Siasa zilivyomdhulumu mzee Moi mwanamke wa maisha yake

Huwezi jua

Pengine Mzee Kenyata alikuwa anasumbua anataka Mzigio na Moi anamwambia katoe Mzigo tulinde madaraka ya Umakamu, Mama akaona isiwe shida
Huyo mwanamke naye huenda shida yake ilikuwa ushamba labda!

Amezingua!

Kwani kucheza tu kidogo kungekuwa na shida gani?

Basi angebaki nyumbani tu ili kuepukana na vishawishi

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanawake hua mkishamzoea mwanaume basi mnaanza kumjibu vyovyote tu sky
mimi hua najuta sana kuwa na mahusiano na mtu siku akinijibu mbovu

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kama mwanaume hujielewi lazima Upewe za uso,
Vijana wa sahivi hawajieelewi na hawajitambui,
Wanawake wamechoka
 
Unaona !!! Bongo huku Moi angepewa majina kibao.
Mara mariooo!
Mume bwege anakaa ukweni.
Mara zoba
 
wanawake hua mkishamzoea mwanaume basi mnaanza kumjibu vyovyote tu sky
mimi hua najuta sana kuwa na mahusiano na mtu siku akinijibu mbovu

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mwanaume ukishamwachia mwanamke balls zako akazipapasa akazipima ukubwa you are vulnerable, and this is not proportional to the size of your balls!
 
Hata ofisini mkiona bosi wote mnamwamkia 'shikamoo mzee', halafu kuna mwanamke mdogo kuliko wewe anamsalimia bosi "za saizi" ujue alishapapasa mayai kitambo!

mapenzi yana heshima mwanzoni tu, baada ya hapo anakupigia simu “upo wapi wewe ? upo na hao mahawala zako ? acha umalaya “

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
KILA mwanaume anaweza kupata mwanamke, akawa mpenzi, mke, mama wa watoto wake na wakajenga familia. Hata hivyo, kupata mwanamke wa maisha, inahitaji mwongozo wa Mungu.

Kila mwanamke anaweza kupata mwanaume. Atamwita mpenzi, mchumba na hata mume. Mwanamke kumpata mwanaume wa maisha yake, sio matokeo ya kujiendeaendea.

Hutokea mwanaume kumpata mwanamke wa maisha yake na asing'amue. Anaweza kumchezea, kumfuja hadi kumkimbiza. Tena anaweza kulaumu kuwa hajapata mwanamke wa maisha yake, kumbe alipompata alimtesa, akaondoka.

Mwanamke anaweza kumlilia Mungu kila siku kwamba hajapata mwanaume wa maisha yake. Maskini, asijue kuwa alishakuwa naye lakini alimfanyia fujo, akajiondokea zake.

Ni kweli Mungu hachoki na ana huruma sana, lakini haimaanishi ndio umlilie kila siku kwa kitu ambacho alishakupa, ukakipoteza kwa ujuaji wako. Tamaa zako. Usaliti wako. Kiburi chako. Majivuno yako. Ukicheche wako. Dharau zako. Ugomvi, ukatili na li’roho lako libaya. Shenzi!

Kabla ya kumlilia Mungu eti hajakuonesha mwenzi wa kweli wa maisha yako, tafakari maisha yako ya nyuma. Nani na nani waliingia kwenye maisha yako na wakaondoka. Pengine yupo mwanaume utamuona. Kuna mwanamke utamkumbuka. Ulimfanya nini?

Sasa, kabla ya kujiliza kwa Mungu na hilo lisauti lako lenye kutu, anza kuomba msamaha kwa kumchezea mwenzi wa maisha yako ambaye vitimbi vyako vilimshinda.

Vipi nafanania kuwa mhubiri eeh? Imempendeza Mungu nikumbushe japo hilo moja. Kisha, twen'zetu tukamuone Rais wa Pili wa Kenya, Daniel Arap Moi wa Kenya na dhuluma aliyofanyiwa na siasa, akampoteza mwanamke wa maisha yake.

Helena Bomett, ndiye huyohuyo Lena Bomett, halafu Wakenya wakammanya kwa ukaribu kwa jina la Lena Moi. Mke wa Makamu wa Rais. Ndiye Lena wa Moi. Mama wa watoto wa Moi. Mwanamke wa maisha ya Moi.

Mapenzi huwa yana fleva ya kushangaza na kusisimua sana! Moi, mtoto yatima. Lena, binti wa familia yenye fadhali kubwa. Walivyokutana, wakaishi na kupendana, ni jibu kwamba walimaanishwa kuwa mwili mmoja. Siasa zikadhulumu mapenzi yao.

Mwaka 1928, Moi mwenye umri wa miaka minne, alimpoteza baba yake, Kimoi arap Chebii. Mama wa Moi, Kabon, hajulikani alijichimbia wapi. Moi alilelewa na kaka yake.

Mwaka 1934, Moi alikuwa mmoja wa vijana wachunga mifugo kutoka mji wa Sacho, Baringo, Kenya, waliopendekezwa kujiunga na shule ya misheni ya Kanisa la African Inland (African Inland Mission ‘AIM’), iliyokuwa Kabartonjo, Baringo.

Story ya Moi na Lena inaanzia shuleni AIM. Lena alizaliwa mwaka 1926. Naye alijiunga AIM. Baba yake Lena, Paul Bomett, alikuwa mmoja wa Wakristo wa mwanzo kulipokea Kanisa la African Inland (AIC), kwenye mji wa Eldama Ravine, Baringo.

Sasa, kwa vile Moi alikuwa yatima, familia ya Bomett, ilimchukulia ni kijana wa Kanisa. Nyakati za likizo shuleni, Moi hakumudu kusafiri umbali wa kilometa 160 kwenda Sacho, hivyo aliitumia likizo yake nyumbani kwa Bomett. Nyumbani kwao Lena.

Bomett alimpa Moi hifadhi ya makazi, Moi akaanza kushawishika kupata hifadhi ya ndani zaidi kwenye moyo wa Lena. Basi ungewaona Moi na Lena wakikatiza na Biblia pamoja. Ni vijana waliompokea Yesu. Watoto wa Kanisa. Walihubiri neno katika umri mdogo.

Lena alipokwenda Marekani kusoma, Moi aliendelea kukomaa na kitabu kwenye Kaunti ya Baringo, Kenya, chini ya Kanisa la AIC. Moi akawa mwalimu na mhubiri wa neno la Mungu. Kila mtu aliamini Moi angekuwa mchungaji na angefikia uaskofu.

Lena aliporudi Kenya, ungemkuta anaongozana na Moi kwenda ziara mbalimbali za kufundisha Kanisa. Wakati huo, Lena alishakuwa mwalimu kamili.

Ni wakati huo, ilibainika kuwa watu wa Mungu, Moi na Lena walikuwa kwenye penzi zito. Moi alikwenda Chuo cha Ualimu Kagumo, Gatitu, Nyeri, Kenya. Alipomaliza chuo, hakutaka jambo lingine lolote, isipokuwa ndoa na Lena wake.

Ndoa ilifungwa mwaka 1950. Mchungaji wa Kanisa la AIC, Erick Barnet, ndiye aliyesimama kama baba wa Moi, kwa vile alikuwa yatima. Zaidi, mchungaji Barnet ndiye aliyemgharamia Moi elimu yake yote. Alimlipia mahari. Alimjengea nyumba ya kwanza ya Moi.

Miaka mitatu baada ya ndoa, Moi na Lena walipata watoto wawili, Jennifer na Jonathan. Kisha walifuata wengine mpaka kutimia nane. Gideon ndiye kitinda mimba wao.

Lena aliacha ualimu, akabaki mama wa familia ili alee watoto na kumhudumia mume wake, Dani wake. Moi alilitumikia Kanisa, kisha akatekwa na siasa. Akashiriki harakati za kudai uhuru wa Kenya. Lena alikuwa naye bega kwa bega.

Mwaka 1963 aliposhinda ubunge alikuwa na Lena. Moi alipojiunga na Kanu ya Mzee Jomo Kenyatta kutokea Kadu, alitokea kuwa kijana pendwa wa Mzee Kenyatta. Moi angefanya chochote alichoagizwa na Kenyatta.

Moi ni wa jamii ya Kalenjin na Kenyatta ni Mkikuyu. Utiifu wa Moi kwa Kenyatta ukafanya Wakalenjin wamzodoe kuwa alinunuliwa na Wakikuyu. Wakenya wana ukabila sana. Mwaka 1967, Moi akawa Makamu wa Rais wa Kenya.

Ungemuona Lena kama mke wa Makamu wa Rais, akitokeza kwenye uso wa jamii katika matukio mbalimbali. Mwaka 1968, Lena aliongoza jopo la wenyeji kutoka serikalini kumpokea mke wa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Marekani, Hubert Humphrey.

Humphrey aliongozana na mkewe Kenya, katika ziara ya “kusikiliza na kujifunza” Afrika. Ni kutokana na uhusika wa kijamii ambao Lena aliuonesha kama mke wa Makamu wa Rais Kenya, Mzee Kenyatta alimtunuku medali ya Moyo wa Dhahabu, yaani Order of Golden Heart.

Maisha yalikuwa murua mpaka mwaka 1974. Mwandishi wa Uingereza, Andrew Morton, katika kitabu chake cha wasifu wa Moi, kinachoitwa “The Making of An African Statesman” anaeleza kuwa mapambano ya kisiasa ya Moi dhidi ya mahasimu wake, yaliingiza dosari ndoa yao.

Hata hivyo, Morton katika kitabu chake, ameandika kuwa tukio la sherehe ya chakula cha jioni, iliyofanyika Chuo cha Ufundi cha Rift Valley, Eldoret, ndilo lilihitimisha ndoa ya Moi na Lena mwaka 1974.

Kwa mujibu wa Morton, wakati wa hafla hiyo, Mzee Kenyatta alimfuata Lena, akaomba wacheze muziki pamoja. Katika hafla hiyo, Moi pia alikuwepo, vilevile mke wa Kenyatta, Mama Ngina.

Morton ameandika kuwa zipo taarifa kwamba Lena alimkatalia Mzee Kenyatta kucheza naye. Wakati huohuo, picha za Lena akicheza na Mzee Kenyatta zipo kama kumbukumbu. Pia, Moi akicheza na Mama Ngina.

Ukisoma vizuri kitabu hicho unapata maelezo kuwa Mzee Kenyatta alimuomba Lena wacheze muziki, Lena akamjibu vibaya. Imeandikwa “alimtukana”, kwamba Lena kama mwanamke aliyelelewa katika misingi ya Ukristo, aliona kucheza muziki na mwanaume asiyekuwa mumewe ni dhambi.

Utapata tafsiri kuwa Lena alikubali baadaye kucheza na Mzee Kenyatta kwa kulazimishwa. Na hilo ndilo liliwagombanisha. Kwamba Moi alikuwa mtiifu mno kwa Mzee Kenyatta kiasi cha kuwa tayari kufanya chochote ili kumfurahisha. Na kwa utayari huo aliamua hata kutofautiana na mkewe. Lena alichukia kulazimishwa kucheza na Kenyatta. Moi alichukia kitendo cha Lena kugoma kucheza na Kenyatta.

Ni kwa tukio hilo, Lena aliona mume wake anaona siasa ni muhimu kwake kuliko yeye mkewe na familia yao. Alikuwa tayari kumridhisha Kenyatta na kumuudhi yeye mkewe. Lena akaondoka kwenye jumba la Makamu wa Rais, akaenda kuishi shambani. Akaachana na Dani wake. Waliyetoka mbali.

Kwa mujibu wa Morton, Lena alipokwenda kuishi shamba, alisema ndio nyumba ya familia na aliweka chumba maalum kwa ajili ya Moi. Alisema kuwa mara Moi angemaliza mambo yake ya siasa, angerejea nyumbani kwa familia, waishi tena.

Lena na Moi walitalikiana rasmi mwaka 1979. Lena hakuolewa tena. Aliishi maisha ya ukimya. Hakutokeza tena kwenye uso wa jamii. Hata kwenye ndoa za watoto wake na Moi, hakutaka aonekane kwenye kamera. Lena alifariki dunia mwaka 2004. Miaka miwili baada ya Moi, Dani wake, kustaafu Urais.

Mwaka 1978, Mzee Kenyatta alifariki dunia, Moi akawa Rais. Moi hakuoa tena, aliishi bila mke hata alipokuwa Rais wa Kenya kwa miaka 24. Na alibaki hivyo mpaka mauti yake akiwa na umri wa miaka 95.

Moi anazikwa leo nyumbani kwake, Kabarak. Wakati akilazwa kwenye kihifadhio chake cha dawamu kwenye tumbo la ardhi, tunakumbuka pia jinsi alivyoendekeza siasa, nazo siasa zikamdhulumu penzi lake, zikamtenganisha na mwanamke wa maisha yake. Lena wake. Mwanamke mrembo na sura yake ya duara. Hatimaye wote sasa hawapo duniani.

Labda wataonana na kuombana msamaha. Labda watapendana tena. Labda hawatagombana tena, maana kwa Mungu hakuna siasa. Nani anajua?

Credit:
Luqman MALOTO

Image may contain: 4 people
Image may contain: 2 people, people standing
 
CREDIT: Luqman MALOTO

Didn't he make a secret pact we devil? People sacrifice something less for something that they think could worth more. In politics and business, some people, because of making alliances or loyalty, they can even sell their own souls to devil, and it backfires.
Am not saying that is what the old man did, but learning later in this life, we creatures of world, differ very much on our approach to different things
 
Back
Top Bottom