Serikali: Tutawafilisi Mafisadi na Wahujumu Uchumi

lile jibu la Rubada ni lini mnalitumbua
Tunaomba PCB iweze kutumbua lile jipu la yule jamaa wa RUBADA tunaona kimya tu sijui lini anafikiswa mahakamani, mali zake zinajulikana ziliko na kampuni hewa na mkewe, tunaomba mtumbue na ilo
 
Katika hatua ya kupambana na ufisadi serikali ya Awamu ya tano Imetaifisha Mali zenye thamani ya Zaidi ya billion 100 na ameomba wananchi kutoa taarifa za wale wenye Mali Zilizopatikana Kifisadi.
 
Imetaifisha mali hewa? hizi ni drama hakuna kitu kama hicho kama wana uhakika na kauli zao waweke orodha ya mali hizo na wamiliki wa mali hizo zilizotaifishwa.
 
Nimepoteza imani na Magufuli,laiti tungejua kuwa atakuja kuminya upashwaji wa habari za bunge asingechaguliwa kabisa kuwa rais.
 
Imetaifisha mali hewa? hizi ni drama hakuna kitu kama hicho kama wana uhakika na kauli zao waweke orodha ya mali hizo na wamiliki wa mali hizo zilizotaifishwa.
Orodha watoe wapi...Watawala wanajua waDanganyika wengi..wanapenda kusikia maneno matam....yasiyo naukweli wowote...ndio maana hao jamaa wamekuja....Vinginevyo...hakukuwa na maana yyt kwenda kwenye Pressconfrence... Ikiwa hawana uwezo wakutaja hata mtuhumiwa 1 kipi kimewaleta....
 
Mange Kimambi hayuko humu? Yeye anatoa live bila chenga. Wengine sisi waoga.
 
Nimeamua kusema Chenge na JK.Hayo ndiyo mawazo yangu na wewe unaruhusiwa kusema yako.
Usipende kuacha mlango wazi sababu jirani yako jana aliacha wazi kwani bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi!!!

Haya jisikie vizuri basi, mwingine ni mzee wa kurudi kijijini baada ya kushindwa licha ya ukweli kwamba hata maneno hayo ni ndoto kutimizwa. Hajazoea, hivyo hawezi. Ufisadi ni ajenda ambayo jamaa flani waliikwepa mno kuizungumza kwani ki kulacho kilikuwa nguoni mwao.
 
Huwa nachoshwa na upuuzi wa namna hii. EPA pia tuliambiwa walirudisha labda ndiyo hizo waligawana? Kwanini washindwe kuorodhesha waziwazi na kuzionyesha hadharani na kwamba kama ni mnada zipigwe mnada? Sasa Serikali ina uwezo gani wa mara moja kuzimiliki hizo mali? Au wanataka kutuambia ni akaunti wame-freeze? Hii ni dharau kwa wananchi, waweke kila kitu hadharani, ninamaanisha hadharani na waliokuwa wanazimiliki waeleweke. Kama ilikuwa ni mali ya umma imeibiwa na mtumishi wa umma, kwanini leo wamuonee haya? Huu utamaduni utaisha lini ambao haujawahi kulisaidia taifa letu kusonga mbele? Haingii akilini ni kitu gani mwizi niliyemkuta akiniibia nimemkamata ndani ya nyumba yangu akiniibia na vingine alishavifikisha nyumbani kwake, atanieleza nini ili nimfichie siri?? Au eti nimsafishe? Niendelee kusalimiana naye na kucheka naye? Hii VIRUS ya Dar-Es-salaam, haipatikani kwengineko. Ni kwetu tu Tanzania basi. Tena huenda wakateuliwa kuwa mabalozi ili kufunika kabisaa. Kama Mh. Magufuli kweli anataka tuamini wanachofanya si kiini macho, hapa ndipo wanatakiwa wajitofautishe na wenzao waliotangulia. Bila kufanya mambo wazi TUTAJUA NI KIINI MACHO TU.
 
B]View attachment 319799
Mkurugezni wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga[/B]




Tangazo hilo la serikali limetolewa leo Januari 28, 2016 na Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini, DPP, Bw. Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi(DCI), Kamishna wa Polisi, Diwani Athumani na Mkurugenzi wa Upeleelzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), wakati wa mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.

I hope watu wananisoma vizuri maana hili nililisema kama mwezi hivi nyuma... mabadiliko hayaombewi; yanaletwa!
 
Wanatumbua majipu tu kansa wanaziacha kama zilivyo. Vinara hasa wa ufisadi ndio kwanza wanazidi kukumbatiwa , mf. vijisenti.
 
Back
Top Bottom