Si kosa la jinai kusafiri na pesa ili mradi tu zisidi USD10,000

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,719
215,833
Unaposafiri na kiwango kikubwa cha pesa ni lazima uwe na ushahidi wa chanzo cha pesa hiyo. Usisahau kuchukua pay slip au salary slip. Kwa usalama zaidi wengine wanachukua na copy ya mkataba wa ajira.

Kuna wanaosafiri na USA$ 4,000 -5,000 si ajabu ni watu wamekupa uzifikishe nyumbani. Wengine pesa hii inachukuliwa na watu wa Custom Duty. Wao wanazuia mzunguko haramu wa pesa.
 
Kuna sheria maalum za kusafiri na pesa tasilimu ila wengi hawazijui
Niliona documentary, kuna mdada wa ki-China alikua na $9,000 cash amezigawa kwenye hand bag, 2.500 kwenye mfuko wa ndani wa handbag, 2,000 kwenye wallet na 4,500 kwenye hand luggage.

Wazee ilikua waondoke nazo lakini ilikuja kuwa confirmed ni muajiriwa na kampuni yake.
 
Nadhani mtoa mada hajaspecify kuwa iyo sheria niya nchi gani.
Hiyo ni Sheria ya Marekani, na kwa international flights, yaani ukitaka au kuingia US, hutakiwi kuingia na kiwango kinachozidi USD 10K, na ukitaka kufanya hivyo, kuna fomu maalumu unatakiwa kujaza fomu ( FinCEN Form 105).

Hata hivyo, kiwango kama hicho kimekuwa adopted na nchi nyingi duniani, including Tanzania.

NB: Kwa ndani hakuna limit lakini ukienda benki (Tanzania) na kutaka kuchukua pesa nyingi, sheria butu inakutaka utoe taarifa polisi ili upewe escort(unalipia) !

Sina hakika kama kiwango kimebadilishwa manake kwa muda mrefu kilikuwa ni kiwango kilichowekwa enzi za Nyerere ambacho, kwa mujibu wa kiwango kile, basi 99.9% ya wananchi wanaoenda benki walitakiwa kwenda na polisi!

ANGALIZO: Kwa wafanyakazi wa serikali kama vile Cashiers na wale wa Bank, kama vile Supervisor or Bank Tellers wanatakiwa kuizingatia sana hiyo sheria.

Ikitokea government officials umeenda benki na kuchukua mpunga, kisha ukaporwa na majambazi, uchunguzi utaanza kwa kuangalia ikiwa ulienda benki na police escort!

Aidha, aliye-authorize cheque pale benki pamoja na Bank Teller aliyelipa, wanaweza kujikuta matatani kama walilipa cheque bila kuwa endorsed na police kuonesha kwamba kuna escort!
 
Mbona wahindi hupita na mabegi ya dollar pale JKNIA hii imekaaje kifundi?
 
Unaposafiri na kiwango kikubwa cha pesa ni lazima uwe na ushahidi wa chanzo cha pesa hiyo. Usisahau kuchukua pay slip au salary slip. Kwa usalama zaidi wengine wanachukua na copy ya mkataba wa ajira.

Kuna wanaosafiri na USA$ 4,000 -5,000 si ajabu ni watu wamekupa uzifikishe nyumbani. Wengine pesa hii inachukuliwa na watu wa Custom Duty. Wao wanazuia mzunguko haramu wa pesa.
SI kosa per se. Ila ni lazima ku-declare pale Customs vinginevyo wakikubaini wanaweza kutaifisha
 
Mkuu kwa faida ya wengi ungeiweka hapa ili itusaidie.
Locally tuna sheria ya zamani sana na nadhani haijawahi kubadilishwa. Ninachokumbuka wayback 1993 kuna mtu aliibiwa milion moja ndani mwake. Mwizi akapatikana lakini mwanasheria wa mwizi akaja na hoja ya kumiliki tasilimu.

Kumbe ni kosa kisheria kuwa na Tsha 50,000 ndani ya nyumba bila kupeleka bank! Sijui kama hii sheria bado inafanya kazi

Kimataifa
Federal law requires a person to report cash transactions of more than $10,000 by filing IRS Form 8300 PDF, Report of Cash Payments Over $10,000 Received in a Trade or Business.

Mwaka 2011 tulitaka kuhamisha usd 300,00 toka Hong Kong kuja bongo siwezi kusahau timbwili tulilopitia kuna mchakato mrefu na mgumu.

Sasa hivi huwezi kwenda nje kununua kitu ukabeba mahela yako cash bila kuripoti kwenye mamlaka utapata tabu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ukiwa umebeba kias zaid ya $10k wakizikamata wanapeleka wap?kwa sababu hawasemagi wakizikamata wanazipeleka wap.
 
ukiwa umebeba kias zaid ya $10k wakizikamata wanapeleka wap?kwa sababu hawasemagi wakizikamata wanazipeleka wap.
Zinatakiwa kuingia kwenye mfumo wa serikali baada ya muda wa kuwasilisha ushahidi wa u halali wake kupita.
 
Mbona wahindi hupita na mabegi ya dollar pale JKNIA hii imekaaje kifundi?
Wahindi na fweza ni Kama tu wamasai na upanga (a.k.a. sime).
Masai akikatiza pale samora na sime, rungu, mkuki, nk ni sawa tu. We ukimuiga siku hiyo utalala lupango🙄
 
Back
Top Bottom