SNAP J
JF-Expert Member
- Dec 26, 2013
- 7,088
- 8,003
Kwa wale wahenga nafikiri wote tutakuwa tunakumbuka kilichotokea Mashariki ya Kati tarehe 7 Oktoba mwaka 1973 katika vita iliyojulikana kana Yom Kippur war auvita ya Oktoba ambapo Egypt, Syria, na mataifa mengine ya kiarabu walipoamua kuivamia Israeli kwa kushtukiza.
Mgogoro huo ulikuwa na madhara makubwa sio tu kwa mataifa hayo yaliyokuwa yakipigana, lakini pia kwa karibu dunia nzima, hasa baada ya baada marekani kuamua kuisadia Israeli. Madhara hayo ni kama ifuatavyo;
i).Vikwazo vya mafuta( oil embargo): Tarehe 17 Oktoba 1973, Jumuiya ya mataifa ya nchi za Kiarabu zinazouza mafuta zaidi duniani (OAPEC) kama Saudi Arabia, Kuwait nk. kama kuonyesha kuchukizwa na hatua ya Marekani kuamua kuisadia Israeli, waliamua kuziwekea vikwazo vya kuizuia mafuta Marekani na washirika wake. Marufuku hii ilihusisha kupunguza uzalishaji na mauzo ya mafuta kwa nchi hizi.
ii).Kuhathiriwa kwa minyororo ya ugavi wa mafuta (supply disruptions of fuel). Kulitokea usumbufu mkubwa katika usambazaji wa mafuta duniani maana mapigano yalisababisha kupungua kwa uzalishaji na usafirishaji wa mafuta.
iii). Mtikisiko kwenye soko la mafuta duniani: Marufuku ya OPEC na kuathirika katika minyororo wa usambazaji mafuta duniani ulisababisha hofu kwenye soko la mafuta ulimwenguni. Wasiwasi kuhusu upungufu wa mafuta na usumbufu katika minyororo ya usambazaji wa mafuta ulisababisha ununuzi wa kubahatisha na kuongezeka kwa haraka kwa bei ya mafuta duniani.
Madhara haya yote kwa pamoja ndani ya miezi michache tangu kuanza kwa mzozo huo yalipekea kuongezeka kwa bei ya mafuta mara nne zaidi. Hapa kama mtakumbuka vizuri nchi maskini zaidi duniani, kama vile za barani Africa haswa zinazopatikana Kusini mwa Jangwa la Sahara, mfano, Tanzania, ziliadhirika vibaya mno. Bidhaa zote zilipanda bei. Seriakli ya Mwalimu ikashindwa hata kuagiza madawa, vipuli vya mashine na bidhaa nyingine muhimu. Uchumi wetu uliokuwa ukikua vizuri ghafla ukaporomoka. misaada nayo ikapungua kutoka nchi wafadhili na marafiki wa Tanzania, mfano Nordic countries kama vile Norway, Dernmark na Uholanzi.
Sasa kinachoendelea sasa hivi huko Israeli kinafanana kwa kiasi kikubwa kabisa na hayo yaliyotokea miaka 50 iliyopita. Tiyari United States Secretary of Defense Lloyd Austin ameshatimiza ahadi yake aliyoitoa kwa Israeli kwa kupeleka silaha. Hamas’s Gaza commander Deif keshawasihi nchi za kiarabu Arabs kuungana kumpiga Israeli, wakati waajemi wao wamewapongeza na wametangaza kuwa watawasapoti wapalestina.
Wakati hayo yakitukia, leo hii taarifa kutoka BBC inasema tiyari bei ya mafuta katika sokola dunia imeshaongezeka kwa asilimia 4. (oil prices surge 4% following Israel Plestine conflict).
Je wachumi, wizara ya nishati, na serikali ya wamu ya sita kwa ujumla wamejipangaje katika hili ili yasije kutokea yaliyotokea awamu ya kwanza tena?