu pekee nashukuru lakini kila nikifikiria yale matukio na msimamo wangu wa kutokwenda kwa waganga wa kienyeji huwa nafsi inanisuta