peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 14,255
- 23,947
KUTOKANA na Hali mbaya ya uchumi, pamoja na serikali kumiliki deni la Taifa la Trilion 91, Serikali imemshinda kuwalipa Posho za madaraka ya walimu wakuu,wakuu washule,vyuo,na maafisa elimu kata pamoja na ruzuku za shule Kwa kipindi cha Mwezi Novemba na Decemba 2022.
Hali hii imekwenda mbali zaidi ambapo watumishi wa Umma wameshindwa kwenda likizo zao Za Mwisho wa mwaka kwa Serikali kushindwa kuwalipa fedha Za likizo ya Mwezi December 2022.
Hii inaonyesha tunakoelekea Serikali inaweza kukosa mishahara ya kuwalipa watumishi wake jambo ambapo ni hatari kupita Kiasi.
Tunatoa wito kwa Serikali ya CCM kuondoa aibu hii mapema kwani kumsifia mama Ana upiga mwingi wakati serikali inashindwa kuwalipa watumishi wake ni Aibu ya mwaka.
Tangu 01/11/2022 hadi sasa (28/12/2022) takribani miezi miwili serikali imeshindwa kupeleka fedha mashuleni kwa ajili ya ruzuku, na hakuna tamko lolote kutoka katika mamlaka husika.
Kushindwa kupeleka fedha hizo kwa wakati mashuleni kuna sababisha walimu kushindwa kupatiwa vifaa vya maandalizi ya kufundishia na kujifunzia shuleni.
Aidha adha hii pia inasababisha shule nyingi kuwa na mrundikano wa madeni kwa wazabuni kwani baadhi ya shule hukopa vifaa na kushindwa kulipa kwa wakati kutokana na kutoingizwa fedha hizo kwa wakati!
Tume Jaribu kupigia simu Waziri wa Elimu Adolf Mkenda, kujaribu kujua tatizo ni nini , naye alijibu kuwa Tatizo liko TAMISEMI .
Prof Mkenda alishauri Tuwasiliane na Waziri wa TAMISEMI, Waziri Anjela Kairuki ambaye yuko likizo Nchini China, Kwa mume wake na simu yake haipatikani.
Hii imejenga sura mbaya kwa chama Tawala kushindwa kuhudumia watumishi wake kwa wakati.