Superintendent kimura
JF-Expert Member
- Feb 24, 2023
- 324
- 1,238
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Yakubu amesema Serikali ya imetoa Tsh 30 π½ππππππ kwa ajili ya kuufanyia ukarabati uwanja wa Mkapa.
Amesema maboresho hayo yatafanyika katika maeneo ya kuchezea, vyumba vya wachezaji na kutoa viti vyote vya uwanja huo.
Uwanja wa Mkapa ulizindulwa rasmi mwaka (2007). Mpaka kukamilika uligharimu kiasi cha $ 56 Million sawa na Tsh 137+ π½ππππππ.
===
Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imesaini mkataba wa makubaliano ya ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya China ambao utagharimu zaidi ya Sh. bilioni 31 hadi kukamilika Julai 2024.
Hayo yamesemwa Dar es Salaam Julai 27, 2023 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Pindi Chana baada ya kusaini mkataba na kampuni BCEG ya China ambao pia ndio waliojenga uwanja huo.
Alisema lengo la kukarabati huo ni kufikia viwango vya Chama cha Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) Pamoja na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili uendelee kuwa bora zaidi.
"Wito wangu kwa kampuni ya BCEG, hakikisheni kazi hii mnayoifanya iwe ya viwango vinavyowekwa iendane na ubora na viwango vya CAF na FIFA na ikamilike kwa wakatiβ amesema Dkt. Chana.
Naye Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw. Said Yakubu amesema uwanja huo utafanyiwa marekebisho katika eneo la vyumba vya wachezaji, chumba cha waandishi wa Habari, eneo la watu mashuhuri (VVIP), kubadilisha viti vyote vya kukalia mashabiki uwanjani hapo, ubao wa kuonesha matokeo, kuweka mfumo mpya wa TEHAMA, kubadilisha eneo la kuchezea na seti mbili za magoli ambazo zitatumika uwanjani hapo.
Maeneo mengine ambayo yatafanyiwa ukarabati ni viti vya benchi la ufundi na wachezaji wa akiba, mfumo wa umeme, mfumo wa sauti, eneo la kukimbilia wanariadha, chumba cha VAR, lifti mbili mpya, mfumo wa taa, mfumo wa maji taka, mgahawa pamoja na vitu vingine ambavyo vimepita muda wa matumizi kwani vilitakiwa kutumika kwa muda wa miaka saba tu.
Aidha, Katibu Mkuu Yakubu ametoa wito kwa watumiaji wa uwanja huo wakiwemo mashabiki, kuhakikisha wanatunza miundombinu ya uwanja huo ili iendelee kutumika kadiri ilivyopangwa na kuendelea kuwa eneo la watanzania kupata burudani wakati wa kuangalia mechi mbalimbali na nchi jirani wanautumia kama uwanja wao wa nyumbani.
Katika kufanikisha ukarabati huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) watatoa viti vipya vitakavyotumiwa na benchi la ufundi pamoja na wachezaji wa akiba wakati mechi uwanjani hapo na Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) litagharimia matengenezo ya eneo la kuchezea mpira katika uwanja huo.