Serikali yamnyang'anya Karakana ya Ndege mwekezaji Uwanja wa Kilimanjaro(KIA)

kutaka na kuwa ni vitu viwili tofauti ATCL ina ndege moja so far
 
Ni
kutaka na kuwa ni vitu viwili tofauti ATCL ina ndege moja so far
kweli,wana ndege moja aina ya DH-8 na moja ya kukodi toka South Africa aina ya CRJ-100...Lakini mkakati ni kununa ndege aina ya A320 sita.Hatua za kujiandaa ni pamoja na kuirudisha KIMAFA mikononi mwa serikali na kuiondoa kwa Suzy,lile jengo lina ofisi zaidi ya 500 kama unajua,Serikali kujenga Karakana kama ile tena kwa sasa ni ghalama sana,hata hiyo $3,000 kwa Hangar kama ile ilikuwa ni swa na bure tu.Hata Suzy mwenyewe hana ndege ila anatumia ndege ambazo anafanya handling au zinazokuwa na Technical landing au Parking ya zile zenye night stop tu...Tulizoea vya bure kwa mgongo wa serikali iliyolala...Wamekuja wasiokuwa na ubia na mtu
 
ok,...i understand...
but some one asked whether she is tanzanian or not..so that was th answer...
 
Kuna ongoing strategy ya Precision kufanya kazi kama Via Aviation. Kutokana na kupungua kwa mtaji na ufanisi mpaka mzee shirima kuuza hisa zake kwa KQ. Isije ikawa figisu zimeanza iki suzzy akae pembeni. Maana ukweli kuhusu Precision kumilikiwa na madon wa kichaga na shemeji yao
 
Kuna wazee nawafahamu wastaafu wa jeshi la wananchi tanzania, waliokua na proposal ya kujenga hanger yao hapo, lakini kwa mizengwe mpaka leo wameachwa kuzurura tu mitaani, inashangaza sana kuona ni kwa namna gani watumishi wazalendo kama hawa wanasahaulika baada ya kustaafu ukizingatia kua wanaujuzi mkubwa katika kufanya matengenezoa ya ndege, nakumbuka JK alishawahi kufungua huu mradi kule kisongo, lakini mpaka sasa wastaafu hawa wamekwama, nadhani it is a high time kuwakumbuka na kuwapa tenda watu wenye nia na weledi wa kufanya hivyo.
 
Hivi ndugu zangu nyinyi mnazungumzia ile hangar ya kia lakini mbona hamzungumzii kiwanja cha ndege cha kia? kwanini serikali ilikodisha kwa kampuni binafsi ya nje [kukiwemo na watz walitengeneza dili]?
Hivi kweli kulikuwa na haja ya kufanya hivyo? mbona matangenezo yote, uwekaji wa vifaa na ukarabati ulikuwa ukigharimiwa na serikali? Ile ndiyo ilikuwa biashara kichaa kabisa na haikuleta tija kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…