Serikali yasaini mkataba wa Bilioni 30 kukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa

TV za kisasa huko kwa wenzetu ktk viwanja huwa ni kama 1b za kitanzania, tena hapo inafungwa mpya. Sembuse kufanya repair hapo? Mbona kipindi cha nyuma ilkuwa inafanya kaz? Cost za pale ni repair ndogondogo tu.

Kuna watu hii mada imewazidi upeo, ni bora wangekaa kimya. Nakubali kuwa marekebisho yote hayo yamkini haizid 5b.
Viti 60,000 kila kiti kimoja ni 70,000.

Mashine za ukaguzi eneo la kuingilia uwanjani.

Mashine za ukaguzi eneo la kuingilia majukwaani.

Kuondoa Pitch yote.

Marekebisho kwenye mifumo mizima ya umeme, taa mpya, CCTV za kisasa.

Mifumo ya Maji, Vizuizi katika ya Jukwaa moja na jingine.

Marekebisho kwenye Run ways.

Marekebisho kwenye sehemu za kukaa wachezaji na benchi la ufundi.

Urekeibishaji wa Paa nk.

Hiyo Bil 5 unanunua VITI TU bila hata kufungwa na ukumbuke hapo hakuna VAT.
 
Serikali imetangaza kuanza Ukarabati wa Uwanja wa Taifa "Uwanja wa Mkapa" kwa gharama ya Tshs. Bilioni 30. Uwanja huo haujakarabatiwa kwa miaka 16 tangu uzinduliwe mwaka 2007.
20230729_233504.jpg

Chanzo kimeeleza kuwa, Marekebisho makubwa yamepangwa kufanyika ikiwemo kubadilisha viti vyote, kubadilisha mifumo ya Taa, Stadium TV Screen, Eneo la kukimbilia na kuweka Mabenchi ya Kisasa ya Wachezaji.

Lengo la marekebisho hayo ni kuboresha miundombinu ya Uwanja kuendana na wakati wa sasa ili kutoa burudani stahiki kwa Wadau wa Soka Nchini na walioko Nje ya Nje.

Uwanja wa Mkapa ulizindulwa rasmi mwaka (2007). Mpaka kukamilika uligharimu kiasi cha $ 56 Million sawa na zaidi ya Tshs Bilioni 137.
images - 2023-07-30T001915.315.jpg
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Yakubu amesema Serikali ya imetoa Tsh 30 𝘽𝙄𝙇𝙇𝙄𝙊𝙉 kwa ajili ya kuufanyia ukarabati uwanja wa Mkapa.

Amesema maboresho hayo yatafanyika katika maeneo ya kuchezea, vyumba vya wachezaji na kutoa viti vyote vya uwanja huo.

Uwanja wa Mkapa ulizindulwa rasmi mwaka (2007). Mpaka kukamilika uligharimu kiasi cha $ 56 Million sawa na Tsh 137+ 𝘽𝙄𝙇𝙇𝙄𝙊𝙉.

===
View attachment 2700662
View attachment 2700663
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharimu zaidi ya Sh. bilioni 31 hadi kukamilika Julai 2024.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam Julai 27, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chana baada ya kusaini mkataba na kampuni BCEG ya China ambao pia ndio waliojenga uwanja huo.

Alisema lengo la kukarabati huo ni kufikia viwango vya Chama cha Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Pamoja na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili uendelee kuwa bora zaidi.

"Wito wangu kwa kampuni ya BCEG, hakikisheni kazi hii mnayoifanya iwe ya viwango vinavyowekwa iendane na ubora na viwango vya CAF na FIFA na ikamilike kwa wakati” amesema Dkt. Chana.

Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Said Yakubu amesema uwanja huo utafanyiwa marekebisho katika eneo la vyumba vya wachezaji, chumba cha waandishi wa Habari, eneo la watu mashuhuri (VVIP), kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo, ubao wa kuonesha matokeo, kuweka mfumo mpya wa TEHAMA, kubadilisha eneo la kuchezea na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.

Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba, mfumo wa umeme, mfumo wa sauti, eneo la kukimbilia wanariadha, chumba cha VAR, lifti mbili mpya, mfumo wa taa, mfumo wa maji taka, mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu.

Aidha, Katibu Mkuu Yakubu ametoa wito kwa watumiaji wa uwanja huo wakiwemo mashabiki, kuhakikisha wanatunza miundombinu ya uwanja huo ili iendelee kutumika kadiri ilivyopangwa na kuendelea kuwa eneo la watanzania kupata burudani wakati wa kuangalia mechi mbalimbali na nchi jirani wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani.

Katika kufanikisha ukarabati huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) watatoa viti vipya vitakavyotumiwa na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa akiba wakati mechi uwanjani hapo na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) litagharimia matengenezo ya eneo la kuchezea mpira katika uwanja huo.
 
Justification ya matengenezo tunaiona 😂😂😂😂 maana kwa mvua hizi za dar zinawahumbua tuu mbona
 
Huu mkataba umesainiwa July 2023, hivi sasa ni November 2024, uwanja bado unakarabatiwa! muda huo uliotumika ungeweza kujenga uwanja mpya na kuumaliza🚮
 
Back
Top Bottom