Sijaona Tamko lolote toka Nchi za Kiarabu kulaani tukio la Kigaidi la Brussels!

Huyu bwana anachokisema ni kweli. Kumekuwepo na siasa za kinafiki katika matukio ya mauaji. Lakini kila upande una makosa kwa kuwa wakiuawa wazungu, waarabu wanaona sawa. Wakiuawa waarabu wazungu wanaona sawasawa ni haki yao kufa. Hii dunia tunapoelekea sio kuzuri, kinachotakiwa wazungu waache siasa zao za kinafiki, na waarabu waache kulipiza kisasi.
 
Heri ya Pasaka kwenu wapendwa wa jamiiforum ni matumaini yangu mpo salama kabisa!

Kuna jambo leo nahitaji kupata uelewa zaidi toka kwenu maana sometimes naweza kuwa sipo sahihi ila kwa majibu na maoni yenu naweza kupata mwangaza sahihi!

Wiki iliyopita yametokea matukio mawili ya ulipuaji wa mabomu katika mji wa Brussels huko Ubelgiji lakini cha kushangaza sijaona popote pale Mataifa ya Kiarabu yakikemea kilichotokea Brussels as if hawajasikia chochote!

Lakini swali la kujiuliza mbona akiuwawa Mpalestina mmoja pale Gaza basi Mataifa yote ya Kiarabu yakilaani kwa Kiwango kikubwa na Mataifa mengine kama Iran yakitishia kuishambulia Israel kwa makombora ya Nyuklia!

Lakini pia tumeona hata madhila wanayofanyiwa Wapalestina na Waisrael Marekani na Mataifa ya Ulaya yamekuwa mstari wa mbele kukemea mambo hayo lakini Waarabu wao wenzao wakifanya Ugaidi wanaona ni kama kawaida sana na hao magaidi hawafai kulaumiwa wala kukemewa!

Naomba kuwasilisha!
Unauliza mambo ya brussles na mataifa ya kiarabu kwa wazalendo wa Kitanzania? Hivi hii ina maana gani? Watanzania kuweni na akili msipalilie chuki miongoni mwenu kwani ikitokea nakama(dhahama) kati yetu sisi ndo tutakaopoteza. Moderator wa jamii forum hivi threads kama hizi huwa hamuzioni?
 
Acha unafiki lini ulaya na marekani wameumizwa na mauaji ya wapalestina?
Mumba huwa wanaumizwa sana binafsi hata mimi naumizwa na kinachoendelea Palestina ila je ukweli upo wapi kwenye ule mgogoro?usiangalie tu Mpalestina angalia matukio ya Hamas kuwaua Waisrael na maroketi yao je ndio njia sahihi ya kumaliza mgogoro wa mwisrael na Mpalestina?
 
Unauliza mambo ya brussles na mataifa ya kiarabu kwa wazalendo wa Kitanzania? Hivi hii ina maana gani? Watanzania kuweni na akili msipalilie chuki miongoni mwenu kwani ikitokea nakama(dhahama) kati yetu sisi ndo tutakaopoteza. Moderator wa jamii forum hivi threads kama hizi huwa hamuzioni?
Kama huna cha kuchangia futa miguu panda kitandani lala!
 
Zile drones hazipo kwa ajili ya innocent civilians zipo kwa ajili ya kuteketeza ngome za magaidi na maficho yao kosa baya wanalofanya waasi wanaounga mkono Ugaidi ni kuwatumia Raia wasio na hatia kama human shield!sasa wakati mwingine wanaenda kujificha hadi kwenye mahospitali!

Nao Magaidi wa Brussels wanadai wako kule kulipa kisasi kwa ndugu zao wanaouliwa pasi na hatia na wanafanya vile kuwaadhibu Walipa kodi wanaotoa kodi na kuchagua Viongozi Wauaji wanaouwa ndugu zao kwa kutumia Drone kwa kigezo chepesi cha kusaka Magaidi. Mbona sasa Mafunzo na mipango ya kulipua inafanyika huko huko Ulaya na husikii Drone zikishusha miji ya Paris.
Ikifika siku tukawa tunalaani na kupinga mauaji ya watu wasio na hatia bila ya kuangalia anaeua au kuuawa ni nani itakuwa ndio hatua ya kwanza ya kutokomeza Ugaidi otherwise tunapoteza muda na resource. Kuna Watu waliamini wakiangushwa Taleban, akiuwaa Osama au kupinduliwa kina Sadam ndio mwisho wa Ugaidi lakini wame prove wrong na hata Donald Trumph kawashushua kwa mbinu zao dhaifu.

"Hatutoacha kuua Ndugu zao wasio na hatia mpaka nao watakapoacha kuua ndugu zetu wasio na hatia"-Osmah bin Mohamed Bin Awadh bin laden
"Hawatoacha kuua ndugu zetu mpaka nasi tuwafikishie Uchungu na majonzi kwa kiwango sawa na kile wanachotuletea kwa kuua ndugu zetu"-Dr Ayman Alzawaheer.
Zote hizi ni kauli za kichochezi kutoka kwa Supreme Leader wa Al qaidah lakini yenye Maana kwa Muombolezaji aliefiwa na ndugu zake kutokana na Maamuzi ya Viongozi wababe na hapo ndio Visasi huanza. Hata Umkotho we Swize ya south Africa wakati wa Ukombozi ilianza kama Ugaidi lakin walipofanikiwa ndio wakaanza kuitwa Wakombozi na hata Nelson Mandela kafutwa kwenye Orodha ya Magaidi wanaotambuliwa na US baada ya kifo chake.
 
Pohamba at least nimekuelewa na nilikuwa nahitaji majibu na mawazo kama haya!
 
Heri ya Pasaka kwenu wapendwa wa jamiiforum ni matumaini yangu mpo salama kabisa!

Kuna jambo leo nahitaji kupata uelewa zaidi toka kwenu maana sometimes naweza kuwa sipo sahihi ila kwa majibu na maoni yenu naweza kupata mwangaza sahihi!

Wiki iliyopita yametokea matukio mawili ya ulipuaji wa mabomu katika mji wa Brussels huko Ubelgiji lakini cha kushangaza sijaona popote pale Mataifa ya Kiarabu yakikemea kilichotokea Brussels as if hawajasikia chochote!

Lakini swali la kujiuliza mbona akiuwawa Mpalestina mmoja pale Gaza basi Mataifa yote ya Kiarabu yakilaani kwa Kiwango kikubwa na Mataifa mengine kama Iran yakitishia kuishambulia Israel kwa makombora ya Nyuklia!

Lakini pia tumeona hata madhila wanayofanyiwa Wapalestina na Waisrael Marekani na Mataifa ya Ulaya yamekuwa mstari wa mbele kukemea mambo hayo lakini Waarabu wao wenzao wakifanya Ugaidi wanaona ni kama kawaida sana na hao magaidi hawafai kulaumiwa wala kukemewa!

Naomba kuwasilisha!
Heri ya Pasaka kwenu wapendwa wa jamiiforum ni matumaini yangu mpo salama kabisa!

Kuna jambo leo nahitaji kupata uelewa zaidi toka kwenu maana sometimes naweza kuwa sipo sahihi ila kwa majibu na maoni yenu naweza kupata mwangaza sahihi!

Wiki iliyopita yametokea matukio mawili ya ulipuaji wa mabomu katika mji wa Brussels huko Ubelgiji lakini cha kushangaza sijaona popote pale Mataifa ya Kiarabu yakikemea kilichotokea Brussels as if hawajasikia chochote!

Lakini swali la kujiuliza mbona akiuwawa Mpalestina mmoja pale Gaza basi Mataifa yote ya Kiarabu yakilaani kwa Kiwango kikubwa na Mataifa mengine kama Iran yakitishia kuishambulia Israel kwa makombora ya Nyuklia!

Lakini pia tumeona hata madhila wanayofanyiwa Wapalestina na Waisrael Marekani na Mataifa ya Ulaya yamekuwa mstari wa mbele kukemea mambo hayo lakini Waarabu wao wenzao wakifanya Ugaidi wanaona ni kama kawaida sana na hao magaidi hawafai kulaumiwa wala kukemewa!

Naomba kuwasilisha!
Ni kweli ila mimi sijajua lini nchi za magharibi zitaacha kuangusha mabomu kwenye nchi za waarabu bila kujali watu wangapi wanakufa nadhani wanachofanya waarabu ni kulipiza kisasi kama wao wanavyouwawa na kujikuta wanakuwa wakimbizi wakati kabla walikuwa wana maisha mazuri
 
Na hilo ndilo chimbuko la mauaji ya kila siku. Inawezekana kuna watu wanafurahia hii hali iwe inatokea kila siku.
 
Kwann unataka kuskia tamko la waarabu...?

Anti_Balaka wakifanya mashambulio yao hua unaskia tamko kutoka kwa nani hata la kulaani
 
Huu mjadala sasa hivi utachafua hewa. Sibanduki hapa nione wafia dini za kigeni watakavyokuwa wanaparurana
 
Ni kweli ila mimi sijajua lini nchi za magharibi zitaacha kuangusha mabomu kwenye nchi za waarabu bila kujali watu wangapi wanakufa nadhani wanachofanya waarabu ni kulipiza kisasi kama wao wanavyouwawa na kujikuta wanakuwa wakimbizi wakati kabla walikuwa wana maisha mazuri

Chanzo cha IS ni Mataifa ya Magharibi kupeleka Madege yaliyoshehena Tani za Silaha na kuanza kuyamwaga kutokea angani bila ya kujua zitamfikia nani lengo ni kuivuruga Nchi na hatimae kuuangusha utawala wa Assad kama walivyofanya Libya bahati Mbaya Waarabu wamechukua Silaha hizo hizo na sasa ndio zinatumika bara la Ulaya.

Unamwaga Silaha hovyo kwa jirani yako ili wauawane mmoja wao anachukua moja ya silaha hizo na kuja kumdhuru Mkeo halafu unataka familia ya jirani yako iomboleze Kudhuriwa kwa Mkeo ,Mimi siwezi kujisikitisha kinafkil!!!
 
Juda pale Syria anachofanya Marekani ni kuwadhibiti Isis wasizidi kujipachulia maeneo kumbuka Syria na Uturuki ni majirani na Uturuki ni sehemu ya Ulaya na pia mwanachama wa NATO kama ilivyo Marekani lazima wahakikishe ISIS wanamalizwa!
Bazoka,jaribu kufuatilia vyanzo vingine vya habari ili upate muda wa kufahamu ukweli, Marekani, Uturuki ndiyo wafadhiri wakubwa wa IS, Turkey ndio Camp ya mafunzo kwa hao magaidi. Magaidi wametengenezwa na Magharibi kuharibu nchi nyingine kwa manufaa yao. Marekani hapambani na magaidi zaidi ya kuwaimalisha kwa lengo la kufanikisha malengo yao. Ahsante
 
Itabidi hao wanaoitwa magaidi wapewe nao ndege za kivita labda sasa mapigano yatakua fair na hakutakuwa na haja ya kulaani mtu
 
Kama amavyo mataifa ya magharibi yalivyoshindwa kulaani kitendo cha Turkey kuua Wakurd holela huko kusini mashari mwa Turkey. Vivyo hivyo walivyoshindwa kulaani maauji yaliyosababisha ndege ya Urusi kudunguliwa milima ya Sinai na IS. Hilo halikukushangaza?
 
Juda pale Syria anachofanya Marekani ni kuwadhibiti Isis wasizidi kujipachulia maeneo kumbuka Syria na Uturuki ni majirani na Uturuki ni sehemu ya Ulaya na pia mwanachama wa NATO kama ilivyo Marekani lazima wahakikishe ISIS wanamalizwa!
Marekani awadhibiti watoto wake? Kichekesho hiki, ISIS Ndio mmarekani mwenyewe,
 
Kwann unataka kuskia tamko la waarabu...?

Anti_Balaka wakifanya mashambulio yao hua unaskia tamko kutoka kwa nani hata la kulaani
Kabla ya Ant-balaka walikuwa akina nani?acha unafki wewe wazungumzie Waasi wa SELEKA ambao ndio waliosababisha CAR haitawaliki sasahivi!
 
Hawezi kuzungumzia ISIS bila kuyaingiza madhehebu ya shia na Sunni na hilo ndio tatizo kuu huku upande mmoja ukiamini upo oppressed against mwenzake sasa msipoyafahamu haya mambo mtabaki kuongea msiyoyajua!
 
Back
Top Bottom