SoC04 Serikali iagize mafuta kwa niaba ya wafanya biashara na kuwauzia bila kodi wala tozo ili kukabili mfumuko wa bei

Tanzania Tuitakayo competition threads

mackj

Member
Jul 25, 2023
34
17
Tatizo la bei ya mafuta kupanda kila siku ukiliangalia kwa undani lina michezo mingi sana ambayo inachochewa na siasa na ukiritimba wa mifumo biashara iliyoko ndani ya koti la mgongano wa kimasilahi kati ya wafanya biashara na wanasiasa
View attachment 2993453
Picha (chanzo ) google
Hapo nyuma wafanya biashara wa mafuta walikuwa wanakichangia chama chenye dola, ambapo walikuwa wanalazimika kuanza ubeberu wa kutolipa kodi makusudi kwa kuwa wanakichangia chama mamilioni ya pesa ili kiweze kushinda chaguzi, lakini akaingia rais anayejua hiyo mifumo hayati dr. john joseph pombe Magufuli kwanza akaitenganisha Wizara ya Nishati na madini, kwahiyo Wizara ya nishati ikajitegemea na Wizara ya Madini vilevile,

Ambapo ilijulikana nani mzembe kusimamia wizara yake nasiyo kujificha kwa mwingine, hapo ndipo ikajulikana nchi hii kuna uhuni unafanywa na watu kumonita bei za mafuta kutokana na viburi tu mara wafiche mafuta ionekane hayapo, “Mara bei ya soko la dunia imebadilika”, “mara dola ya marekani imepanda”! Na lugha nyinginezo nyingi, km hizo
Udhibiti ulifanyika chini ya Rais wa wanyonge tukashuhudia mafuta ya petroli yakafika Tsh 2500 kwa lita mpka 1850 kwa lita hapo ndipo
Screenshot_20240518-010515.jpg

Picha( Chanzo) google
wengine wakahama nchi wakaenda kuanzisha biashara nchi zingine wanakoweza kuishi kihuni bila kuulizwa lolote, wengine wakafunga biashara, maana hawakuzoea kulipa kodi na walizoea kuichezea serikali wanavyotaka wakipandisha bei serikali inatetemeka sasa hayo ndio km yanaanza kurudi tena masna nawao baada ya kifo chake wamerejea.

Kinatokea nini kwenye mafuta hadi bei haidhibitiki?

Siyokweli kwamba serikali imeshindwa kudhibiti bei ya mafuta inayopelekea mfumuko wa bei ya bidhaa mbalimbali kwenye nchi na kusababisha ugumu wa maisha la hasha,
Tunayo mashirika hapa nchini yanayohusiana na mafuta mfano shirika la petroli la taifa TPDC tunayo TIPER tunayo EWURA wote hawa ni wadau muhimu kwenye kiwanda cha mafuta nchini kupitia serikali lakini hakuna wanaloshauri serikali kuhusu mbinu bora ya kuleta ahueni ya kilio cha wananchi juu ya bei ya mafuta

Screenshot_20240518-010341.jpg

Picha (chanzo) bbc
Hii inatokana na nini?
Kwasababu na wao wamegeuka wafanya biashara na wengine wako upande wa kutetea wafanya biashara kwa masilahi yao binafsi huo ndio mgongano wa masilahi wenyewe, wengine ni wamiliki wa shelly fulan fulani na wengine ni wabia kwenye makampuni ya mafuta

Mfano TPDC ina miaka karibu 25 haijaagiza mafuta kama lilivyojukumu lake kubwa na la msingi kitu amabcho kinaipa serikali mzigo wa kulipa watumishi ambao kimsingi ni kama hawana kazi ya kufanya.

Nini kifanyike ili kuwepo na ahueni ya bei ya mafuta hasa petroli nchini?

Ifahamike kuwa mfumuko wa bei unalalamikiwa na wananchi wa kada mbalimbali kwa nchi hii ni kwasababu ya bei ya mafuta kwani nchi yetu wafanya biashara asilimia 80%wanategemea usafiri wa maroli kusafirisha bidhaa zao kwenda kwenye sehemu zao za biashara kutokana na ukweli kwamba reli nchi hii iko maeneo machache sana ambapo hata katika maeneo hayo iliko reli nako treni safari zake ni za kusuasua kutokana na miundo mbinu chakavu sana hivyo kupelekea matumizi ya maroli kuwa ndio kimbilio la wafanyabiashara sasa unapokuta bei ya mafuta iko juu kwa mfano kama sasa mikoa ya pembezoni kama Mara n.k lita moja ni sh 3500, kimsingi na bei ya kusafirisha mizigo inakuwa juu ili mfanya biashara apate faida
Screenshot_20240518-234158.jpg

Picha (chanzo )sky news
Ambapo lazima katika uuzaji wa bidhaa zile acomperset na bei ya nauli iliyotokana na bei ghali ya mafuta maana mwenye roli pia anahitaji faida lazima apandishe bei ya nauli ya kusafirisha mizigo ili apate faida

Kwahiyo ni muhimu serikali ifanye kama mataifa mengine yanavyofanya ili kunusuru wananchi wao kuishi katika hali ya malalamiko na ukata mkubwa kwa kuagiza mafuta yenyewe na kisha kuyaweka kwenye bohari za TIPER na kuwauzia wafanya biashara kwa bei elekezi isiyo na kodi ikiwezekana itoze kodi moja ya ongezeko la thamani (VAT) tu hapo itawezekana kwa wakala wa udhibiti wa nishati na maji EWURA kupanga bei za mafuta lakini kwa sasa ni uongo maana mfanya biashara anagiza mafuta kwa pesa yake kisha akifika hapa anatozwa kodi zaidi 6 kwenye bidhaa moja lazima apandishe bei ya mafuta ili aweze kupata faida kwa kufidia kodi alizotozwa na serikali

Lakini kama serikali ikiagiza mafuta maana yake nikuwa, mfanya biashara hajatoa jasho katika mafuta hayo kwa gharama yoyote ile hivyo hana sababu ya kuuza mafuta kwa bei anayotaka yeye bali atauza kwa bei elekezi ya serikali
Mfano nchi ya kenya hivi karibuni bei ya mafuta ilianza kuwa changamoto serikali iliagiza shehena ya mafuta na kuwauzia wafanyabiashara kwa bei elekezi ya serikali na hata mataifa km Marekani, India, na China, wao wanaagiza mafuta kupitia mashirika ya serikali, na kisha serikali ndiyo yenye mamlaka ya kuagiza mafuta na siyo mtu binafsi au yanapewa mashirika yenye mtaji Kupitia mfumo PPP na yanapewa exemption na serikali yanaingiza mafuta serikali inayalipa mashirika hayo baada ya mafuta kuingia kwenye mzunguko, na serikali kupata kodi yake ya ongezeko la thamani na kumlipa mzabuni

Mwaka 2022 mnamo tarehe 5 mwezi may aliyekuwa waziri wa nishati januari makamba aliahidi mambo mengi sana ambayo yalishauriwa na waheshimiwa wabunge lakini mpaka leo hakuna ambalo limetekelezeka hata moja katika kufanya bei ya mafuta inakuwa himilivu kwa link hii
View: https://youtu.be/RMUqvu5uN2Q
utaweza kuona na kusikia mikakati ya serikali aliyoitoa aliyekuwa waziri wa nishati nchini tanzania

Lakini Kwa kufanya haya niliyoaanisha hapa kwa miaka mitano ijayo tutaipata tanzania tuitakayo ambayo haina chembe ya changamoto ya mfumuko wa bei wala kilio cha kudumu cha bei ya mafuta kilichojificha kwenye koti la siasa rushwa na mgongano wa masilahi
Naomba kuwasilisha
Naitwa

Makiwa Jumanne
Kwa heri
 
Mfano TPDC ina miaka karibu 25 haijaagiza mafuta kama lilivyojukumu lake kubwa na la msingi kitu amabcho kinaipa serikali mzigo wa kulipa watumishi ambao kimsingi ni kama hawana kazi ya kufanya.
Hivi kumbee, mafuta yanatakiwa yaagizwe na hao? Je ni haya mafuta ghafi au mafuta yote tu?
mataifa km Marekani, India, na China, wao wanaagiza mafuta kupitia mashirika ya serikali, na kisha serikali ndiyo yenye mamlaka ya kuagiza mafuta na siyo mtu binafsi au yanapewa mashirika yenye mtaji Kupitia mfumo PPP na yanapewa exemption na serikali yanaingiza mafuta serikali inayalipa mashirika hayo baada ya mafuta kuingia kwenye mzunguko,
Kama tayari ipo mifumo ya mfano toka nchi nyingine, vizuri tukaiga na kifanyia kazi kama iko na faida. Maana nishati ni kitu muhimu sana kuathiri maendeleo na uchumi wa nchi kwa uchanya. Ahsante Mackj
 
Hivi kumbee, mafuta yanatakiwa yaagizwe na hao? Je ni haya mafuta ghafi au mafuta yote tu?

Kama tayari ipo mifumo ya mfano toka nchi nyingine, vizuri tukaiga na kifanyia kazi kama iko na faida. Maana nishati ni kitu muhimu sana kuathiri maendeleo na uchumi wa nchi kwa uchanya. Ahsante Mackj
Bro shukrani wewe ni mdau muhimu sana katika jukwaa hili
 
Back
Top Bottom